Who is Salim Ahmed Salim?


Hapo sasa, watu wengine wameigueza CCM kuwa dini yao!!
 

Kijiji chake kilijifia; ukimuuliza anakwambia serikali ilimfanyizia kwa kumnyima bajeti.

Salim anaweza akaenda kwa Shayo, lakini it will be a very poor political calculation! By the way, kwa wale wanaomini kwamba falsafa na sera ndio tatizo la vyama vyetu, nawashauri wasome falsafa na sera za Prof Shayo. Nafikiri kama tunachagua kwa kuangalia sera, hakuna chama chenye sera bomba TZ na Afrika kwa ujumla kama sera za chama cha Prof Shayo.
 

Kalamu, heshima mbele Mkuu.

Ni sifa adimu, adimu mno ambayo unaiongelea hapo. Salim nadhani hana hiyo, nakubali. Nina ka anecdote kaliko nifundisha hilo. Nimewahi kukutana na S.A. Salim kwenye msafara wa Mkapa ng'ambo. (Unajua Watanzani ughaibuni ndio wana access ya one-on-one na viongozi kuliko wakiwa Bongo - ingekuwa nchi nyingine watu wange riot kwa hili).

Nikamuuliza kuhusu gaffe zilizo jaa kwenye spichi Mkapa aliyo kuwa ametoka kuitoa. Spichi ilikuwa imejaa ma recitation ya salamu za mafanikio kutoka Tanzania. Basi, jamaa alianza kumtetea Mkapa, Sisiemu na Serikali kama kada wa chama wakati wa uchaguzi. Nakwambia nilipigwa na butwaa. Mkapa alikuwa ana spew jibberish, za Pinda zimenyooka. Huu ni wakati ile migodi iko mwenye yard sale, kwa hiyo hata huhitaji kusikia alichosema Mkapa kuamini pointi yangu on the merits.

Nikaondoka pale nasema Salim pia? Duuuh!
 
...It is always possible to possibily the impossibilities... watu wamesulubiwa, wakafa, wakafufuka na kwa mkwala wakapaa mbinguni.. then wakaahidi watarudi kama walivyopaa... sembuse waafrika kujitawala bila kutegemea wakoloni????

Incendiary!
 


Kuhani Mkuu:

Worshipping dictators is a pain in the a$$. Viongozi wa Tanzania walipambwa kwa sababu ya vyombo vya habari kuwa chini yao lakini wengi wao ni pain.
 
Wakulu,

..hivi kuna Mtanzania yeyote yule anaweza kutuonyesha mchango wa Salim Salim ktk jambo lolote la maendeleo Tanzania?

..nadhani kazi zinazomfaa huyu Mzee ni hizo za kwenye majukwaa ya diplomasia na siasa za kimataifa.

..Salim angekuwa na interest na siasa za ndani, zile zinazohusu mustakabali wa maisha ya walalahoi, angeutema ubalozi na kuingia Ubunge.

..sijapata kusikia kama Salim Salim alisema kazi za nje zimemtosha anataka kurudi nyumbani kujenga nchi? wako wenzake waliotema Ubalozi na nafasi za kuteuliwa na kuamua kujenga nchi wakiwa wabunge tu.

..siasa za "kuandaliwa" kuwa Raisi zimepitwa na wakati. kama mtu anataka the highest office in the land basi aanzie chini at least kwenye Ubunge. tumpime uongozi wako umelete matunda gani kwa wananchi wake.

..Uraisi siyo lelemama. unahitaji mtu anayeijua nchi, wananchi wake, na matatizo yanayowakabili.

..Kule Njombe mtu anayekurupuka kugombea madaraka baada ya nafasi kutokea huulizwa ALIKWINAA.
 
Jokakuu,
Unajua mambo haya mnayarudisha tena upya lakini tulishazunguzia kabla ya Uchaguzi 2005.

Niliwahi sema kwamba hakuna candidate mzuri zaidi ya Salim ndani ya CCM ktk wakati wa uchaguzi uliopita, akina Yakhe nyie mlimpamba Kikwete hadi wadanganyika sie tukafuata kama bendera leo tena mnakuja na mpya zenu baada yaa.

Na ajabu ni kwamba leo mnakuja andika vipande kuhoji tena alichokifanya wakati akishika wadhifa ndani ya serikali yetu as a fact na mnaelewa wazi kuwa Salim aliweza kufanikisha kila jukumu alopewa ktk nafasi zoteee!. Akiwa balozi China aliweza kutuletea mradi wa reli ya Tazara na akiwa UN ndiye akiyeshinikiza Uhuru wa South Africa baada ya nchi za magharibi kukubali kuweka vikwazo vya kiuchumi.

Sasa wewe nambioe kuna kiongozi gani Africa hii anaweza ku reason na viongozi wa magharibi hadi wafikie kubadilisha mawazo yao. Kifupi kwa ncjhi za magharibi kuiwekea vikwazo South Africa ni sawa la leo atokee kiongozi kuwaambia mataifa makubwa kuwa Israel inatakiwa kuwekewa vikwazo vya kiuchumi.

