Who is Salim Ahmed Salim?

KIMSINGI SALIM HATAKUBALI TENA KUGOMBEA URAIS..KWA SABABU HATA HII 20005 ALIGOMBEA KWA KUOMBWA....NA ZAIDI AKAKATISHWA TAMAA NA KAMPENI CHAFU ZA JK.....

HISTORIA ITAMPA NAFASI STAHILI...AANDIKE VITABU NA KUTOA MIHADHARA VYUO VIKUU ZAIDI SASA!![/B]

Mkuu Kibunango,

Kwanza heshima mbele, niarudia kuwa Salim kwangu hafai kuwa rais wetu kwa sababu hana sifa zinazotakiwa, je unanielewa lakini sina tatizo kuwapa wanaotaka kunilkazimisha!
Mkuu FMES
Jumla ya mjadala huu mrefu na mkali umehitimishwa na maneno ya Phillemon Mikael kama yanavyosomeka hapo juu.
 
1.
KIMSINGI SALIM HATAKUBALI TENA KUGOMBEA URAIS..KWA SABABU HATA HII 20005 ALIGOMBEA KWA KUOMBWA....NA ZAIDI AKAKATISHWA TAMAA NA KAMPENI CHAFU ZA JK.....

HISTORIA ITAMPA NAFASI STAHILI...AANDIKE VITABU NA KUTOA MIHADHARA VYUO VIKUU ZAIDI SASA!!
[/B]

2.
Jumla ya mjadala huu mrefu na mkali umehitimishwa na maneno ya Phillemon Mikael kama yanavyosomeka hapo juu.

Mkuu Kibunango,

Kama maneno ya hapo juu yanamaliza mjadala, mimi kwangu naona kwamba kama ninayaelewa vizuri basi hata mjadala haukutakiwa kuwepo kabisa, kwa sababu kumbe tulikuwa tunajadili kiongozi aliyeombwa kugombea urais, lakini yeye binafsi hakuwa na hiyo nia, wewe huoni kuwa ilikuwa ni waste of time hata kumjadili as we did? Maana kama ni kampeni chafu hata alipogombea ukatibu mkuu wa UN si tunajua kuwa nako alipambana na kampeni chafu ambako tunasikia Uarabu/Uafrika wake ulikuwa tatizo kukubalika na wakubwa wa dunia?

Halafu hii historia itakayomhukumu stahili, itaandikwa na nani? Si walioko kwenye power, kweli watamhukumu inavyotakiwa? Maana Mkapa tu hajamaliza hata miaka miwili nje tayari historia imechafuka walioko kwenye power,

Mkuu mjadala ni safi, lakini unaweza kuendelezwa tukajifunza zaidi!
 
Wabaguzi wote wanampinga salim leo na walimpinga kwa sababu moja tu ..UBAGUZI..

LAKINI TUWEKE RECORD WAZI...SALIM NI SHUJAA WA TAIFA HILI!!!

..REKODI YA SALIM KUWA WAZIRI MKUU...pekee kutoka zanzibar ni wazi ..haitatokea tena..kwani uwaziri mkuu ni nafasi ya tanganyika....!!

salim anajivunia utanzania kuliko uzanzibar ambao wabaguzi wanataka kiwe kigezo....kuwa mlezi wa ccm tabora inatosha kumuweka karibu na wananchi...

wote mnafahamu majeraha ya the so called MAPINDUZI MATUKUFU.....yameondoa sultani weupe yakaweka weuzi....wenye haki ya kutawala...hata leo shein akitaka urasi watasema ni mpemba!!!!..upemba ni disqualification!!!

ukweli ni wazi baada ya zanzibar kuikataa nafasi ya kumpitisha salim...hatakaa atokee tena rais kutoka zanzibar..sioni mwenye sifa!!...zanzibar ndio walimpa ushindi jk...kura 500 alizopata salim ni za bara..zanzibar voted jk as a block ..walikuwa na kura 500 wangempa zote salim angeshinda au kungekuwa na re run ..na hilo lingetokea wapenzi 200 wa mwandosya wangempa salim na angeshinda !!!!...tatizo ni ile hotuba ya mwenyekiti mkapa pia ilimkandamiza salim na hii NI BAADA YA KINA JK MUFUATA MKAPA NA SECRET FAILI LAKE..LA AMBAYO HATA HIVYO YAMEISHIA KUIBULIWA LEO!

