Who Is Mange Kimambi? Jua ukweli wenye facts sio grapevine kumhusu huyu mtu, biography and facts!

Who Is Mange Kimambi? Jua ukweli wenye facts sio grapevine kumhusu huyu mtu, biography and facts!

Status
Not open for further replies.
C&P - Joshua Lawrence.

Je kuna watanzania hawamjui au hawajawahi kulisikia jina la MANGE KIMAMBI? Kama wapo basi ni wachache sana. Je, ni nani huyu Mtanzania mpare aishie US?

MANGE KIMAMBI alizaliwa Hindu Mandal hospital, Dsm mwaka 1984. Baba yake, mpare, alitengana na mama yake MANGE, mmakonde, MANGE akiwa na umri wa miaka 2 tu. Mange akalelewa na mama wa kambo. Inadaiwa kuwa mateso makali aliyoyapata toka kwa mama huyo wa kambo hayakuwa ya nchi hii! MANGE , kutokana na kuteswa huko, akajenga chuki mno kwa kila mtu na aliwahi kufukuzwa shule ya vidudu akiwa na umri wa miaka 6 tu kutokana na kuvionea na kuvipiga sana vitoto vya kihindi kwani alikuwa mtukutu sana.

Elimu ya msingi aliipata Bunge primary school ambako alisoma kwa mwaka mmoja tu. Kuna wakati hakwenda shule kwa wiki mbili na badala yake akawa akienda kitaa kucheza. Baba yake alipoarifiwa akaenda shuleni na kumtandika mboko mbele ya wanafunzi wote pale Assembly. Baadaye MANGE akahamia boarding kutokana na ukatili wa mama wa kambo ambapo alisoma Arusha school. Huko licha ya kuwa na akili sana darasani pia alikuwa mwanamichezo hodari ambapo alikuwa nyota na Kapteni wa michezo yote shuleni hapo yaani swimming, netball na mbio. Siku ya graduation, MANGE alizawadiwa zawadi ya *Sports Personality of the Year*. MANGE alifaulu mtihani wa darasa la 7 kwani akili yake ilikuwa ikichaji sana na kuchaguliwa kujiunga na Arusha sec school.

Mzee KIMAMBI alifurahi na kumpeleka kusoma Zimbabwe ambako alisoma miaka kadhaa. Baadae MANGE akaenda US kusoma lakini akapata mimba na kulazimika kurudi Bongo na kujifungua mtoto aitwae BHOKE.

Mwaka 2004 MANGE alijiunga na AVU-UDSM ambako alipata degree ya Business Administration na baadae akaenda Dubai alikoibuka na Masters(MBA).

Mzee KIMAMBI akawa na mahusiano na Dr. MWELE NTULI MALECELA kama mkewe. MANGE aliishaweka wazi kuwa anamuheshimu na kumtii DR. MWELE kuliko mtu yeyote duniani. Mzee KIMAMBI ambae alikuwa tajiri akimiliki mali kadhaa ikiwemo Tiger Motel na jumba la kifahali Mbezi beach alijiua ghafla kwa sababu anazozijua mwenyewe.

MANGE, muongo mmoja uliyopita, alianzisha blog iitwayo U-TURN ambayo ilijipatia umaarufu mkubwa.

Sababu kubwa ya kuanzisha blog hiyo ni kutafuta sehemu ya kujitetea. Mara nyingi magazeti ya Udaku hasa ya ERIC SHIGONGO yalikuwa yakitunga habari dhidi yake naye hakuwa na mahali pa kujitetea ndipo alipopata wazo hilo la kuanzisha blog hiyo.

MANGE, tofauti na bloggers wengine karibu wote, yeye ni muumini mkubwa wa FREEDOM OF SPEECH yaani UHURU WA KUJIELEZA na ndiyo maana hata yeye akitukanwa huwa anaachia tu comments kwani she is a free spirit. Blog yake ilikuwa na matusi ya kila aina na inaongelea mambo mbalimbali. Hata hivyo aliifunga lakini sasa yuko kwenye Instagram.

MANGE aliolewa na mzungu aitwae LENCE waliyekutana Dubai na kuzaa watoto 2 wa kiume KEANO na KENZO lakini sasa wameachana.

