Who influenced Nyerere: His Ujamaa Philosophy and Azimio Principles?


Mchungaji hivi hapo 'Ivy League' ulipo hakuna makabrasha yanayoonesha jinsi gani hii 'discourse/ideology', yaani, mtazamo uliojificha wa kiitikadi wa kudai kuwa waafrika na 'watu weusi' kwa ujumla ni wavivu ulivyoanzishwa na wakoloni na wabaguzi wa rangi ili kujipa moyo kuwa ni haki kabisa kututawala na kututumikisha? Kama waafrika ni wavivu ilikuwaje tukatumikishwa sana kama watumwa kujenga miji ya Liverpool huko Uingereza, Boston huko Marekani, Cape Town kule Afrika Kusini na sehemu mbalimbali duniani? Kama sisi ni wavivu sana kwa nini tulikata sana katani kama manamba kule Tanga na kuongeza sana pato la Serikali ya Mkoloni wa Tanganyika?

Kwa kweli Mchungaji umenisikitisha sana. Kuna makala ya Ayub Ryoba inaongelea jinsi gani watu hawa hawa unaowaita wavivu hapa Bongo wanavyopiga mzigo kinoma huko Ulaya. Kaisome maana hayo maboksi mnayoyabeba huko mpate dola 7 kwa siku hapa Bongo mkiambiwa myabebe hamtakubali alafu mtaitwa mvivu. Leteni utaratibu wa kulipana kwa masaa hapa Tanzania uone jinsi madei waka watakavyopiga mzigo kama hawana akili nzuri! Yaani, kha, kweli hawa wamachinga na wabeba mikokoteni mchana kutwa kwenye hili jua kali la Dizim ni wavivu?
 
We kind of practice socialism still but we lean more towards capitalism....

what is this "socialism" and what is this "Capitalism" and how does both of them manifest themselves in sociocapitalism? What are the characteristics of sociocapitalism?
 
what is this "socialism" and what is this "Capitalism" and how does both of them manifest themselves in sociocapitalism? What are the characteristics of sociocapitalism?


Socialism is a social and economic system in which the economic means of production are owned and controlled collectively by the people whereas Capitalism utilizes the willpower of individuals, especially entrepreneurs, to foment economic activity. Capitalism is based on the assumption that individuals operate based on self interest; however, by doing so they not only help themselves, but also propel others towards economic success.

Sociocapitalism is an improved version of capitalism that corrects its weaknesses. It has the following guidelines:

1. The mechanism is based on the self-regulating supply and demand (the "invisible hands").

2. The basic principle is free competition and seeking profit (the principle of "survival of the fittest"). But it also adopts social policy to help the disadvantaged through universal healthcare, low income subsidy, etc.

3. It normally requires private ownership of capital and properties.

4. It favors free market, deregulated rather than centrally planned economy, and minimum government intervention.

5. It prevents excessive uneven wealth distribution through social policies such as ceiling of wealth or accumulative tax.

6. It adopts some regulations in regard to international trade to reduce the disadvantages of developed market due to its higher cost and to protect the emergent market from imperialism.

7. It utilizes government intervention in a mixed economy to prevent "market failure" such as the Great Depression or what is going on now with the markets.

8. It adopts regulations to prohibit immoral business practice, poor labor treatment, imperialism, etc. It also uses regulations to protect the environment from profit-driven pollution or abuse.
 

vizuri sana; sasa katika Tanzania hayo mambo nane yanaonekana vipi ili kuthibitisha kuwa tuna sociocapitalism?
 
vizuri sana; sasa katika Tanzania hayo mambo nane yanaonekana vipi ili kuthibitisha kuwa tuna sociocapitalism?

Kwa vile ndo tunaanza kujaribu ku practice sociocapitalism, ni vigumu kuthibitisha yanaonekana vipi lakini tunakoelea ndio huko.
 
Kwa vile ndo tunaanza kujaribu ku practice sociocapitalism, ni vigumu kuthibitisha yanaonekana vipi lakini tunakoelea ndio huko.