Mbali na Uhbalozi Salim kisha shikamadaraka ndani ya nchi kama waziri wa Ulinzi na waziri mkuu yote haya mnaamua kuyafukia, lakini msitafute ni wakati gani Salim kashika nafasi hizo. Wakati ambao nchi yetu ilikuwa na matatizo makubwa ktk jeshi ama kuuza sera za chama kitaifa.

Yes alikuwa natatizo moja la kuwa Mjamaa ambalo ktk dunia ya leo halina nafasi. Hakuna kingozi hata mmoja anayefuata siasa za Kijamaa kwa maana ya Ukomunist kwani dunia imebadilika Kiuchumi.

Labda ni swala la kumuuliza yeye mwenyewe kama atakuwa rais ni msimamo gani wa kiuchumi atauchukua maanake CCM wenyewe hawanajulikani kama ni Progressive ama Conservative. Ndani ay CCM kuna makundi na sifahamu Salim kasimama kundi gani na nini mrengo wake binafsi.

Ni ajabu sana chama tawala hakina mrengo zaidi ya maandishi ambayo yana tafsirika tofauti.
 



Hiyu ni Salim aliyekuwa OAU mkuu kabisa wakati wale Wanyarwanda na Warundi wanakufa anangoja UN hadi Clinton akasema waache wauane wakichoka wataacha?

Nielewesheni hapa jamani sijaelewa shujaa yupi tuna mwongelea hapa .
 
Inabidi usubiri atakeyetumwa na Mungu.. kama ni hawa wanaozaliwa na mwana wa Adamu.. I have very bad news to report to you.. none of them is without a spot! Sorry. Utakuwa na muda mrefu sana wa kusubiri.

Mzee mwanakijiji napingana na wewe kwa hilo, yes tunao watu safi sio akina MR "Clean" unawajua wewe wenye nia na moyo wakuongoza nchi hii kwa mafanikio ya kila mtanzania ila nafasi hiyo hatuwapi, au wanaikosa kwa sababu hawapo kwenye mtandao.
 
TANZANIA YA LEO HAIWEZI TAWALIWA NA MWARABU....MAISHA YAKE.
 
Mkandara,

..sijahoji uwezo wa Salim Salim ktk masuala ya diplomasia na siasa za kimataifa.

..kinachonikwaza mimi ni kwamba Salim Salim hana rekodi inayopimika ya kushughulikia matatizo ya wananchi wa kawaida. pia hana rekodi ya kupimika ya kushughulikia matatizo ya kiuchumi.

..kuhusu Tazara kuna mambo mengi sana yaliyopelekea kupatikana kwa mradi ule.

..hivi una uhakika kwamba bila Salim Salim wachina wasingetupa msaada wa reli?

..Kuhusu Salim Salim kuwa Mjamaa, which i doubt, hizi siyo zama za Itikadi. Kama ni Maraisi Wajamaa tulishakuwa nao, tena wakereketwa kuliko huyo Salim Salim.

..Tatizo langu na Salim Salim ni kwamba sioni kama ana interest na siasa za ndani za Tanzania, other than seeking the country's highest office. kama Salim angekuwa na interest na siasa za ndani basi baada ya kushindwa Uraisi angetafuta jimbo akagombee ubunge.

NB:

..niliwahi kuonya zama zile kwamba Kikwete hatatufaa. nasikitika kwamba utabiri huo unaelekea kuwa kweli.
 

Nashindwa kukuelewa Ben, Makamba anahusishwa vipi na na uchimi, yeye si katibu tu wa Chama?, nafikili kushindewa kwetu kwa uchimi na nchi jirani ni swala la rais na wizara husika

usiwe na chuki binafsi na chama, hayo ni maoni tu
 
Lunyungu,
Itakuwa vizuri ukitwambia nafasi yake OAU wakati mauaji ya Rwanda yanafanyika na pia kama hakuweza kuwakilisha swala hili ktk vyombo vinavyohusika.

Usianze kumlaumu mtu kwa sababu tu unafikira kwamba alikuwa mahala fulani badala ya kufikiria angeweza vipi kutatua matatizo hayo ktk wadihifa wake..
 
TANZANIA YA LEO HAIWEZI TAWALIWA NA MWARABU....MAISHA YAKE.

Jamani acheni ubaguzi. Tukitoka hapo tutasema Tanzania haiwezi kutawaliwa na Mchagga, au Mhaya, au Mnyakyusa, ad infinitum. Salim ni Mtanzania, full stop!
 