ukweli ni wazi kikwete alishinda primaries kwa hila na majungu ..na ndio ameyakalia hadi kesho...sidhani kama atakuja kuwa kati ya mashujaa wa taifa letu!
 
1.
Kwa hiyo mkuu hapa Mwinyi, Dr. Omari Juma, Shein, na Salim, wanakuwa mashujaa wa taifa kuweza kushika nafasi nzito za jamhuri wakitokea huko visiwani, au?

2.
Very strong point, lakini ndio political realities za bongo, ambazo tunajua ziliko anzia, lakini great education.
 

"I do want to write, but not my memoirs. The problem with memoirs is that people talk to me in confidence about sensitive issues, including what are deemed top state secrets. I cannot betray their trust," he explained. "Moreover, I will inevitably annoy, even anger, many people if I do so. Prickly events are still fresh in people's minds, others ongoing.

Many distinguished personalities in Africa and abroad might feel embarrassed if I write freely and honestly about my experiences working with them or about the roles they played in the often turbulent and controversial developments that swept the continent in the past decade. Too many feathers will be ruffled at this particular historical juncture,"
 


mkuu salim close allies can still advise him to write his memoirs inspite of the fact that it may tend to uncover many secrets..yet he can go ahead..i dont see a prolem if he write the memoirs today and release them 15 years later..hata secret files za secret service huwa zinafunguliwa baada ya miaka 25 hadi 30..naamini akiandika leo hadi kuja kuzindua kitabu siri nyingi zitakuwa zimepita kwa sababu tangu amestaaafu ni miaka mingi sasa..in his presence or without..the mentality he has may end up depriving tanzanians,african and general world the right access to his experience ..we have lost that opportunity with mwalimu failing to write his memoirs in time ..we wish not to lose that again ...huyu ni ,mtanzania i can say baada ya mwalimu anayefahamu mengi kuhusu dunia..

i would be happy if our message raches him....pia ningependa tufikie mahali watanzania waliotia fora na wasomi ..wanapostaafu watumiwe na vyuo vyetu vikuu ili kujenga kina salim ,mongela,tibaijuka,asharose wa baadaye..they will not be like normal proffessors rather they will be like inspirations to our youth!
 
1.


Very strong point, lakini ndio political realities za bongo, ambazo tunajua ziliko anzia, lakini great education.

FMES, it doesn't have to be that way!!! Zitto amezungumzia hapo awali kwamba tatizo ni mfumo uliopo. Siasa za Tanzania si kwamba ni chafu na unahitaji kuwa mjanja, ni kwamba it is tasteless, exploits the poverty and ignorance of people, ni ya kubabe na cha character assasination.
Ukiniambia mbona nchi zingine ziko hivyo sikubali kwa upande wa nchi ambazo tunaona wamekomaa kisiasa kwani there's a strong media, si wale wanaonunuliwa na akina RA kwa sh laki 5 -laki 5!

Salim was ready to play the political game, but a proper one si ya kishenzi kama ya Bongo. Eti kuwalipa takrima mashabiki waje kumbeba anapozunguka mikoani, na kuwalipa laki 5 waandishi. Alikataa akijua that it is WRONG, sasa according to your argument hii ndio kosa lake!?

Alafu tunalia na Kikwete na ufisadi! Si ndiyo inapoanza. Kama mtu ata-purchase urais unafikiri tutapata rais gani? He has already paid to be elected, so wananchi: SHUT UP and watch him loot himself sick with his buddies, si walitumia hela nyingi kumfikisha alipo? Do you see how sick the system is? Do you agree that this is not a healthy environment for a decent person to run for presidency?