Manki acha kukimbia ligi ya Mwanavileji, hicho ni kisingizio tu - kuna vitu vingi tu vinathibitisha kuwa tunatekeleza hiyo 'third way' unayoongelea, kwa mfano:

1. Ununuzi wa mazao kwa stakabadhi ghalani
2. Uuzaji wa hisa za NMB kwa wananchi
3. Uundwaji wa mamlaka za usimamizi kama EWURA
4. Kutoa ruzuku kwa wakulima kwa kutumia fedha za EPA
5. Kutoa ruzuku ya maendeleo kwa wanafunzi kupitia PEDP
6. Kubana mfumuko wa bei kwa kununua au kutoa dola BOT
 
Mnajua kuna kitu kimoja ambacho nafahamu fika Watanzania tuliolimbukeni kutokana na kutaka ufahari wa "Uzungu Weusi".

Nilikuwa kwenye mji fulani hapa Marekani, kukawa na jamaa watatu wa Kibongo ambao walianza kazi Payless na McDonald mpaka wakafikia kuwa store managers.

Sasa Wazungukoko na vyeti vyao, wakawa wanawadhihaki hawa jamaa kuwa Umeneja gani au cheo gani kufany akazi Payless shoes au McDonald.

Nikakaa chini na kujiuliza, kwa nini tunawadharau wale wanaofanya kazi mcDonald ambako tunakimbilia kupata chakula cha bei poa na kunenepeana? What is wrong with someine to work at McDonald or Nursing home?

Hivi hawa si wanajifunza kazi na nidhamu ya kazi mpaka kuwa ma-expert wa kazi zao? Sasa sisi tuajitapa nini kuwa na vyeti huku hatuna hata ujuzi chembe wa kujua mzunguko mzima wa biashara ya mcDonald? Je hamtegemei huyu jamaa wa McDonald akipiga shule yake atakuwa na nafasi bora kwa kuwa kajifunza kwa vitendo ukiongezea darasani?
 

Mwanakijiji anakupa Thanks kama vile ameisoma. Na akisoma atajua kwanini ali-lost kusoma kipindi cha Nyerere.
 

Kujitegemea kulishindikana kwa sababu Kujitegemea hakuendani na Ujamaa. Msingi wa Ujamaa ni kutegemeana. Sio kujitegemea. The contradictory genius - or, alternatively, the incredible naivete - of J.K. Nyerere was to think that the two are compatible. They are not. Kuwa Wajamaa na Kujitegemea hakupikiki chungu kimoja. J.K. Nyerere alitaka eti tujitegemee kama Taifa. Kama Mkuu Pundit anavyosema, huwezi kutegemea watu wajitegemee kama Taifa wakati at the local level unawafundisha sera za kutegemeana. Unawachanganya. Huwezi sema sisi ni Watanzania katika international stage lakini ki loko loko sisi ni Wazanzibari na Wabara. It is such a confused Kikweterian proposition.

Mtanzania kafanya nini kwa nafsi moja au nafsi mkusanyiko kama jamii na taifa kujitegemea?

Sidhani kama tumeanza juhudi mahsusi za kujitegemea. Kiongozi wetu "Mkwere anafahamika kwa bakuli na vikengele vile vinavyovaliwa miguuni wakati wa kucheza ngoma," kuazima lugha ya Mkuu mmoja kulieleza tatizo hili. Wengine tunasema hii dhana hatutaki. Tumepinga hata taswira mbaya ya viongozi wetu kukimbilia matibabu nje ya nchi. Hususan waasisi waliohubiri kujitegemea. Bado hatujui kujitegemea maana yake nini kwa sababu tulikuwa indoctrinated kutegemeana.

Wamarekani walipopata Uhuru wao, hawakuwa matajiri usiku wa pili, walichokivuna katika miaka 200 ni matunda ya kuchapa kazi pamoja na unyonyaji.

