Who influenced Nyerere: His Ujamaa Philosophy and Azimio Principles?


Hivi Nyerere aliwahi kuwataka watu kuimba zidumu fikra zake? Hilo tamko au agizo alilitoa wapi na lini na kwa njia gani i.e. hotuba, memo, sheria ya bunge...?
 
Hivi Nyerere aliwahi kuwataka watu kuimba zidumu fikra zake? Hilo tamko au agizo alilitoa wapi na lini na kwa njia gani i.e. hotuba, memo, sheria ya bunge...?
kama alikuwa hataki si angekataza watu kusema hivyo. tatizo nadhani jamaa alikuwa anapenda watu wanaomwambia "yes sir". Huitaji kuwa Rocket scientists kuelewa hilo.
 
mimi mpaka sasa bado sijaona makosa aliyoyafanya na hasa ukizingatia wakati huo nchi ilikuwa ni changa sana ila kinachonishangaza ni watu kuendelea kulaumu tu.lakini swali linakuja je wakati wa utawala wa mwalimu na utawala uliopo sasa ni upi wenye muelekeo? maana ninapotizama tanzania inakoelekea naona ni gizani?sasa nyie wana jf mnaojifanya mabingwa wa kuchambua na kukandia yale yote aliyofanya nyerere nawaona ni wenda wazimu.maana mngejiuliza kitu kimoja tu JE NI NINI SERA YA MAENDELEO YA NCHI KWA SASA? je baada ya miaka kumi tanzania itakuwaje.nafikiri baada ya miaka kumi tanzania itakuwa ni giza totoro
 

Sajo,

Kwa niliyoyasikia na kuyafahamu, kuna watu watatu tuu ambao walikuwa washauri wa na wasaidizi wa Nyerere (watendaji) ambao walikuwa wakiweza kusimama kidete na kubangua mada na Kifimbo. Edward Sokoine, Cleopa Msuya na John Malecela.

Wengine sijui kama walikuwa na ubavu kama Jasusi alivyoeleza kutoa hoja za msingi kwa Mwalimu.

Ukiangalia kwa kina wale waliokimbilia kuua Azimio la Arusha na kulikumbatia Azimio la Zanzibar na kuchangua ni wapi na kina nani walifanya kazi chini ya Mwalimu, utagundua kuwa katika CCM kwa ukubwa walikuwa ni wanafiki na ni wachache sana walikuwa wakweli na kuweza kum-face Mwalimu kwa jambo lolote.

Haya ni maoni yangu kwa mtazamo wangu na natumaini ukiongeza watu kama Kaduma, Msekwa, Sefu Hamad, Salim, Warioba na hata Kolimba, hawa wanaweza kuwa walikuwa na uwezo wa kuongea na Mwalimu bila shida.
 
kama alikuwa hataki si angekataza watu kusema hivyo. tatizo nadhani jamaa alikuwa anapenda watu wanaomwambia "yes sir". Huitaji kuwa Rocket scientists kuelewa hilo.

Ok, kuna ushahidi wa kwamba aliwataka watu? Na kuna ushahidi kwamba hakuwakataza watu? Na kama watu walijiamulia kuimba hizo nyimbo au ngonjera kwa nini alaumiwe Nyerere? Hivi ni yeye pia aliyewataka watu kumwita baba wa taifa?
 

Kuna mengi mno tunayoyasikia kuhusu Nyerere and therein lies the "myth"......
 
Suala la mapungufu ya Nyerere sikutaka kulifanya liwe ndio msingi mkuu wa mjadala huu.

Mjadala huu ulikuwa ni kujua ni wapi Nyerere alipata mawazo na mwamko wa kutuletea Ujamaa na hata Azimio la Arusha.

Najua kuna thread nyingine ambayo ilishawahi kuanzishwa kuhusu mapungufu, basi tuende kule kulalamikia mapungufu yake.
 

hata MAO alikuwa haambiliki alipokuwa hai lakini baada ya kufa, leo wachina wote wamegeuka na kumfanya Mungu maana wanamuabudu kama sisi tunavyomuabudu Yesu tusiyemjua,Swali je ni yupi mzuri kati ya nyerere asiyeambilika na H .MWINYI au B. MKAPA AU JK wanaoambilika? 'shame on you'
 

You should know by now that any thread about Nyerere will take this kind of a detour....