MANGE toka utotoni alikuwa mwanaCCM kindakindaki. Kwa maneno yake mwenyewe aliyoyasema tarehe 27 Februari 2011:
*"Mimi ni mtoto wa CCM. CCM ni kila kitu kwangu. Bila CCM labda nisingekuwa hapa. Baba yangu alikuwa supporter mkubwa wa CCM. Nimelelewa nikiona wazazi wangu wakiipenda CCM. Rais Kikwete anafanya vizuri. Kuna matatizo kidogo kwenye utendaji na CHADEMA wanayatumia kuwadanganya wananchi kuwa CHADEMA ndiyo suluhisho. Watanzania nawaambia siku mnakayowakabidhi nchi CHADEMA tutakuwa tunalala tukiskia mitutu ya bunduki next door.."*

Mwaka 2015, MANGE alitoka US na kuja kuchukua fomu ya kugombea ubunge wa Kinondoni kwa tiketi ya CCM. Hata hivyo hakugombea jimbo hilo.

Mange alitumia kipawa chake kikubwa cha kuandika na kujenga hoja alichopewa na Mungu kwa kumpigia kampeni za kufa mtu Mh. DR. JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI na aliweza kuwashawishi wengi na hasa vijana kumpigia kura. Hakuna tusi ambalo mgombea wa CHADENA Mh. EDWARD NGOYAI LOWASA@ LAIGWANAN hakutukanwa na MANGE.

MANGE mwenyewe amedai kuwa baada ya uchaguzi Mh. ABRAHMAN KINANA na MH. NAPE MOSES MNAUYE walimshukuru kwa kazi kubwa aliyoifanyia CCM kutokana na kampeni hizo.

Baada ya Mh. MAGUFULI kuingia madarakani, MANGE akaendelea kumfagilia sana kutokana na namna yake ya uongozi. Jambo la ajabu, baadae kwa sababu ambazo haziko wazi, na in vema tukazifanyia utafiti wa kina, MANGE akageuka na kuwa mpinzanii dhidi ya Rais Dr. MAGUFULI na serikali ya awamu ya tano.

Mwaka 2016, MANGE alijitwisha hoja zote za upinzani na kuwafanya wapinzani waonekane hawana lolote wafanyalo kwani walikuwa wakimsikiliza na kufuata kila asemacho MANGE. Hili lilimkera Mh. LOWASSA ambaye akalazimika kutoa msimamo wa chama kwamba-: *CHADEMA kama chama cha upinzani lazma iwe na sera nzuri na mipango mizuri na madhubuti ya kuin'goa CCM. CHADEMA haiwezi kwenda Ikulu kwa kumtegemea msichana aliyeko Marekani*.

MANGE kwa sasa amekuwa maarufu mno. Tafakari juu ya Harambee ya kumchangia matibabu ya Tundu Lisu, alivyofanikiwa kuchangisha takribani shilingi za kitanzania milioni hamsini. Hakuna blogger anayemkuta kwa followers. Kwa vile Magazeti sasa yanaogopa kuandika mambo dhidi ya serikali hasa baada ya ITV kupigwa faini ya TZS 15M kwa kumwonesha Mkurugenzi wa HLRC akielezea matukio ya kinachodaiwa ni uminywaji demokrasia katika chaguzi za Udiwani kata 43 nchini, watu sasa wameona sehemu pekee ya kupata habari ni kwa MANGE. Kwa maana nyingine, kukosekana kwa Uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania kunamjenga MANGE na kuwa turufu na rufaa ya mwisho wa yale yaliyofichwa uvunguni mwa Tanzania. Hali ikiendelea hivi MANGE ataitwa nabii wa Watanzania.

Kuna kila dalili kwamba, baadhi wafanyakazi serikalini humtumia MANGE nyaraka nyingi na nyingine zenye muhuri wa *SIRI*. Mf kuna barua toka Ikulu kwenda kwa Mh. Prof. JOYCE LAZARO NDALICHAKO kuhusu suala la watoto wa kike kutoruhusiwa kuendelea na masomo. Barua hiyo licha ya kugongwa muhuri wa SIRI lakini MANGE alipewa na kuianika!