Ni kweli. Lakini ingevumilika kama ingekuwa maendeleo nchini kwetu yanakuja taratibu. Nchini kwetu tunarudi nyuma! Waziri Ngeleja na TANESCO wanatangaza kwamba wanakata Umeme kwa sababu mashine zimezeeka. Wanatuambia kuna mashine hazijawahi kufanyiwa ukarabati toka zisimikwe siku za Ukoloni! Yaani, tunarudi nyuma! Hii hoja ya "Marekani hakuwa tajiri usiku wa pili" ni kidonge cha placibo. Ni danganya toto ya toto dogo aliyechoka na safari anaeuliza mbona hatufiki mbona hatufiki. Mama anamwambia tutafika tutafika hivi karibuni, kumbe wanazunguka zunguka pale pale na na kurudi nyuma kwa sababu Mama kapotea njia!

Marekani haikufika hapa bila kupitia misukosuko, shida au dhiki. Hata leo hii, pamoja na Utajiri wake wote, bado leo hii kuna umasikini wa hali ya juu katika baadhi ya wananchi wake kuliko hata Tanzania

Hiyo data Mkuu Kishoka, mmmmh! Isije ikawa dataz!

unaposema Maendeleo, tunamaanisha maendeleo ya namna gani? Tunapima maendeleo kwa mizani gani? ni vipengele vya namna gani? Ni maendeleo ya Uchumi tuu? what about umoja wetu?

Nadhani kuna umuhimu wa kuangalia vitu vingine zaidi ya Uchumi. Tanzania imeipita Northern Ireland kwa national stability, na hayo inawezekana tunaweza kuyaita maendeleo. Tumeendelea kuwazidi Northern Ireland, kwa kipimo hicho. Lakini historia inaonyesha kwamba mara nyingi tumbo likiwa linauma maendeleo mengine yote yanakuwa sio muhimu sana, tena yanaweza kupelekea kupoteza hayo maendeleo mengine kwa sababu patakuwa hapaliki wala hapalaliki. Sasa sisi matumbo yanatuuma!


Marekani walijenga nchi yao lakini Wamarekani hawakuanza kuendelea wakiwa Marekani. Wamarekani, zaidi ya Wahindi wekundu, ni Wa Europea waliokwenda Americana na maendeleo yao vichwani. Wakayatumia kujenga nchi. Waliowapa Uhuru na waliopewa Uhuru walikuwa wana kiwango kile kile cha elimu, ujuzi, maendeleo vichwani, upeo wa kisiasa, kiitikadi na vinginevyo. Na Wamarekani walipopata Uhuru hawakuanza kuwekana vizuizini willy nilly walipotofautiana mawazo.

Sasa sisi tunaikana Historia ya dunia hii kwa kutaka kujenga Taifa kamili lenye viongozi Malaika wasio na makosa au kila walichokisema na kuahidi kitimilike na kinyume cha hayo, basi ni kosa na tutanyooshea vidole milele.

Tunapojifunza na kujadili historia hatunyooshi vidole. Hata tunaposema, kwa mfano, Waasisi wetu walikuwa wanafiki na wazandiki kwa kupigania Uhuru wa majirani na haki za Waafrika Kusini wakati wao hapa nyumbani walikuwa na wafungwa wengi wa Kisiasa kuliko Afrika Kusini wakati wa kilele cha siasa za kibaguzi za Kaburu, tunaonyesha tu yaliyojiri nchini kwetu. Tunataka historia isipindishwe. Halafu kusema viongozi sio malaika ni kujaribu kuhalalisha kila anachofanya kiongozi. Tunajua hakuna Mwana wa Adamu ambae ni malaika. Hata "Mkwere" sio Malaika. Sasa kwa nini mwamtusi na "mabakuli na kengele" zake? Si na yeye sio Malaika?

Lakini kuna tofauti kubwa sana kati ya Nyerere na kikwete ikiwa kuna watakaosema tumwachie Kikwete naye afanye makosa kama Nyerere, Mwinyi na Mkapa. Mswahili anasema kosa si kulifanya kwa mara ya kwanza, bali ni kulirudia kosa.

Kikwete nae anajaribu sera zake. Hafanyi yale yale ya B. Mkapa na J. Nyerere. Kama J. Nyerere sio Malaika basi J. Kikwete nae sio Malaika. Tusitetee failures kwa kurushia mpira kwa wengine.