Tatizo wabongo we don't call a spade a spade, tunaleta unafiki tu, eti Kikwete alishinda! NO he paid for the kura and CCM members were ready to sell democracy and the future of our country down the river for a few millions, secrets to remain secrets, etc We are now paying the price alafu tunamlaumu Kikwete! No, si mlimsifia na kum-reward yeye and his cronies that they know how to 'play'the game. Unafikiri with this argument what kind of leaders can we expect?

I accept and respect your opinion kwamba unaona SAS hafai kuwa rais, even though I think otherwise, lakini naona kama unataka kumpunguzia sifa unfairly just to make a point. Mi nadhani kila mtu amekubali mchango wake SAS, swali labda does he have the temperament and is ready to sink as low to become president? He answered No! Alafu mnasema ni arrogant? I think he was smart enough to assess what happened and realized that politics in Tanzania is immature, brutish and childish.

Mi nasema unless we change the system and say ENOUGH to such base politics tusitegemee kupata viongozi bora. Hata Slaa, Zitto na other opposition figures wataendelea kuota ndoto tu ya kutawala! Alafu mnauliza kwa nini hawashindi? The system has been bastardized and rigged from the beginning that if you are honest you are the 'sissy' and if you are a thug you are rewarded!

Nilishasema it is our loss not SAS's loss.
This was a very good discussion!
 
The system has been bastardized and rigged from the beginning that if you are honest you are the 'sissy' and if you are a thug you are rewarded!

Susuviri,

Ni nani aliyetufikisha hapa? What Salim has to say kuhusu wizi wa uchaguzi kule visiwani mwaka 1995?
 
Susuviri,

Ni nani aliyetufikisha hapa? What Salim has to say kuhusu wizi wa uchaguzi kule visiwani mwaka 1995?

Nani aliyetufikisha hapa?
- Swali zuri sana na niko tayari kufungua thread mpya kujadili hili. Lakini kwa kifupi mimi naamini system hii ilianza baada ya kifo cha Nyerere. Kukawa sasa hakuna yule Benevolent Dictator ambaye alikuwa anatuambia tufanye nini na vipi. Sasa tukabaki kuona viongozi wetu walivyo na uchu wa madaraka ambapo kila mtu anajiona sawa.

Muhimu ikawa sasa kutishiana nani mbabe zaidi, au wananchi wanamkubali nani etc.
What Salim has to say kuhusu wizi wa uchaguzi kule visiwani mwaka 1995?
- Naomba nionyeshe data nilizopata huko UN:

Hivyo ninavyoelewa alikuwa nje ya nchi mwaka huu wa 1995. Sidhani kama ilikuwa vyema kwake kuzungumzia masuala ya ndani ya nchi zaidi ya kusihi pande zote mbili (CCM na CUF) wakae chini na kufikia maelewano au muafaka.
 
Salim Was My Ccm Candidate Then, Sasa It Is Too Late Considering Miaka Kumi Ile Yetu Tunayowapa Marais Wa Ccm Zawadi.

Bora Jina Jipya.
Halafu He Is Too Clean And Straight Forward Haya Mambo Ya Kitanzania Yatampa Pressure Bure, Mwacheni Atulie, Tunaapreciate Sana Kazi Yake.
 
Nina hakika Field Marshall Es anafahamu wazi mchango wa Salim ktk kuijenga Tanzania isipokuwa nadhani mwenzetu anakwenda hatua moja zaidi ya kutafuta kiongozi ambaye yuko tayari kuubeba msalaba asulubiwe ktk kutetea haki ndiye anayefaa kuitwa shujaa.

Nakumbuka tuliwahi kuzungumzia swala hili ktk mada moja siku za nyuma inayohusu Mashujaa na nakumbuka yeye mwenyewe alisema mashujaa ni watu kama Mandela ambao walijitoa mhanga pale haki ilipokosekana.
Tofauti na mawazo ya wengi kati yetu ni kwamba Tanzania haikufikia hali ya kutafuta wabeba msalaba ktk wakati wowote wa Utawala wa Nyerere, Mwinyi ama Mkapa isipokuwa tulihitaji kiongozi mwenye uwezo wa kuwajenga wananchi imani mpya ya MAPINDUZI ya KIFIKRA.

