Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,540
- Thread starter
- #341
Sasa tujiulize ilikuwaje ghafla katika miaka ya 70 JKN aliingiwa nini akilini mpaka akakubali viongozi waanze kutumia nguvu za dola kulazimisha wananchi waende kuishi misituni?Nini kilisababisha fikra za JKN zibadilike na aanze kutekeleza yale ambayo hakuyadhamiria hapo awali? Hivi hayo mawazo yake ya mwanzo nayoyanukuu hapo chini kutoka kwenye hicho kijitabu chake cha sera yana tatizo gani - mbona mengine wanayaiga kwenye hizi refomuzi tulizoletewa na hao hao ambao sasa wanabeiliauti na kutaifisha makampuni yao?.,!
Companero,
Nina deni kwako kukujibu kuhusu kauli ya uvivu wa Mtanzania(Mwafrika), nilikuwa nimekujibu, bila kufahamu mitambo ilipoteza mawasiliano kwa muda, hivyo majibu yangu yakapotea. Lakini nitakujibu swali na masikitikmo yako baaday.
Kwenye hili uliloliuliza hapa juu, nafikiri baada ya vurugu zote za 60's mpaka kifo cha Karume an Obote Kupinduliwa, Nyerere si ajabu aliingiwa na na Paranoia!
Ilipokuwa kitu kuhusu Usalama wa Taifa au Usalama wa uongozi wake, nafikiri woga ulimtawala kimawazo na hivyo kama Kawawa au DC fulani waliwasilisha habari ambazo zilionekana credible on surface, Nyerere inawezekana aliidhinisha hatua za kidola kufanya kazi.
Sasa wale wanaompinga Nyerere watasema mbona yeye hakusimama kidete bila woga? Waswahili wanasema, "kwa mwgoa hakujaenda kilio" au wengine husema "kinga ni bora kuliko tiba"
Sasa kama aliamua kutumia madaraka yake iwe kwa kuweka watu kizuizini au kamata kamata ili kuwepo hali ya utulivu na kuzuia mawazo ya kuleta chokochoko ambazo zingehatarisha ustawi na usalama wa Taifa letu changa ambalo lilikuwa ndio linaanza kujijenga kiuchumi, kisiasa na hata kiitikadi huku likijihami na Ubeberu na ubabe wa Makaburu, Ian Smith na Wareno wa Msumbiji, je tutasema haikuwa haki yake kutumia madaraka yake kwa manufaa aliyoyaona kuwa ni ya Taifa?
Leo hii tunapata nafasi nzuri kumchambua na kutofautisha ni yapi aliyoyafanya yalikuwa mazuri na ni yapi yalikuwa si sahihi na mabaya. Lakini tusimnyime haki yake kuwa alifanya mengi kwa nia ya kulijenga Taifa imara.
Kama Nyerere angekuuwa hana utu, basi wengi wangeuawa, angekuwa ni tajiri wa kupindukia na si ajabu angekua anaishi ukimbizini!
Nyerere aliwaamini sana wasaidizi wake. Wengi walifanya mambo na kumletea kila aina ya habari na aliwasikiliza na kuwapa uhuru ambao leo hii, tunaupinga!
Leo DC anakuwa huru tunadai ana nguvu nyingi. Lakini katika pumzi hiyo hiyo, tunataka demokrasia na DC wawe na uwezo wa kujiamulia.
Zoezi la Vijiji vya Ujamaa, Uhujumu Uchumi, Operesheni Maduka na mengine mengi ambayo yalikwenda kombo, mabaya yaliyotokea hakuyafanya Nyerere. Kosa lake ilikuwa kushindwa kusitisha uonevu ulipotokea.
Hilo nitakuwa wa kwanza kusimama mbele kulitamka na bado mapenzi na heshima yangu kwa Nyerere hayatabadilika!
Historia inatufundisha mengi, labda sasa ni wakati tuwafuate kina Mwinyi, Malecela, Msuya, Kingunge, Kawawa na wazee wengine waliokuwa madarakani kati ya mwaka 1967-1985, tuwaulize, nini kilitokea hasa baada ya mauaji ya Karume na Tanzania ikaanza kudidimia na ubabe wa Serikali na TANU/CCM kushika hatamu?
Tuwaulize hawa ndugu, je Nyerere alikuwa mtu wa namna gani miaka hiyo baada ya Azimio la Arusha na Uasi wa kina Kambona?