MANGE amevuta watu wa rika zote, wafanyakazi wa serikali, sekta binafsi na hata wanafunzi ambao wakiamka tu asubuhi kitu cha kwanza ni kumsoma kaandika nini. Hata mawaziri nao hawakauki page ya MANGE mf kuna wakati MANGE aliripoti kuna nesi anazingua hospitali ya MUHIMBILI na Mh. HAMIS ANDREA KIGWANGALA mara moja akiwa Naibu wa Wizara ya Afya akafika hospitalini hapo na kutatua tatizo hilo kisha akaripoti kwa MANGE. Mh. POLEPOLE nae mara kadhaa anajadiliana *inshu* na MANGE. Na si tu hao bali wengi tu wakiwemo wabunge mf Mh. HUSSEIN MOHAMED BASHE.

Aidha, watanzania wengi ni kama wamevurugwa kwani badala ya kupeleka matatizo yao kwa viongozi wao mf wabunge nk, wao huyapeleka kwa MANGE. Cha ajabu MANGE naye amekuwa akifanikisha utatuzi wa matatizo hayo ingawa yupo US, mf kuna wakati mwananchi mmoja alimtumia MANGE picha ya mlango wa hospitali ya TEMEKE ukiwa umeharibika vibaya sana. MANGE aliwataka hospitali hiyo kuona aibu na iutengeneze mlango huo haraka. Baada ya siku 2 tu mlango mpya ukanunuliwa na kuwekwa!!

Umaarufu wa MANGE kwa sasa umekuwa maradufu. Watu, wa ndani na nje ya nchi, lazima wamsome hata mara tatu kutwa kama dozi ya panadol!

MANGE, kwa nyakati zingine, ameutumia umaarufu huo vibaya kwa kuwatukani viongozi matusi ya nguoni. Huo sio ustaarabu wa kitanzania Nikiwa mmoja wa watu wanaopigania UHURU wa MAWAZO na kujieleza ningependa kuchukua fursa hii kumwomba biinti huyu abadilike!!!

MANGE sasa ameutumia huo umaarufu kuandaa maandamano siku ya muungano tarehe 26 April 2018. Hiki ni kitu kibaya sana na kitatia doa kubwa kwa taifa letu.

Hata hivyo, nashauri kuwa juhudi kubwa zifanyike ili nchi yetu inayosifika kama kisima cha amani isitumbukie katika machafuko, maaana tatizo sio ushawishi wa MANGE, Bali tatizo kubwa OMBWE linalojazwa na MANGE.

Kutokana na ushawishi mkubwa alionao MANGE watanzania Diaspora walioko US na Ulaya sasa wameanza kuomba vibali vya maandamano na nchi hizo hutoa kirahisi vibali hivyo. Jana Ujerumani imewapa watanzania waishio huko kibali cha kuandamana siku hiyo!.

Kwa vile kuna uwezekano mkubwa maandamamo hayo yakabeba taaswira ya kimataifa, ni vema hekima na busara vingetumika badala ya ubabe na hasira. Iwapo hekima na busara havitatumika, athari za maandamano hayo ni:

1. Taifa letu litatiwa doa kubwa;
2. Potential investors wataogopa kuja
3. Potential tourists wataogopa kuja
4. Uchumi utaathirika kwani Nchi zenye vurugu ni nadra sana kuendelea.

Kama ningelipewa fursa ya kuongea nawe Mheshimiwa Rais wangu, ningekunong'oneza kuwa URUHUSU watanzania waandamane tu, na Jeshi la Polis lihakikishe usalama unakuwepo. Kwa kufanya hivyo ungejenga MSHIKAMANO wa Kitaifa. Mungu ibariki Tanzania. Mungu Ibariki Afrika.
Aruhusu ili upate cha Kuandika kuwa hata JPM anamuogopa Mange! Big no
 
kwenye mitandao mange anaonekana shujaa, but kwenye uhalisia sio hivyo, ni kama ilivyo upinzani wafuasi wake ni wachache ila wako busy mitandaoni lakini ccm ina wafuasi wengi na wengi wao hawako mitandaoni.
Ni chizi tu atakayekuamini, ccm inawafuasi wengi wkt inaogopa katiba mpya, inaogopa uchaguzi huru wako bize kuhakikisha uchaguzi unasimamiwa na makada wao. Siku iyyo tukipata uhuru wa kweli utaiona ccm kuwa nyepesi km ubua
\q\~\
 
