Who is Salim Ahmed Salim?

Hivi kuna mtu anayejua yaliyomkuta huyu Mzee mpaka akashindwa kuwa rais wa Tanzania japo alikuwa kipenzi cha Nyerere, CCM, Tanzania na Africa kwa ujumla?

Nitaomba kama kuna mtu anaweza kuwarejesha wana JF wenye kupia nondo kama Mwanakijiji, Halisi, Pasco, William Malecela, FMES, Rev Kishoka na bila kumsahau Mkandara na Mohammed Said kama wakiwepo wa Zanzibari pia njoon mtuletee ukweli wa huyu jamaaa kuanzia alikoanzia, shule alizosoma, alipokuwa Foreign, OAU na baada ya kurudi Tanzania, kutaka kugombea uhuru na status yake hivi sasa.

Naomba sana mfunguke kwa style ya orijino JF
 

Kutokana na historia ya siasa za Zanzibar hawawezi kumweka Salim kugombea uraisi,hawamkubali kwasababu hajui matatizo ya zanizbar,huyu ni mtanganyika kazaliwa tu zanizibar,wazanzibar ndio waliotia fitna salimu asipewe urais alipotaka kugombani uraisi wa JMT
 

Kutokana na historia ya siasa za Zanzibar hawawezi kumweka Salim kugombea uraisi,hawamkubali kwasababu hajui matatizo ya zanizbar,huyu ni mtanganyika kazaliwa tu zanizibar,wazanzibar ndio waliotia fitna salimu asipewe urais alipotaka kugombani uraisi wa JMT
 
Pamoja na uzoefu wake huyu jamaa na tena Mzanzibari sijui kwa nini CCM hawamtumii kwenye muafaka. kweli huyu asingeweza kutoa mchango maridhawa kwenye Muafaka wa zenji?

Nabii hakubariki kwao
 


wewe muongo..CV ya Dr. Salim haiwezi kuwa fupi kiasi hicho. Mwaka 2008 CV ya Dr. Salim ilisomwa pale Nkurumah UDSM kwa dakika arobaini na tano, leo imekuwa fupi kiasi cha ukurasa mmoja tu!!!!
 
Nianze kwa kusema mimi ni mmbara naisitoshe ni mkristo. Baada ya kuangalia wagombea wate waliojitangaza kwa mtazamo wangu bado sijaona mwenye nia ya dhati kuongoza nchi especially wagombea uraisi kutokea bara. Kama ningekuwa nauwezo wakusuggest nadhani tunge wapa this time Zanzibar watuongoze after two terms za wa bara.

Na pia nadhani Salim will be the right man to lead us. Mawazo yangu tu.
 
Hakika nilipoisoma Historia ya Mh.Salim Ahmed Salim nilikubali kuwa kiongozi huandaliwa.

Hayati Baba wa Taifa Mwl.Julius Kambarage Nyerere ndie kiongozi aliyemwibua Balozi Salim Ahmed Salim Na kumpa Ubalozi akiwa Na umri mdogo. Mh.Salim Ahmed Salim alijisomea Na kupata Degree mbalimbali, Mh.Salimu Ahmed Salim anajua zaidi ya lugha 5 za Kimataifa, Balozi Salim Ahmed Salimu alikuwa Muafrika wa kwanza kugombea Nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Balozi Salim Ahmed Salimu amekuwa Katubu Mkuu wa Umoja wa Nchi huru za Afrika Balozi Salim Ahmed Salimu amekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania.

Hakika Balozi Salimu Ahmed Salim ni Mtanzania aliyeitangaza Tanzania Duniani kote.Nachukua nafasi hii Kumpongeza Balozi Salim Ahmed Salimu Kwa Utumishi wake uliotukuka katika Kiwango cha hali ya Juu.

Nawaomba Watanzania wenzangu tujenge utamaduni wa kuwapongeza Na kuwashukuru watu , makundi au Viongozi walioitangaza Nchi Yetu ndani Na nje ya Tanzania.
 
Huyu ndio alitakiwa awe Rais mstaafu wa Awamu ya nne sema uarabu wake ulimponza.

Aendelee kuwa kimya tu maana nayo ni burasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…