Kwa hili nawashukuru sana watu kama Dr.Slaa, Zitto na pengine chama kizima cha Chadema kwa mbinu zao ja kujaribu kujenga upya imani za wananchi kwamba Tanzania yetu sio nchi maskini isipokuwa umaskini wetu unatokana na mfumo mzima wa Utawala.

Sasa mtu kama Salim, mheshimiwa Field Marshall ES hawezi kumweka ktk kundi la mashujaa kwa sababu hayupo kundi moja na kina Mandela, Slaa na Zitto na hakuna wakati wowote ktk Utawala wa Nyerere, Mwinyi, Mkapa ama JK ameweza kusimama against the Government pale yeye FMES anaona haki ilikosekana.

Na ndio maana mimi muda wote nimemwambia kwamba Salim ktk wakati wote wa Matatizo Tanzania alitupwa nje na kafungwa kamba za miguu.. Hii ilikuwa ni jeuri ya mwalimu ambaye alifahamu uwezo wa Salim. Ni pale tu alipotaka kujiuzuru ndipo alipomrudisha Salim nchini na kwa bahati mbaya kama inavyojulikana viongozi wa CCM Zainzibar(baraza la Mapinduzi) ambao wali hijack Mapinduzi kisiasa walikataa pendekezo la mwalimu ikiwa hana jinsi isipokuwa kumweka Mwinyi.

This guy hakuteteleka wala kuonyesha dalili ya kudhoofika na kukataa position ya Waziri mkuu ama wadhifa uliofuata.
Mkapa pia alihakikisha mtu huyu anatupwa nje tena kuondoa upinzani ndani hivyo bado sii rahisi kumshutumu Salim anapolitumikia taifa kama walivyofanywa kina Sarakikya na kundi kubwa la wafuasi wa mwalimu ambao walipingana sana na mfumo huu mpya wa kiutawala.

Tatizo la mkuu wangu FMES ni pale anaposhindwa kuona siasa za CCM kama ni Mafia na kwamba watu kama Malecela, Msuya, Nyalali, Warioba, Mrema na wengine wengi waliobakia ndani ni miongoni mwa watekelezaji wakubwa wa siasa za Udikteta wa mwalimu na ndio maana pamoja na makosa yao yote bado walikuwa na nafasi kubwa ndani ya chama cha CCM...Hawa ndio walikuwa watu wa - YES SIR! na mwalimu alifahamu hawana uwezo wa kufikiria nje ya siasa za Kigamboni. They were good leaders na hakika hadi majuzi kama sio leo maisha yao ni sawa na Wadanganyika wengi walalahoi.

Tatizo kubwa ni huu utawala mpya wa Mkapa aliyekuja na mfumo wa CHUKUA CHAKO MAPEMA. Naweza sema ulianza toka awamu ya pili ya Mwinyi ambaye alikuja tangaza Azimio la Zanzibar ambalo kwa mara ya kwanza viongozi wetu waliona nafasi ya kuvuna kile walichokipanda ktk retirement zao...

Hivyo, shujaa wa leo ni yule atakayeweza kusimama dhidi ya UFISADI..yule atakaye weza kuwaelimisha Wadanganyika millioni 40 kuondokana na UPUUZAJI (negligence) na UVIVU (incompetence) wa kufikiri...

Ni kazi kubwa sana na inahitaji nguvu sio ya mtu mmoja kwani Umaskini wetu haswa unatokana na Upuuzaji na uvivu wa kufikiri kiasi kwamba hadi leo hii ni wachache sana wanaoweza kusema CCM has to go!