Mkuu huyu Mange ndo huyu wa instagram kweli? Maana mimi nnayemjua ni Mtoto wa Marehemu mzee Kimambi yule aliyeishi Kahe; Moshi Vijijini ambaye alitujengea msikiti kule...BTW duniani ni wawiliwawili huenda huyu na huyo wa Mbezi Beach wanafanana sana au mapacha maana huyu wa Kahe wakati anaolewa alikuja pia na mzungu anayefanana na yule aliyepostiwa na Mange wa instagram. Nadhani hata mabwana zao walifanana pia.
Kwani huwezi kuishi Moshi baadae ukahamia Mbezi.
 
ndugu Nakushukuru kwa kutupa data za Huyu Dada yetu , Mimi sio mshabiki wake na nadhani nimeingia mtandaoni kumsoma kama mara tatu tuu, na mara zote hizo nilikerwa sana na lugha anayoitumia. sikujua kumbe ana ukaribu na Kijana Malecela amabya alikuwa akimtukana matusi ya kushtua sana.

kwa namna alivyokuwa na wafuasi wengi, nadhani angekuwa na busara angeweza kuitumia fursa hiyo kuisaidia nchi yake na yeye mwenyewe vizuri sana, lakini kwa hii tabia yake ya MATUSI ama UCHOCHEZI, inaonyesha kuwa sisi tumekuwa taifa la wajinga wengi, kwani wafuasi wengi wanafuata kuyasoma matusi ama ni wapenzi wa lugha chafu isiyokuwa mila zetu.

Wafuasi wake wangejiuliza , JEE ni kwanini Mange haelewani na watu wake wa karibu, Kwa nini anapoteza marafiki au washirika wake kirahisi, na MUHIMU KABISA KWA NINI KANAACHWA NA MUMEWE NA MAHAKAMA YA UMAREKANI IMEMNYANGANYA WATOTO NA WAKO KWA BABA YAO, NAYEYE AMEPEWA FURSA YA KUWAONA WANWE MARA MOJA KWA WIKI?????????? Ndugu waguasi wa Mange, America mama hanyanganywi watoto kirahisi hata kidogo, hilo huweza kutokea iwapo Mzazi mwenzake atakapoweza kuionyesha Mahakama ushahidi uliohakikiwa na SOCIAL SERVICES ya kuwa Mama hana MAADILI MAZURI YA Kuweza kuwalea watoto, na hao watoto wakiachwa kwa mama yao watopotea.

sasa kama mange ni hodari wa kuanika makosa ama aibu za watu asiowapenda amd kama ni mkweli basi henbu aweke hizo documents za mahakama zilizo mnyanganya watoto, wafuasi wake wajue ukweli.

Ni kitu cha kushangaza and it only happens in Tanzania AN UNFIT MOTHER CAN LEAD OR HAVE SUCH A BIG NUMBER OF FOLLOWERS. THERE IS NO DOUBT AT ALL THAT SHE IS INTELLIGENT AND VERY INTELLIGENT, BUT SHE IS NOT SMART OR ETHICALLY RIGHT AT ALL.

I AM EXPECTING ALL TYPES OF INSULTS FROM HER LAMBS AND HERSELF, BUT FORTUNATELY I NEVER LOOK BACK NOR DO INSULTS FROM THOSE BELOW ME DO BOTHER ME.
Mbona wewe unakubali kuongozwa na mtu aliyezaa na shemeji take pamoja na wasaidizi wake?
 
Kwani huwezi kuishi Moshi baadae ukahamia Mbezi.
Ila kwa kipindi alichoishi Moshi na brand aliyoitengeneza kule, sikutegemea kama pasingekuwa kwenye wasifu ulioutoa. Ni kama umzungumzie JK Nyerere halafu usitaje Butiama.
 