For some reason it's hard for people to stay focused in this forum....
 
Kuna kitu kimoja ambacho Watanzania tunakifanya kwa ama ushabiki wa chuki kutokana na yaliyotusibu kwa namna moja au kwa kuishi kwenye mawazo na nchi ya kusadikika.

Nyerere tunamsema kuwa alituletea umasikini, alikuwa haambiliki, alikuwa akitesa watu na maneno mengine mengi kana kwamba Nyerere alikuwa ni Malaika mtakatifu ambaye asiye na mapungufu ya kiubinadmu kama wanadamu wengine.

Naomba kama kuna mmoja wetu mwenye ushahidi na kutupa mfano wa japo viongozi watano duniani hii ambao wamekuwa wakuu wa nchi ambao hawakuwahi kufanya maamuzi ambayo hayakuwafurahisha kila mtu, na atuletee hayo majina na mifano!
 
hata MAO alikuwa haambiliki alipokuwa hai lakini baada ya kufa, leo wachina wote wamegeuka na kumfanya Mungu maana wanamuabudu kama sisi tunavyomuabudu Yesu tusiyemjua,Swali je ni yupi mzuri kati ya nyerere asiyeambilika na H .MWINYI au B. MKAPA AU JK wanaoambilika? 'shame on you'
 

Mapungufu ya Nyerere sio mahala pake hapa; na mapambo ya Nyerere yasiyohusiana na Azimio la Arusha na vyanzo vya fikra zake? Hayo ni sawa, sio?

Tena mapambo ya kupotosha, ya uongo, hayo hayakataliwi? Nimeona wasifu wa uongo umejipenyeza nikapinga mapambio hayo, na nikijua ni mada nyingine, nikaeleza kwa nini nimeandika niliyoandika.

Sasa tukikataa yasiyohusika hapa tukatae yote, mapambio ya uongo na mapungufu ya Nyerere. Yote sio mahala paka.

Haya nawaacha na majadiliano yenu, al muradi yasisemwe ya uongo yasiyohusika, maana hatutaruhusu vizazi vya kesho kutwa vidhanie woooote tulikuwa bado tumepumbazika (hoodwinked ) na bunk za Nyerere, mpaka mwaka 2008.

(Kwanza nilichokiongelea hata hivyo kiko on point, kwamba Nyerere hakutaka kutofautiana na mtu. Kimewashtua kwamba nimeongelea jinsi alivyosweka watu ndani waliojaribu kutofautiana nae ? Come on guys!)
 
Hebu jaribu kufikiria kama yeye mwenyewe leo angekuwa hai na pia member humu ndani labda tungepata majibu mengi sana,lakini hayupo.
Kila mtu anakuja na tafsiri yake kuhusu mambo aliyoyafanya Mwalimu wakati wake.Lakini wengi tunakubaliana kuwa he had his countries interests in his heart,kwa sababu kama sio hivyo basi kuna mengi mengine zaidi ambayo angefanya,na sijui hapa tungekuwa tunasema nini sasa hivi.
Why Nyerere all the time? Kila siku mambo yanakwenda yanajirudia yaleyale,Nyerere kafunga watu,Nyerere fisadi,Nyerere haambiliki,Nyerere mkatili.....kweli jamani huu sio wakati wa kuweka vichwa vyetu na kuangalia matatizo ambayo tunayo sasa hivi.Fine Ujamaa failed,yeye mwenyewe ali admit,sasa ambacho tunacho sasa hivi in its stead ni bora?Watoto wanauza mali walizoachiwa na baba yao,then wanamlalamikia kuwa ni kosa lake. The country seems to have gone backwards,lakini bado tupo hapo kumlaumu mtu aliyetoka Madarakani miaka 23 iliyopita....only in Tanzania.Maana kuna watu humu wanasema hata JK katuletea Nyerere,wakati nyie wenyewe ndio mlienda kumpa 80% of the votes,na yeye mwenyewe aliwa warn kama mnapenda sura yake mkanywe nae chai.
Let the man rest in peace guys,na tujaze pages hapa with what we have infront of us for the good of our kids and theirs
 
