BIGURUBE
JF-Expert Member
- Mar 11, 2014
- 6,748
- 4,252
Siwezi kuhadaa ulimwengu kwamba najua majibu ya maswali haya.
Lakini hilo halina maana kwamba nikipewa jibu ambalo si la kweli na lenye mikingamo isiyoafikika, siwezi kulitambua hivyo.
Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hawezi kuwa na viwango vya upendo vilivyo chini ya upendo unaowezekana kibinadamu. Kwa hivyo, kama kweli ana uwezo wote na upendo wote, tungetegemea kuona ulimwengu wake ukiwa mzuri zaidi ya huu wa matetemeko ya ardhi yanayoua kqa mafungu, Ebola isiyotibika kqa watu masikini, mauaji, vita, njaa etc.
Kama mungu angekuwa binadamu mwenye uwezo wote huo anakaa Washington DC, New York, London, Dar au Dodoma, na ana uwezo wa kuzuia hayo yote, lakini hazuii tu, watu qangeandamana kumlaani, na hata kumshtaki mahakama ya The Hague kwa mauaji ya jumuiya.
Sasa inakuwaje huyu mungu mqenye uwezo mkubwa kulimo vyote kwa madai ya wengine, tumuwekee viwango vya chini kabisa vya uwajibikaji?
Huyu mungu yupo kweli au tunajisahaulisha tu kwamba kuna mambo hatuyajui na kila tusilolijua tunamsingizia mungu tusiyemjua?
Kama mungu mwenye uwezo wote na upendo wote yupo, kwa nini mabaya yapo duniani?
Ni kwa sababu sababu anaweza kuzuia ila hataki tu?
Kama ni.hivyo, je, ana upendo.wote kweli?
Au nin kwa sababu anataka kuzuia maovu lakini hawezi?
Kama ni hivyo, je anaweza yote?
Umetaja mabaya unayosema ni mabaya kwa kiwango chako cha kufikiri, hujataja mazuri ambayo Mungu amekuwa akufanya juu yako, uwepo wako duniani ni upendo tosha aliokufanyia Mungu na sidhani km unamlalamikia kuwa kwanini alikufanya uje duniani. Kiranga nilikwambia kwa uwezo wetu wa kufikiri sisi binadamu ni mdogo sn, nilikupa mfano kuwa sisimizi ajifanye kutaka kulingana uwezo wa kufikiri na ww binadamu, hivi ni vitu viwili tofauti kabisa. Ukimfikiria Mungu in physical matter hutapata jibu, ila ukimfikiria Spiritually utafika mbali na utamuona Mungu