Easyfit uzi wako ni mzuri na binafsi nimepata fursa ya kuelewa historia ya huyu binti Mange. Aidha, ushauri ulioutoa hasa kuhusu kuziba ombwe linalotumiwa na Mange. Nasita kukubaliana nawe kuhusu kuruhsu maandamano. Mambo yanayodaiwa na wahamasishaji, yapo yanayoweza kutekelezwa kwa muda mfupi na mengine yanahitaji muda mrefu zaidi. Miye ningeshauri kuwepo na mjadala wa wazi wa mahitaji ya wananchi kama uhuru wa vyombo vya habari n.k. Ni kweli maandamano hasa yenye vurugu yanaweza kuathiri uchumi kwa njia nyingi, mambo hayo yasemwe hadharani na kuwelimisha wananchi.

Viongozi wetu wajitokeza hadharani na kwa lugha za kiungwana badala ya vitisho kutoa maelezo juu ya madai ya wananchi. Mambo ya muda mfupi yafanyiwe kazi na yale yanayohitaji muda mrefu kama katiba, maelezo ya kiungwana na ya kuridhisha yatolewe.

Imani yangu ni kwamba maandamano hayatafanyika; siyo kwa sababu ya vitisho, lkn kwa sababu ya nature na uungwana wa watanzania. Hata hivyo, hata kama hayatafanyika hiyo trh 26/4 hapa tulipofikia tunapaswa kukaa kama taifa na kujiuliza wapi tumekosea na hatua za kurekebisha kasoro hizo zichukuliwe haraka kama tunataka kuendelea kuwa taifa la amani.

Tulipofika leo ni dalili tosha kuwa tuendapo tunaweza kuipoteza amani yetu ikiwa malalamiko yanayotolewa yataendelea kupuuzwa.

Viongozi wastaafu wamsaidie Rais, wanalipwa kwa kazi yao na hata baada ya kazi yao. Uzoefu wao wanaweza kuutumia na kuisaidia nchi badala ya kukaa kimya kama vile hawapo.

Binafsi nawashauri watanzania wenzangu, kuwa hatuna haja ya kuandamana. Tumeijenga nchi kwa muda mrefu, hatuna sababu za kuibomoa kwa siku moja kwa mambo ambazo kimsingi yanatekelezeka kama tutakubaliana kufanya hivyo kama nchi. Siyaandiki haya kwa uoga, lakini kwa kutambua na kuthamini tunu hii ya amani tulionayo ambayo inapaswa kuthaminiwa na kulindwa na kila mtanzania.
 
Katika kosa kubwa sana ambalo serikali ya JPM imefanya ni kumjibu huyu Dada Mange Kimambi juu ya kuhamasisha maandamano ya nchi nzima kupitia mitandao kijamii. Sasa habari zimeenea kila kona. Wengi hawakuwa na taarifa juu ya maandamano ya tarehe 26 /4. Lakini baada ya Magufuli kuyapinga kwa vitisho, Wakuu wa Jeshi la polisi pamoja na mkuu wa mkoa Paul Makonda, sasa kila mmoja kajua.

Nikiwa mtaani, nikapita kwa wazee wenzangu kupata kahawa, kila mmoja anazungumzia habari za maandamano. Jina la Mange Kimambi halikuachwa kutajwa kama kiongozi na mhamasishaji wa maandamano hayo.

Mzee mmoja mwenye heshima zake sana pale mitaa, mstafu wa Jeshi la wananchi. Akauliza " Mange Kimambi ni nani? Anafananaje ? Nataka nimuone tu" haraka haraka nikafungua simu nikaonyesha picha yake, wazee wote walikuja kuchungulia mwanadada Mange Kimambi.

"Kumbe ndo huyu anaitesa serikali hii? Huyu ndio anamtisha Magufuli namna hii? Huyu ndie anaetisha Jeshi la polisi? Kapata wapi hujasiri huu" kweli huyu Dada anamnyosha Magufuli.

Sasa maandamano kila mtanzania anajua, ni bora serikali ingekaa kimya, kuliko kusimama majukwani na kuanza kutoa vitisho vya ajabu zidi ya waandamanaji. Hata yasipofanyika, tayari Mange Kimambi kaishafanikiwa mpaka hapa.
 
mange kawapeleka kibra na wao wameelekea. sasa wamebaki kuweweseka.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom