Who is Salim Ahmed Salim?

Who is Salim Ahmed Salim?

Brutus:

Tofauti ni kwamba huko US Gore alishindwa technically kwea taratibu walizojiwekea wao. Kwetu ni kwamba hao CUF walishinda kwa taratibu tulizojiwekea wenyewe lakini wakanyang'anywa na akina Mkapa.

Sasa ili kupoza hayo makovu ya kunyang'anywa ushindi ndio mambo ya mwafaka yanakuja. Kwa hiyo kwa kifupi ni kwamba miafaka ipo Afrika kwa sababu kuna watu wamejipa hati miliki ya kuwa viongozi wa nchi zao. Siku watawala wakianza kukubali kushindwa ndio mambo ya miafaka yataisha. Na mimi nakubaliana na wewe haya mamiafaka hayana maaan.

Sasa angalia huko Kenya hilo limwafaka lao litamsaidia vipi mwananchi wa kawaida wakati wamepewa liserikali likubwaaaaaa ambao halina umuhimu wala ulazimu wowote!
 
Mimi namchukulia Dr Salim kama kiongozi anaefaa kuongoza Tanzania ya leo.

CV yake inajitosheleza yenyewe na katika masuala ya uhusiano wa kimataifa ndio kabisaa tutamwachia yeye kuhakikisha mabepari hawachoti tu bali pia wanaacha kiasi kikubwa cha utajiri wetu na tule nao 50-50.

Sasa wale wote wasiohitaji maendeleo Tanzania wajiandae, nawapa Dr Salim, Dr Shein, Abdul-Rahman Kinana na Karume imani yangu kwamba wao ndio watatuzi wa matatizo ya Muungano Tanzania.

Kazi ya kwanza na ambayo ni ngumu kidogo na itafanikiwa ni kuifanzia CCM "total purification" na kubaki na NEC yenye nguvu na isio "too concervative".

Hawa jamaa nawaita "unsung heroes" naanza kunigotiate kutafuta election strategists, wapo wengi tu.
 
Mkuu Gamba,

Heshima mbele, tatizo sio CV za viongozi wetu, isipokuwa tatizo ni CV za sisi wananchi wapiga kura, Salim ana CV nzito lakini tatizo ni kwamba urais hauamuliwi na CV peke yake, kwa bahati mbaya pamoja na CV yake kuwa nzito, alishindwa kwenye uchaguzi wa mgombea wa rais wa CCM,

Sasa kama Muungwana tu alimshinda kule CCM, je atawezaje kupambana na kina Freeman, na Lipumba? Na je akikutana na Dr. Slaa sio ndio itakuwa mauti kabisa kwetu CCM! Pole pole ndugu, urais ni pamoja na kushinda uchaguzi,

Salim ni kweli ana CV nzito, na pia ametuweka kwenye ramani ya Dunia politically, lakini tatizo hakuwa na political base nyumbani, kuanzia visiwani mpaka Bara, sasa uongozi wa kubebwa kama wake ulimalizwa na siasa za vyama vingi!

Otherwise, ni kweli CV yake ni nzito sana!
 
Kama mtu akishindwa uchaguzi then analilia serikali ya mseto kuna haja gani basi ya kupiga kura.. kwa nini tusikubaliane tu . leo Rais anatoka CUF... VP CCM... baada ya miaka mitano zamu ya CCM.. VP atoke CUF.?

wakikusoma CUF watakwambia hatukushindwa uchaguzi, tuliibiwa uchaguzi
Kitu kingine; unaposema tujifunze demokrasia kwani lazima tujifunze mfano wa Bwana Kichaka na Gori? taja basi na somo litokanalo na alichokifanya Mandela kule A.Kusini.
 
Brutus:
Tofauti ni kwamba huko US Gore alishindwa technically kwea taratibu walizojiwekea wao. Kwetu ni kwamba hao CUF walishinda kwa taratibu tulizojiwekea wenyewe lakini wakanyang'anywa na akina Mkapa.

FMES na Nyani Ngabu hawakosei kabisa!
Waafrika ndo tulivyo!

Ila mkuu, kwa nini tuwapigie kura watu wasiotaka kutoka madarakani?
Vipi kuhusu watu kama Maalim Seif.. tangu 1995 anagombea yeye tu?
Siku akishinda ataweza kutoka madarakani kwa hiari kweli?
 
Mmmmmmm angalieni sana. Msianze kupigia debe mafisadi wengine. Tunataka mtu safi asiye na doa.

Inabidi usubiri atakeyetumwa na Mungu.. kama ni hawa wanaozaliwa na mwana wa Adamu.. I have very bad news to report to you.. none of them is without a spot! Sorry. Utakuwa na muda mrefu sana wa kusubiri.
 
Mkuu Gamba,

Heshima mbele, tatizo sio CV za viongozi wetu, isipokuwa tatizo ni CV za sisi wananchi wapiga kura, Salim ana CV nzito lakini tatizo ni kwamba urais hauamuliwi na CV peke yake, kwa bahati mbaya pamoja na CV yake kuwa nzito, alishindwa kwenye uchaguzi wa mgombea wa rais wa CCM,

Sasa kama Muungwana tu alimshinda kule CCM, je atawezaje kupambana na kina Freeman, na Lipumba? Na je akikutana na Dr. Slaa sio ndio itakuwa mauti kabisa kwetu CCM! Pole pole ndugu, urais ni pamoja na kushinda uchaguzi,

Salim ni kweli ana CV nzito, na pia ametuweka kwenye ramani ya Dunia politically, lakini tatizo hakuwa na political base nyumbani, kuanzia visiwani mpaka Bara, sasa uongozi wa kubebwa kama wake ulimalizwa na siasa za vyama vingi!

Otherwise, ni kweli CV yake ni nzito sana!

Piga picha mwalimu angekuwa hai halafu Salim akagombea 2005.
By the way, ya 2005 yashapita 2010 lugha yaweza kuwa nyingine kabisa hasa baada ya kuona Vasco alivyochemsha.
 
Pamoja na CV yake huyu jamaa ni nabii asiyeheshimika nyumbani! Unaweza ukajiuliza ukashindwa kupata jibu hivi JK ameshindwa kabisa kumtumia Salim kwa sababu gani! Bado ana visa vya wakati wa uchaguzi! Jamani hii ni nchi ya watu, si ya viongozi!

Pamoja na ubaya woote wa Mkapa mbona alimpa yeye JK uwaziri wa nje kwa miaka yote kumi! Mimi kwa kweli sioni senior politician mwenye sifa nyumbani na nje kama Salim! Au JK anamwogopa Karume! Mimi naamini JK hana sifa ya kiongozi mwenye upeo, dira na nia safi na makini kwa taifa hili. Amejaza wababaishaji!

Ona sasa! nadhani anashindwa hata pa kushika, mikashfa kila mahali!Bado anashindwa kutoa maamuzi! Akubali kujifunza na pia akubali kuwa urais ni kazi kubwa sana na ni kazi takatifu, haihitaji usaniii.

Huyu jamaa ataondoka madarakani akiwa ametuacha midomo wazi, hakuna atakachofanya mabali ya smile kama Dwight Yorke kwa wapenzi wa mpira! Hivi hata huko singida aliko kunanoga kweli! Ngoja wananchi waanze kumuuliza maswali ya moja kwa moja!
 
wakikusoma CUF watakwambia hatukushindwa uchaguzi, tuliibiwa uchaguzi
Kitu kingine; unaposema tujifunze demokrasia kwani lazima tujifunze mfano wa Bwana Kichaka na Gori? taja basi na somo litokanalo na alichokifanya Mandela kule A.Kusini.

Ishu ya South Afrika ilikuwa tofauti kabisa.
Strategically ilibidi kuwe na 2 vice presidents Frederik Willem de Klerk na Thabo Mbeki.

Na kwenye usalama wa raia ilibidi Chifu Buthelezi awepo kuweza kuleta utulivu Kwazulu-Natal maana wafuasi wake wa Inkatha Freedom Party (IFP) walikuwa bado wanaleta violence!

Baada ya kufanya mabadiliko ya serikali hakuna tena mseto!
Sisi hatuna hili tatizo!
 
Ishu ya South Afrika ilikuwa tofauti kabisa.
Strategically ilibidi kuwe na 2 vice presidents Frederik Willem de Klerk na Thabo Mbeki. Na kwenye usalama wa raia ilibidi Chifu Buthelezi awepo kuweza kuleta utulivu Kwazulu-Natal maana wafuasi wake wa Inkatha Freedom Party (IFP) walikuwa bado wanaleta violence!Baada ya kufanya mabadiliko ya serikali hakuna tena mseto!
Sisi hatuna hili tatizo!

Mzee mmoja huwa anapenda kusema hivi;
Bingwa wa ligi kuu sio timu ya taifa
Besides, Vasco mwenyewe alikiri tuna mpasuko, na huo mpasuko ni gonjwa ambalo lisipotibika twafa. Umesahau kulitokea nini Januari 2001
 
Marketing Strategies hizo!
Nikitaka kukuudhia bidhaa nitatafuta lugha yoyote itakayokuingia akilini ili nikuchomoe senti zako!

Tunaweza kusema lolote kuhalalisha hoja zetu.. lakini ukweli utabaki pale pale! We don't need Miafaka whatever u call them!

Ni utumwa wa kiakili!
We can do better than that if we want to!
 
Marketing Strategies hizo!
Nikitaka kukuudhia bidhaa nitatafuta lugha yoyote itakayokuingia akilini ili nikuchomoe senti zako!
Tunaweza kusema lolote kuhalalisha hoja zetu.. lakini ukweli utabaki pale pale!
We don't need Miafaka whatever u call them!
Ni utumwa wa kiakili!
We can do better than that if we want to!

