WHO : COVID-19 bado tishio licha ya mafanikio ya majaribio ya chanjo

WHO : COVID-19 bado tishio licha ya mafanikio ya majaribio ya chanjo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Tedros Adhanom Ghebreyesus

Tedros Adhanom Ghebreyesus

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani Tedros Adhanom Ghebreyesus anasema kuna kazi kubwa inayohitajika kupambana na janga la virusi vya corona licha ya kuwepo na habari nzuri wiki hii kuhusiana na mafanikio ya majaribio ya chanjo.

Akizungumza kutoka Geneva Ijumaa wakati idadi ya maambukizo yakiwa yameongezeka kote duniani Tedros amesema chanjo ni chombo kimoja tu katika kupambana na janga hili lakini watu wasisahau masharti mengine ya kujikinga Ikiwa tunataka kutokomeza ugonjwa huu.

Idadi ya watu wanaoambukizwa kwa siku huko Rushia na Marekani zimefikia kiwango cha juu kuwahi kushuhudiwa tangu janga hili kuanza.

Rashia iliripoti kuwepo na zaidi ya watu 21,000 walioambukizwa jana pekee yake.

Huko Ulaya hali ya wasiwasi imezuka kutokana na kuongezeka maambukizo na kusababisha mataifa mengi kuanza kuchukua tena hatua kali za kudhibiti kuenea kwa virusi.

Huko ufaransa peke yake zaidi ya watu 35,000 waliambukizwa kwa kipindi cha saa 24 zilizopita.
 
Hari si hiyo tu. Corona pia imewapata wanyama wanaitwa mink

Tatizo linaongezeka hasa huko Ulaya ambapo wanyama aina ya Mink wafugwao katika baadhi ya nchi hizo wamekutwa na Covid 19. Kwa hali hii basi hawa Virusi wanabadilika, (mutation) na kuwa na uwezo wa kuhimili chanjo ambayo imetengenezwa kwa ajili ya virusi wenye vinasaba vitofauti na vyao. Kuna hatari ya kurudi tena maabara ili kutengeneza chanjo nyingine kwa ajili ya hawa wapya.
 
Tishio wapi?

Huku Ikungulyabashashi hakuna mtu mwenye time na hiyo C-19....
 
Hapa Tarime tulisahau hiyo kitu tokea tulipomaliza maombi ya Siku 3
 
Back
Top Bottom