Out of 40 millioni naweza sema ni aslimia 10 tu ambao hadi leo hii wamejenga fikra mpya za kutopuuza ama kufanya uvivu ktk maswala ya maslahi ya nchi kiasi kwamba viongozi wetu kina Kikwete wanafahamu fika kuwa wakati huo bado..Kundi kubwa la wananchi bado ni wapuuzaji na wavivu wa kufikiria kwani tumeshazoea maisha ya Umaskini.

Ni kazi mpya ya watu kama kina Dr. Slaa na Zitto kuendelea kuuza siasa hizi mpya za kumkomboa Mtanzania toka ktk dimbwi hili la Umaskini wa kutofikiria.

Hata hivyo jitihada zao zinapigwa vita na kuna watu wanaamini kabisa kwamba wanaopata elimu hiyo ni watu wachache sana labda tone ktk bahari na utawakuta hapa JF na baadhi ya vijiwe (blogs) lakini sio ktk vyombo vikuu vya habari kama vile TV na magazeti yanayowafikia wananchi hadi vijijini...Ni kazi nzito sana..

Nitamalizia kwa kusema kwamba, Mheshimiwa Salim kwa yale aloweza kuyafanya chini ya Utawala wa mwalimu na wakati mfupi sana ndani ya serikali yetu chini ya Mwinyi unatosha kabisa kumpa sifa ya Ushujaa kwa sababu sii lazima mchezaji acheze dakika 90 kuipata sifa ya ufungaji goli.

Machache aloweza kuyafanya ktk muda mfupi ndani yasiwe sababu kubwa ya kuondoa ushujaa wake ati kwa sababu tu alitumikia Taifa letu nje zaidi ya ndani. Yale Mapinduzi za Zanzibar tu kumwondoa Sultan yalitosha kumpa sifa ya Ushujaa na sio watu kama Karume waliodandia sifa hii waka hijack Utawala wa visiwani. Bila shaka kwa tendo hilo tu hawezi kupendwa na pande zote mbili iwe Hizbu ama ASP..kama alivyoondoka Abraham Babu bila kupatiwa heshima ya kitaifa.

Nitafurahi sana kuona kama ataweza kuandika kitabu kinachoeleza mchango wake ktk maisha yake alotumikia taifa na Ulimwengu kwa Ujumla.
 
Mkandara: as always excellent analysis! Nimekukubali mkuu!
Nadhani huu uvivu wa kufikiria ndo unaotuangusha siku zote, pia ushabiki! Lakini ushabiki mzuri kwenye mpira au hata katika siasa za wenzetu lakini si katika siasa zetu za ndani kwani inarudisha tu maendeleo.

Kuna ulazima mkubwa wa kuanzisha mjadala yaani dialogue miongoni mwetu kitu gani kifanyike ili tuweze kubadili mfumo uliopo na kuchagua viongozi bora kama SAS.
 
Salim mbona kichwa mazee si unafiki wa wana-CCM kuangaliana sura kaka vinginevyo angekamata nchi nina imani huu uchafu unaondelea sasa usingetokea vinginevyo wampige kipapai ubongo ujikoroge.

Lakini tuombe uhai tuifikie hiyo 2010 huenda mwenyezi mungu akawabadilisha akili akawa-nominated yeye au ndio mpaka muungwana nae amalize terms zake 2 hata kama amechafua hali ya hewa?

Inawezekana eh!! teh!! teh!! tehtehteeeeh!!!mavyama mengine bwana mh!!!
 
Mkuu Bob,

Nimekusikia na heshima mbele, lakini I am not moved, ninataka kiongozi wa kuweza kusimama mwenyewe kwa miguu yake, hawa mafisadi wanataka wanaume kama Zitto, Slaa, Mwakyembe na Mama Kilango,

Samahani mkuu kina Chenge, Mkono, na the likes hawajui diplomasia, ninataka kuongozwa na kiongozi anayesema msimamo wake wakati maovu yanapotokea kwenye taifa lake hata akiwa China au NY, ninataka kiongozi atakayesimama mbele ya hadhara na kusema wazi kinachomkereketa mpaka anataka kuniongoza,