Tumefika hapa tulipo ambapo mimi Mndengereko nalonga na Msukuma bila woga huku nimekaa na mke wangu wa Kinyaturu. Hiyo pekee ni maendeleo makubwa.

Hii si kweli kwamba hatukuwepo hapo toka siku za nyuma. Ni myth, ni hadithi. Ni hekaya fulani ambayo imeaminika na kukubalika. Ukinionyesha kwamba katikati ya Karne ya 20 Tanganyika kulikuwa na Ukabila ndio tutasema tumepata maendeleo ya kuufuta na kujenga undugu. Lakini hilo halijaonyeshwa. Harakati za Uhuru zilikuwa ni za mchanganyiko wa watu wote. Waasisi wengi wa Taifa letu walikuwa "walugha lugha" kutoka maziwani na milimani katikati ya nchi, waliokaribishwa Kariakoo na Wazaramo wa pwani. Cha ajabu, tunawasifia waasisi wetu hawa kwa kutoendekeza ukabila. Lakini, humpi mtu sifa kwa kufanya alilotakiwa kufanya. Ukiwahi kazini kila siku hudai bonus au sifa. Kusema waasisi wetu wameleta maendeleo ya kutokuwepo na ukabila ni myth.

Je kuna uwezekano kuwa kufeli kwa Ujamaa kulitokana si kwa sera au fikra za Nyerere tuu, bali ni pamoja na hali halisi ya Uafrika wetu ambayo Nyani anaukiri kuwa "Ndivyo Tulivyo"?

Sasa hapa ndio huwa "napoteza utu wangu" hapa, na najikuta naziita hoja kama hizi kuwa ni za ki hohehahe, za ki baradhuli. Eti mtu una wonder kama "tumefeli kwa sababu ndivyo tulivyo"! Bado utanipa "pole za matatizo yanayokusibu" nikisema hizi hoja ni za kihayawani, za kizugezuge ?

Leo hii tunasimanga detention act za Tanzania, lakini Patriotic Act ya Marekani tunaiamini kuwa itatulinda tunaoishi Marekani kupata balaa la Ugaidi!

Hakuna Mmarekani anawekwa kizuizini bila mashitaka isipokuwa adui mpiganaji anaekutwa kwenye milima na mapango mashariki ya kati huko. Tanzania hiyo draconian law ilitumika kumuweka kizuizini Mwanasheria Mkuu mstaafu aliyetoa maoni mbele ya Tanganyika Law Society kuhusu mabadiliko ya katiba! Imagine that. Hebu fikiria hilo sekunde moja. Wabunge wana jadili fiscal policy bungeni unawatumia political police wawasweke kwenye vyumba vya giza Oysterbay police bila mashitaka kweli? Kujadili bajeti ? Imagine that!

Halafu tunasema eti Waasisi walikuwa wana hoja kali kiasi cha kuogopwa. Una hoja kali ungetuma political police kuweka detention watu wanaojadili ishu katika jamii ? Kuna siku, Mwalimu, utajibu kwa haya uliyoyafanya.

In any society, even a liberal and progressive society like USA, if you are a dissident, you are an enemy. Take a look of the praised Capitalistic America with its attitudes towards minorities, communist or even muslims!

Muslims and minorities are not dissidents. Mchungaji vipi tena ? Wakomunisti wapo America na sio maadui wa kuwekwa kizuizini bila mashitaka. Tusitetee maovu.

Yes I am an ardent Mwalimu fan, and there are things I did not agree with him and that does not make me an out of touch Mdingi mla Chumvi or Haambiliki!

Nini usicho kubaliana nae ?

Kila serikali na wananchi hufanya makosa, kama Zakumi alivyosema, je tumejifunza nini kutokana na makosa yetu? Jee awamu tatu zilizomfuata Mwalimu Nyerere zimefanya nini kusahihisha makosa ya awali?

Mwinyi alifunguliwa soko huria. Mkapa alipigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la sera za Ujamaa. Kikwete anarudi kule kule kwa uomba omba.