Someni yote aliyoyaandika Mwalimu; sikilizeni hotuba zake zinazoendelea kurushwa na redio yetu ya Taifa; mtagundua kwamba akili na mawazo ya Mwalimu vilikuwa vya kwake mwenyewe na aliweza kuyasimamia vizuri yale yote aliyoyaona ni sahihi na ya MSINGI kwa TAIFA letu.Angalieni mifano hapa kwa majirani zetu tu. Mtu anakuwa maarufu kwa sababu ya KABILA yake, DINI yake, UTAJIRI wake,... Rais anahutubia watu wake kupitia wakalimani...
 

Kuhani,

Kosa lako ni kujiona kuwa ni wewe pekee ambaye unajua watu walioathirika na utawala wa Mwalimu Nyerere. Na hii si mara ya kwanza kulifanya hili!

Je unajua ni mangapi ambayo familia yangu iliyapata au kuyapoteza kutokana na huyo huyo Nyerere? If you would have known ungekaa kimya, ila ni jambo la binafsi na sitalileta hapa!

Kuna wengi ambao walipoteza mali, marafiki hata watu kuwekwa ndani kama ulivyotuletea listi, lakini katika mada hii, hakuna hata mmoja wao aliyesema kuwa aaah Nyerere ni hive au vile isipokuwa wewe.

Imekuwa ni kawaida yako kuyasema haya, na hilo naliheshimu, lakini kama nilivyosema, mjadala haukuwa unachunguza ni nini Mwalimu alikifany aau kukosea, ni kujiulilza, chimbuko la Mwalimu Nyerere kuwa mjamaa na kutuletea siasa za Ujamaa, Kujitegemea na Azimio la Arusha.

Kwa nini usianzishe basi thread nyingine ya facts na data zako kuhusu waliofungwa, kupoteza mali au kunyanyaswa na Nyerere na tuje huko kufocus machungu yetu kuhusu Nyerere?
 

Mchungaji!... hii inaitwa kumtolea mtu uvivu; kuna watu wanadhania kuwa ni wao peke yao wanaijua historia ya nchi yetu na wimbo wao kila wakati umekuwa ule ule kana kwamba sisi wengine tumezaliwa na kukulia Ulaya! Hapo umemkoma nyani giledi.
 
Nimewafungulieni wale wenye ugwadugwadu na Nyerere thread yenu maalum, nendeni kule mkayatoe yale ya moyoni tujadili mapungufu, ubaya na ukatili wake!
 
Mchungaji!... hii inaitwa kumtolea mtu uvivu; kuna watu wanadhania kuwa ni wao peke yao wanaijua historia ya nchi yetu na wimbo wao kila wakati umekuwa ule ule kana kwamba sisi wengine tumezaliwa na kukulia Ulaya! Hapo umemkoma nyani giledi.

Mwanakijiji,

Alichonacho Kuhani dhidi ya Nyerere ni chuki na si kukosoa mapungufu ya uongozi dhidi ya Nyerere.

Hili kaliweka wazi baada ya kuja kudai Nyerere anatia aibu kwa kwenda kufia nje uya nchi badala ya Lugalo.

Hiyo hoja nilipoisoma, nikajiuliza maswali mengi sana pamoja na Kuhani kuoneka kuwa ni mahiri, ni vipi akose utu na kuanza kudhihaki? nikagundua kuwa ni chuki na si kitu kingine na hivyo kamwe hapatakuwa na jema kuhusu Nyerere machoni pake.

Ni haki yake kutokumpenda Nyerere, lakini anapokuja na kuharibu mada alimradi hampendi Nyerere, hapo anakosea.

Nimemsaidia yeye na wenzake wasioona hata chembe ya jema alilofanya Mwalimu Nyerere kwa kuwafungulia thread waende huko wakajadili ubaya wa Nyerere!
 
Kuhani,
Fortunately you do not have monopoly on the truth, do you? Hii dhana ya kuita maoni ya wengine uwongo ni dhana muflisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…