Ninaelewa mapungufu ya Muungwana as rais, lakini bado ninaheshimu the hustle yake mpaka kuchaguliwa, that is wassup! Salim anafaa kuwa balozi wetu huko nje, au kuwa mwenyekiti wa UN na mambo ya nje nje tu, huku bongo maji ni ya shingo, kama hawezi hizi pilika pilika za kushindana kina Muuungwana, nchi yangu ikishambuliwa itakuwaje itakuwa diplomasia? The man is arrogant, alikuja Dodoma akijiamini kuwa atapita tu kwa kampeni ya kupigiwa na kina Warioba na Butiku, wewe huoni kuwa that by itself was a big joke? Mtu kichwa kama Salim anawezaje kuwaamini hawa Pwagu na Pwaguzi?

One day wanasema hawataki rushwa, halafu Lowassa anajiuzulu kwa sababu ya rushwa wanalia tena kuwa ameonewa? Warioba Bunda kumemshinda mpaka ilibidi wazee huko CCM wamuombe aaache maana ni aibu, Butiku ndio hivyo Mungu nisaidie, hawa ndio wapiga kampeni ya urais wa mtu kichwa kama Salim? Salim ana uwezo wa diplomasia za nje, lakini uwezo wa siasa zetu za local hana na sasa hivi tayari maepitwa na wakati, maana yeye alifikiri kuwa Butiku na Warioba bado wana ule ule ujiko kama wakati Mwalimu alipokuwepo, ndio kupitwa kwenyewe na wakati huko, maana hata hawezi soma upepo wa siasa zetu,

Ninasema hivi, kweli Salim CV yake ni nzito sana, na ana sifa kubwa sana huko nje, anahitaji kugombea ukuuu wa UN, sio bongo hawa kina Mkapa na Kiwira hawahitaji diplomasia, wanachohitaji ni wanaume kama DR. Slaaa!

Otherwise, wakuu ninawasoma na elimu yenu nzito sana kuhusu uwezo wa Salim, samahani kwamba I am not convinced, na sina tatizo personal na any of you, naona wengine mnajaribu kunishambulia personal kwa sababu tu mawazo yangu juu ya mgombea wenu hayakubaliani na yenu, lakini I am too big for that, maana mimi ninasimamia taifa langu tu na siamini kuwa Salim ana uwezo wa kuwa rais anayefaa kwa taifa langu ndio maana alishindwa na akirudia atashindwa kabisa na nitajiunga na kampeni against kambi yalke tena kiroho mbaya!

Mimi sina ushabiki wala unazi, what you see hapa ndio what you get in me, straight talk, na jina langu ni moja tu, maneno mbele na vitendo inapobidi, Salim abaki huko huko alikokimbilia baada ya kushindwa, na sisi bongo kama kawaida tutaendelea kuwajali waliopo hapa bongo kwanza, kabla ya hao wa kutoka nje, wakishindwa wanarudi huko nje, saa ya uchaguzi ikifika wanakuja maana sisi bongo tumelala sana!

Ahsante Wakuuu, tuendelee kukata ishus!
 

Huo ubavu hana ingawa itakuwa a good idea, maana atakapojibiwa ya kwake, ya kuanzia wake za watu, uzinzi wake, mlinzi wake aliyekufa bila habari kamili, ushiriki wake kwenye siasa za visiwani, tabia zake anapokuwa kwenye kitengo cha kazi, connections zake na the Arab world, mkuu yote anayajua kuwa kuna watu wanayo, akiandika tu atajibiwa kwa hiyo ni both ways, sidhani kama angependa hayo,

Ingawa inaweza kuwa ni saafi sana akiandika something serious for once tukamsoma mawazo yake, maana so far hatuyajui zaidi tu ya kubuni na kueletewa article ambazo hakuandika yeye!!
 
1.
Halafu unasema kuwa hapa watu ni washabiki na wanazi, na kwamba wanapindisha ukweli, hivi kweli inaweza ku-get lower than hayo maneno yako hapo juu?kwenye hizo lines?