Wengi tunayaongelea haya nyuma ya vioo tu. Bado hakuna uhuru Bongo. Much less kujitegemea.


Ndio. Waasisi wetu walitufanya panya wa maabara. Wewe wasema.
 
Kuhani,
Inaonekana hujasikia habari za Seneta Joseph McCarthy na crusade zake za anti-communism hapa Marekani. Watu walipoteza ajira zao kwa kusingiziwa tu kuwa walikuwa ni communist symphathisers katika enzi za kuanzia miaka ya 40 hadi hamsini na kitu katika US. Hata katika miaka ya 60 Edgar Hoover alitumia anti communist phobia kuwanyanyasa watu, akiwemo Martin Luther King Jr, pamoja na maprofesa chungu nzima ambao waliachishwa kazi kwa kusingiziwa tu ni communist sypmhathiser.
 


There you go again bwana Kuhani, rhetorical and grandiloquent presentation!
 

Unavyoupenda Ujamaa nifikiri kuwa hupo Venezuala, Cuba au North Korea kumbe huko hapa hapa Mtoni.

Baniani mbaya kiatu chake dawa.
 
Mchungaji nadhani siyo vema kumdismiss Kuhani..ukisoma mawazo yake utaona yana mantiki kabisa. Hali kadhalika hata watetezi wa mwalimu hapa hoja zao zina mantiki.

Nadhani wengi tunachoshindwa kuelewa ni kwamba Nyerere alikua binadamu kama wewe na mimi. Kuna mengi aliyafanya kama kiongozi na kwa yote aliyafanya kama wajibu wake. Ndicho kitu inabidi tuelewe, kiongozi yeyote akiingia madarakani he is supposed to do good for his/her people. Lakini kwetu Africa ni kinyume na ikitokea kiongozi akfanya hata 5% ya wajibu wake tunampigia makofi na kumpendekeza apewe zawadi ya nobel! Kwa sababu hatujazoea kuona viongozi wakitimiza wajibu wao. Kama Nyerere angefanikiwa katika sera zake, naamini kabisa wengi tungekuwa tunazifia sera za ujamaa na kujitegemea. Lakini kwa sababu zilifail, basi hatuna budi kuzikosoa.

Hivi mchungaji, unafikiri kama Hitler angeshinda ile second world war ingekuwaje? Hakika Hitler angekuwa ni shujaa katika historia ya binadamu na kila mtu angetaka kuji-associate naye! LAKINI KWA SABABU ALISHINDWA, basi ndo maana leo hii anaitwa kila aina ya majina machafu. Wazungu wanasema, victory is a friend of everybody while failure is always an orphan.

Personally naamini, Nyerere alikuwa na nia nzuri na taifa letu, lakini matendo yake mengi kwa kiasi kikubwa YALIDUMAZA demokrasia NA ITATUCHUKUA MIAKA MINGI SANA KU-RECOVER. Ni Nyerere mzee wetu huyu huyu alikuwa anaona sahihi yeye kushindanishwa na kivuli wakati wa uchaguzi! Ni mzee wetu huyu huyu alikuwa havumilii mawazo mbadala! Ni sheria nyingi sana kandamizi Nyerere alipitisha kulinda madaraka yake na ni sheria hizo hizo ambazo mpaka leo zinatupeleka pabaya (ziko nyingi sana kwenye vitabu vyetu). Why? kwa sababu hata siku moja kiongozi hawezi kutengua sheria inayompa nafasi kuwakandamiza wengine. Ingawa Nyerere aliondoka madarakani miongo miwili na ushee iliyopita, lakini bado athari za maamuzi yake tutaendelea kuzipata miaka mingi ijayo! Kwa hiyo usitegemee mtu kama Kikwete leo abadili katiba ambayo itaweka mbele maslahi ya watanzania wote. Kwa sababu na yeye anajua kusudi aweze kusurvive kwenye utawala atahitaji kuwa kama watangulizi wake. Kama unakumbuka Nyerere aliwahi kuadmit kwamba ana madaraka makubwa sana, lakini kwa sababu ana "busara" hawezi kuyatumia vibaya. Lakini je yeye hakujua kwamba iko siku atakuja kiongozi asiye na busara?