Jokakuu,
hivi una uhakika kwamba bila Salim Salim wachina wasingetupa msaada wa reli?
Mkuu mchango wa balozi ni mkkubwa sana katika maswala ya diplomasia laa sivyo tusingekuwa na haja ya kuwa nao... unless unataka kunambia hufahamu umuhimu wa mabalozi. Balozi kama Sifue wa Marekani ni balozi bora kwa sasa hivi ndiye aliyewezesha maziri mkuu wa Canada kuja Tanzania na pia ziara ya Kichaka hivi majuzi.. balozi kama huyu anastahili kila sifa..
..
Kuhusu Salim Salim kuwa Mjamaa, which i doubt, hizi siyo zama za Itikadi. Kama ni Maraisi Wajamaa tulishakuwa nao, tena wakereketwa kuliko huyo Salim Salim.
Kweli kabisa hapa tupo sote!
Mkuu angeweza vipi kutafuta jimbo wakati kesha jiandikisha kugombea Urais? ni wakati gani unaozungumzia hapa.

Yeye ni mwana CCM, chama ambacho kimemkuza na kumboresha kuwa kiongozi bora na ktk kufahamu huko pengine yeye pekee ndiye angeweza kuleta mabadiliko.. Hamkutaka!

Kisha huwezi kuwa na mapenzi na wananchi ikiwa hupewi nafasi.. hivi kweli hujapata kujiuliza kwa nini Salim toka Nyerere ameopndoka amenyimwa kabisa nafasi ndani ya serikali hizi za mafisadi?

There must be something haiwezekani kabisa atemwe kiasi hiki hasa ukija zingatia nafasi alizowahi kushika ndani na nje ya nchi yetu..
 
Mkandara,

..kuna Watanzania kama Salim Salim ambao walidiriki kuutema Ubalozi na kurudi nyumbani kujenga nchi.

..Kuna wengine walikataa ukuu wa mikoa na kuamua kurudi majimboni kwao kutumikia wananchi.

..watu kama hao wananipa ushawishi zaidi kwa nafsi zao zinawatuma katika kushughulikia matatizo ya wananchi wa kawaida.

..labda mimi na wewe tunatofautiana jinsi tanavyoiangalia hii nafasi ya Raisi wa Tanzania. binafsi naangalia matatizo yetu, historia yetu ktk kuyashugulikia, yalishughulikiwa na watu wa aina gani, kabla ya kuamua ni nani anatufaa ktk zama hizi.

..mashaka yangu na Salim Salim ni kwamba kuna uwezekano mkubwa interest yake ikawa kwenye siasa za kimataifa, zaidi ya masuala ya ndani ya maendeleo ya Mtanzania wa kawaida.

..leo hii ukitembea nchi za nje kuna watu wengi wana-identify Tanzania na Nyerere kuliko mlima kilimanjaro, tanzanite, au serengeti. Wakati wenzetu wa Kenya wanakuwa indentified zaidi na mlima kilimanjaro na Maasai Mara kuliko Mzee Jomo Kenyatta.

..majuzi Raisi Kikwete amekwenda kutatua mgogoro wa Kenya. Baada ya hapo Wakenya wametufunga goli wanafungua mtambo wa kusafisha almasi ambayo itakuwa inatoka Tanzania!! kumbuka kwamba hata sisi tulipatwa na matatizo hapa na Wapemba wakakimbilia Kenya. je, ulimsikia Mzee Moi au Mwai Kibaki kujishughulisha na matatizo yetu.

..Mimi nafikiri Raisi anayetufaa ni yule atakayejielekeza zaidi ktk siasa za ndani kuliko za nje. Sababu hizo ndiyo zinazonifanya nisimfikirie Salim Salim kwa nafasi ya Uraisi wa Tanzania.
 
Huyo mtu mnayemsifia kwa ma honorary Doctorates sio msafi kama mnavyodhani. Ulizeni TTCL aliwafanya nini?

Zimbabwe wamemchagua Morgan Tsvangirai hata darasa halijui. Afrika ya kusini wanampenda Jacob Zuma. Hajui hata darasa lilivyo. Mnadhani hawana akili? Tunataka kiongozi mwenye uchungu na nchi hii siyo ma CV uchwara. Kwa hilo la huyo mpemba JF mnachemka.

Kwanza hata kipindi chake cha ukatibu mkuu wa OAU jambo gani la maana amefanya?
 


Raia bora kwanza karibu hapa .
Salim hapa anapingwa na wengine wanamkubali ndiyo uhuru haina maana ya kusema JF tunachemka maana nawe ni mwanachama utakuwa unachemka pia .Nakubaliana nawe kwamba Salim asingaliweza kuwa Rais mzuri nan hana sifa za uongozi kabisa .
 
Iandikwe hivi bwana, S.A.S THE DELAYED PRESIDENT
akingali hai u never know
Siku akitwaliwa hajawa ndio biography za never became ziandikwe.

Salim Ahmed Salim
The President delayed

Sio mbaya pia ingawa ninajua kabisa kuwa hana nia kabisa na siasa na hana wazo la kuwa Rais. Hata hivyo anaweza kuwa drafted na Watanzania wanaomwona aweza kuwa Rais mzuri kwa Taifa letu....... Draft Salim, 2010.

Salim-Slaa ticket kinda possible!!!!!! Tuendelee kujadili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…