Yaani wewe unaona miafaka isiwepo, jamii moja ya wazanzibari iendelee kususiana misiba, kupeana talaka,kuvunja undugu na kuachiana safu misikitini nk, may be you dont know how terrible the mpasuko is
 
Tatizo la watu kama Salim ni tabia ya woga, au nidhamu za kinafiki; au ukipenda sema ni 'diplomatic approach' anazozitumia.
Yaani hata kuzungumzia mambo mazito yanayotokea nchini kama ufisadi, au kichama kuwa cha mabepari inakuwa ni shida?

Ulishamsikia wapi Ahmed Salim akichukua msimamo ulio wazi kupinga mambo yanayowadidimiza wananchi. Kuwa kiongozi ni pamoja na kuchukua 'risk'. One has to stick out a neck - sio mambo ya ku-comform tuuu siku zote! In fact ni nyakati kama hizi ndio tungekuwa tunawasikiliza viongozi imara wakisimama kuhesabika.
 
1. Ulishamsikia wapi Ahmed Salim akichukua msimamo ulio wazi kupinga mambo yanayowadidimiza wananchi.

2. Kuwa kiongozi ni pamoja na kuchukua 'risk'. One has to stick out a neck - sio mambo ya ku-comform tuuu siku zote!

3. In fact ni nyakati kama hizi ndio tungekuwa tunawasikiliza viongozi imara wakisimama kuhesabika.

I love Jambo Forums, kila ukifikiri umemaliza kuhesabu members vichwa, anatokea mwingine ohh thank God for JF!

Mkuu Kalamu never before like this, hapa inapaswa kuwa mwanzo na mwisho wa mjadala!
 
I love Jambo Forums, kila ukifikiri umemaliza kuhesabu members vichwa, anatokea mwingine ohh thank God for JF!

Mkuu Kalamu never before like this, hapa inapaswa kuwa mwanzo na mwisho wa mjadala!

hapana bwana, mjadala unaendelea, haujaisha
 
Ni wangapi wako tayari kumsupport Salimu kama akiwa tayari kutaka kugombea? Nani atakuwa tayari kumsupport na kujibu mashambulizi...
 
Yaani wewe unaona miafaka isiwepo, jamii moja ya wazanzibari iendelee kususiana misiba, kupeana talaka,kuvunja undugu na kuachiana safu misikitini nk, may be you dont know how terrible the mpasuko is

Muafaka ndio utakao ondoa hayo mambo....?
Huo mpasuko umeletwa na hao wanasiasa kwa sababu ya tamaa zao za madaraka wakati wao nyuma ya pazia wanachit chat vizuri na wanaenjoy posho kutoka kwa "mahasimu wao".

Kuhusu Salim kuzungumzia maswala yanayoendelea nchini...sina la kusema ila mwenyewe si alishasema siasa za Tanzania basi.
 
Yaani wewe unaona miafaka isiwepo,

Hii miafaka ni ujinga na watse of our national time and money, uchaguzi umefanyika upande mmoja ulioshinda umeibiwa kura, ulioiba kura unasema tuwe na muafaka!

eti suluhisho ni kuwa na serikali ya mseto, only in Tanzania, halafu tuna maneno mengi kuhusu Zimbabwe, kumbe sisi ni afadhali hata Mugabe aliyekalia matokeo!
 
CCM wakituletea huyu 2010 mbona nitawapenda!!, kama hawataweza kumwambia Vasco da Gama aachie usukani, basi angalau wamsimamishe Visiwani Zanzibar.

To be frank am impressed with the idea...wazo la mgombea binafsi huenda likatutoa watanzania kwenye matatizo ya kudumu..especially kwa hiyo combination ya Dr Salim na Dr Slaa...wabadhirifu lazima wakione cha moto...
 
I love Jambo Forums, kila ukifikiri umemaliza kuhesabu members vichwa, anatokea mwingine ohh thank God for JF!

Mkuu Kalamu never before like this, hapa inapaswa kuwa mwanzo na mwisho wa mjadala!

Hii ya Kalamu hata mimi imenikata maini kabisa pamoja na mapenzi yangu kwa Salim. Yaani huyu bwana hutakuja kumsikia akinyanyua mdomo kabisa kuhusu uozo wote unaendelea. Sasa wakati mwingine tunashindwa kujua convictions zake ni zipi na kama hatujui convictions zake anatukwaza sana sisi wapenzi wake kumtetea mbele ya vichwa kama akina FMES!

Hata hivyo nafikiri huyu mzee wetu walishamjeruhi sana na sidhani kama anaweza kuuzika tena na kukabili mashambulizi ya wanasiasa wa leo TZ.
 
Back
Top Bottom