Well, kama wengine walivyosema, sasa siyo mda muafaka wa kumlaumu Nyerere au Kambona au yeyote, ni mda wetu kama wananchi tufunge mbeleko tuanze kudai haki zetu maana kamwe, demokrasia Tanzania haitawezekana kwa initiatives za viongozi, isipokuwa sisi wenyewe. Tanzania itajengwa na sisi wenyewe. Leo tunamlaumu KAMBONA KUKIMBILIA UINGEREZA, lakini hatujiulizi ni wangapi wako Nyumbani hapa kupambana na ubaradhuli wa serikali yetu. Its painful, lakini lazima pro-Nyerereist and the like wajue kabisa kwamba Nyerere ana yake mazuri lakini vile vile ana mengi ambayo aliyafanya kwa selfish interests kujilimbikizia madaraka ambayo mpaka leo yanatuathiri.

And make no mistake, bila demokrasia ya kweli TZ hatuwezi kupiga hatua yoyote kamwe. Maana matokeo yake tunayaona..una katiba inayompa raisi virtually uhuru hata wa kutuuza kwenye New York Stock Exchange kama taifa! watu wanaiba mchana kweupe..lakini kwa sababu wako protected na mkuu wa kaya..what do we do? Ni mengi ambayo historia ya nchi yetu imepitia, ndo maana nasema tuachana na Nyerere, waliobaki hai tupambane tupate demokrasia ya kweli.

Kifupi naomba niseme kwamba Nyerere alikuwa ni kiongozi aliyeipenda nchi yake na aliamini katika utu wa mtu, lakini alikuwa ni kiongozi ambaye aliamini kwamba he knew what was good on behalf of his compatriots. Ukiangalia katika historia ya taifa letu mambo mengi sana ya muhimu WANANCHI HATUKUSHIRIKISHWA. IWE MUUNGANO, KATIBA, NK..na ukiangalia mambo yote yaliyofanywa kwa busara ya Nyerere kwa NIABA yetu leo ndo yanatuletea matatizo makubwa kama taifa! Taifa gani hilo uhusiano wa watawala na watawaliwa unakuja kipindi cha kupiga kura tuu?..

Hatuna haja ya kulaumu yeyote, yaliyopita si ndwele, tukae chini tutafakari tulijikwaa wapi, tuijenge nchi yetu!
 
Zakumi,Kuhani,

..nashukuru kwamba hata wewe umeona jinsi 'washabiki' wa Mwalimu walivyoikimbia ripoti ya wachumi toka Goteborg Univ na ESRF.

..ripoti hiyo inatoa mwangaza wa jinsi mijadala ya uendeshaji uchumi wa taifa letu ilivyokuwa ikiendeshwa wakati ule.

..zaidi ripoti inaelezea matatizo yaliyokuwepo, mapendekezo tofauti ya hatua za kuchukua, pamoja na maamuzi yaliyofikiwa kutokana na mapendekezo hayo.

..kuna wananchi walipoteza kazi/nyadhifa zao. kosa lao lilikuwa ni kumsihi Mwalimu kubadili mwenendo wa jinsi uchumi wetu ulivyokuwa ukiendeshwa.

..kuna walioitwa wasaliti, wakapakaziwa kwa wananchi, wakatengwa kisiasa, na kudhalilishwa ndani ya chama.

..Mwalimu alitekeleza ushauri mbaya, matokeo yake uchumi ukadidimia. lakini hakuna aliyewajibishwa badala yake watu hao hao wakapewa nafasi ya kutekeleza mapendekezo ambayo mwanzoni waliyopinga kwa nguvu zote.

..mazingira na mahusiano ya utendaji kazi na kisiasa wakati wa utawala wa Mwalimu hayaku-encorage mawazo mbadala, badala yake kulikuwa na mashindano ya kudumisha fikra za mwenyekiti--hata zile zilizokuwa na athari mbaya kwa uchumi.
 
