Who created God? Who made him? Where did he come from?


Hata haueleweki!
 
nazani albert einsten na newton.walikiri..huwez jaji kitu kilichokuumba.pia ikili ya binadau ni FINITY.BUT YA MUNGU NI INFINITY..SO INFINITY KUPATA JIBU
 

Hapana

Unachanganya mambo....

Ukijua jambo fulani litatokea kesho kwa uhakika wa 100% halafu ukawa na uwezo wa kulizuia bado utakuwa hujalipanga litokee!
 
Hapana

Unachanganya mambo....

Ukijua jambo fulani litatokea kesho kwa uhakika wa 100% halafu ukawa na uwezo wa kulizuia bado utakuwa hujalipanga litokee!

Except mungu wenu anatakiwa kuwa ndiye muumba wa vyote na hakuna kinachoweza kutokea bila ruhusa yake.

Kitu kikiweza kutokea bila ruhusa yake, maana yake mungu si muweza wa yote.

Na kama kila kitu kinatokea kwa ruhusa yake, huko ndio kupanga kwenyewe.
 

Kuruhusu ni kupanga kwa maana gani?
 
Kuruhusu ni kupanga kwa maana gani?

Kwa maana ya kwamba, huyu mungu wenu haruhusu kama mwalimu mkuu anavyoruhusu mwanafunzi mtoro achapwe fimbo sita (ambazo mwanafunzi mtoro mjanja anaweza kuziepuka kwa kutoroka bila kushikwa, au akashikwa na kumbembeleza mwalimu asimchape kwa sababu alitoroka kuwahi hospitali kumhudumia mama yake aliyekuwa anafariki kwa ugonjwa hatari).

Kuruhusu kwa huyu mungu wenu mnavyosema ni kwa aina isiyopingika wala kurekebishika.

Kama vile kuruhusu binadamu aweze kuishi katila muda unaoenda mbele tu na usiorudishika nyuma.

Kuruhusu huku ni kupanga. Mungu kuruhusu muda uwe unakwenda mbele tu kwa binadamu ni kumpangia binadamu aishi katika ulimwengu ambao muda hauwezi kurudishika nyuma.

Ukisema mungu karuhusu tu muda uwe unaenda mbele na haurudi nyuma kwa binadamu, na hajapanga hivyo, una imply jwamba kuna kingine kilichopanga hivyo ambacho kipo juu ya uwezo wa mungu.

Jambo ambalo litavunja hoja ya kwamba mungu ni mjuzi wa yote na muweza wa yote.
 

kwa nini mungu hayupo ??
 
Hapa unajichanganya

Kuruhusu jambo hakuna maana ya kutowezekana

Unaweza kuruhusu mtu auwawe lakini asiuwawe kwasababu mbali mbali
Kama vile kuruhusu binadamu aweze kuishi katila muda unaoenda mbele tu na usiorudishika nyuma.
Muda unakwendaje mbele?

Huwezi kuwa na mbele bila ya kuwa na nyuma

Muda unaouzungumzia hapa ni upi?
Hii hoja yako imejengwa kwenye assumption,kama sio nioneshe muda ....!!
 
Kwa sababu anavyoelezwa anajipinga mwenyewe kwa namna isiyowezekanika kuwepo.

Kwani Kiranga ww unasemaje kuhusu asili ya dunia na viumbe vyake? Bana mwanzo au havina? Km vina mwanzo, huo mwanzo ni lini na nini asili yake? Km hivina, ww hapo km Kiranga na dunia yote mmetoka wapi?
 
Kwani Kiranga ww unasemaje kuhusu asili ya dunia na viumbe vyake? Bana mwanzo au havina? Km vina mwanzo, huo mwanzo ni lini na nini asili yake? Km hivina, ww hapo km Kiranga na dunia yote mmetoka wapi?

Siwezi kuhadaa ulimwengu kwamba najua majibu ya maswali haya.

Lakini hilo halina maana kwamba nikipewa jibu ambalo si la kweli na lenye mikingamo isiyoafikika, siwezi kulitambua hivyo.

Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hawezi kuwa na viwango vya upendo vilivyo chini ya upendo unaowezekana kibinadamu. Kwa hivyo, kama kweli ana uwezo wote na upendo wote, tungetegemea kuona ulimwengu wake ukiwa mzuri zaidi ya huu wa matetemeko ya ardhi yanayoua kqa mafungu, Ebola isiyotibika kqa watu masikini, mauaji, vita, njaa etc.

Kama mungu angekuwa binadamu mwenye uwezo wote huo anakaa Washington DC, New York, London, Dar au Dodoma, na ana uwezo wa kuzuia hayo yote, lakini hazuii tu, watu qangeandamana kumlaani, na hata kumshtaki mahakama ya The Hague kwa mauaji ya jumuiya.

Sasa inakuwaje huyu mungu mqenye uwezo mkubwa kulimo vyote kwa madai ya wengine, tumuwekee viwango vya chini kabisa vya uwajibikaji?

Huyu mungu yupo kweli au tunajisahaulisha tu kwamba kuna mambo hatuyajui na kila tusilolijua tunamsingizia mungu tusiyemjua?

Kama mungu mwenye uwezo wote na upendo wote yupo, kwa nini mabaya yapo duniani?

Ni kwa sababu sababu anaweza kuzuia ila hataki tu?

Kama ni.hivyo, je, ana upendo.wote kweli?

Au nin kwa sababu anataka kuzuia maovu lakini hawezi?

Kama ni hivyo, je anaweza yote?
 
isiyowezekenia ni nini ?

Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kuumba ulimwengu wenye mabaya kama huu.

Soma post yangu ya awali.

Mungu wenu anajipinga mwenyewe.

Kama ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, kwa nini aliumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekanika kama huu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…