Ujamaa wa Nyerere ni mchanganyiko wa mambo huwezi kuupeleka China au Urusi kwa vile mambo kule yalikuwa ni ya kutumia nguvu dini zilikuwa haziruhusiwi, yeye alikuwa anatumia ushawishi. Naweza kusema kwamba alipata influence ya Mahtama Gandhi kwenye kupigania uhuru.
Na mimi niwaulize swali Vurugu za kiuchumi zinazotokea Marekani zinaelekea kuonyesha mfumo wa Ubepari nao umedunda? Ninavyofahamu mfumo huo huwa hauingiliwi na serikali unatumia nguvu za soko mbona serikali inatupia taulo kuokoa makampuni naomba mnifahamishe wanelekea wapi jamaa?
 

Jasusi,

Nani aliwekwa kizuizini bila mashitaka wakati wa McCarthyism ?

Unavyoupenda Ujamaa nifikiri kuwa hupo Venezuala, Cuba au North Korea kumbe huko hapa hapa Mtoni.

Baniani mbaya kiatu chake dawa.

Zakumi,

Hilo kombora ni kali mno, sidhani kuna wengi wanaweza kuli handle hapa. Unafanya mchezo. Nimemuuliza Bubu Ataka Kusema juzi hapa, kama unabeza ubepari na unasema "mazuri ya ujamaa ni mengi mno kuliko mazuri ya ubepari" sasa kilichokufanya ukimbilie kwa mabepari ni nini? Oooh sijakimbia, sasa kumbe umefanya nini, unatafuta matibabu ya dharura Saint Thomas Hospital ? Wakaja ma defense attorney wake, wakina Pundit, ambao nao hilo kombora lime "hit home" kwa sababu inawezekana ndio wale wale waliokimbilia kwa mapepari halafu wanatukana ubepari. Wakashindwa kumtetea! Huwezi kuimba Ujamaa ujamaa, halafu umekimbilia kwa mabepari.
 
Tatizo kubwa la Waafrika/Watanzania ni kuwa akitokea Mwafrika/Mtanzania anayejaribu kuvumbua kitu kinachotokana na mazingira ya Kiafrika/Kitanzania na kitakachofanya kazi Afrika/Tanzania basi anapigwa vita mpaka kaburini. Ila akitokea mzawa akaenda ASEAN kuomba sera ya MINITIGER2020 anaonekana wa maana. Tena mzawa mwingine akienda US kuomba dozi ya PRSP ili atengeneze MKUKUTA/NSGRP wa kuombea misaada kupitia kopo la maombi la HIPC anaonekana wa maana!

Mpaka leo tunajadili tuige kipi, cha magharibi au mashariki, badala ya kunoa bongo zetu na kuvumbua vya kwetu wenyewe. Hivi hizi nadharia za ubepari na usoshalisti/ukomunisti zinamsaidia nini mkulima wa pale kijijini Mtakuja? Ujamaa ilikuwa ni jitihada ya dhati ya kuvumbua mfumo wetu wenyewe wa maendeleo! Ndio maana hata Mwalimu alisisitiza kuwa anachukia 'dotrinaire socialism', yaani imani ya kisoshalisti, inayosema maisha yetu ni maisha ya migogoro ya watu/matabaka na unaoutukuza ubepari kwa kudai kuwa lazima tuwe kwanza mabepari alafu tupambane wee uchumi uanguke pwa kama unavyoanguka sasa duniani ndipo tuwe wasoshalisti. Ujamaa ulikuwa ni msingi wa usoshalisti wa Kiafrika wenye mantiki ya Kiafrika kwa ajili ya Mwafrika anayeishi Afrika kwenye mazingira ya Kiafrika (Rejea http://www.nathanielturner.com/ujamaanyerere.htm)!

Fellow Africans/Tanzanians let us stop consuming the knowledge that we don't produce while we produce the knowledge that we don't consume, yaani, Waafrika/Watanzania wenzangu hebu tuache kufakamia maarifa ambayo hatujayavumbua na kuvumbua maarifa ambayo hatuyatumii!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…