2.
Alikuwa nje, kwa hiyo Mwalimu alikuwa anajaribu kupitisha kivuli chake Salim kule Dodoma, kabla ya kumpitisha Mkapa? au?
 
Halafu He Is Too Clean And Straight Forward Haya Mambo Ya Kitanzania Yatampa Pressure Bure, Mwacheni Atulie, Tunaapreciate Sana Kazi Yake.

Mkuu wangu tema mate chini kwanza, maana huna uhakika na unachokisema hapo juu!
 

Susuviri,
You have a very strong point here; u-rais wa kununua - which is precisely why I am saying everybody, including the Salims who saw and decided to look the other side, even not saying a word long after the fact - wana-fail na hawafai katika uongozi wa nchi yetu.

Hata tukiacha mambo ambayo labda wengi tunayachukulia kuwa ni 'controversial' kama ufisadi; je kweli kiongozi atashindwa kuwa na mjadala hata wa kiujumla tu unaohusu maswala ya kimaendeleo ya nchi? People like Salim have to articulate ideas, (not necessarily on controversial issues) and citizens will have a basis of judging their leadership capacity on those ideas.
 
Field Marshall Es,

Mkuu heshima mbele na sidhanikama kuna sehemu nimejaribu kuvuta sheatni wako isipokuwa nimeeleza kwa kirefu nilichoelewa mimi kutokana na msimamo wako.

Ni kweli kabisa Salim hawezi kushika Urais wa Bongo kwa sababu ya Uharamu wa siasa zetu, sasa nikitazama swala hili kwa makini inaonyesha wazi unajaribu kuhalalisha vitendo vya kina Kikwete na Mkapa kuwa ndio wanaume na wanatakiwa wanaume wengine kina Slaa kwa kupitia mlango huo huo kupigana na viongozi kama Mkapa.

Mkuu tuzungumze kwa kuwatazama watanzania wenyewe kwanza. Hizi habari za kuchukua Ikulu by any means necessary zinaweza kumharibia mtu kama Dr. Slaa kwa sababu kinachogomba hapa ni uwezo wa mtu KUONGOZA..na sifa za kiongozi ni ktk usukani na kubadilisha gear sio swala nla nani anaonekana vizuri akiwa ktk driver's seat.

Hawa wajinga walikimbilia mlango wa dereva kuendesha mwenyewe hawajui hivyo haiwezi kuwa sifa kwa Slaa naye akimbilie tu usukani kugombana na washenzi.

Hawa wote ulowataja ni watu ambao sote tulidhani wana liseni ya kuendesha kumbe fake... na mada hii inazungumzia zaidi uwezo wa mtu kuendesha, sasa kama Salim liseni anayo na umekubali anaweza kuendesha gari hili isipokuwa hana Ubavu wa kupambana na madereva wabaya, sidhani kama utakuwa umetusaidia ktk hoja hii.

Nitarudia kusema kwamba Ushujaa wa Salim na uwezo wa kuongoza Tanzania anao na pengine ana qualify zaidi kuliko kiongozi yeyote tuliye naye leo hii isipokuwa wakati wake umeshapita.
Hizo hadithi za watum kuandika kitabu kuonyesha uzinzi wake na kadhalika ni hadithi za jikoni mkuu kwa sababu nani kweli atakaa hapa na kusoma kitabu kinachomzungumzia Salim nyumba alizowahi kupita, wengine hapa tunakaa kimya tu mbona tunajua relation ya Mwinyi alipokuwa akija mtaa wa Mahiwa Kariakoo kuvizia mke wa pili.

Nyerere mwenyewe hakuwa safi, huyo Mkapa ndio usiseme kabisa maanake inasemekana alikuwa akipiga mke wa Mramba wakiwa bado ktk ndoa. Kikwete ndio kabisaaa yaani ktk maswala hayo hakuna msafi na siasa za Zanzibar huwezi kabisa kumweka ktk kundi moja na wahuni wengine kwa sababu hakuwa na Muda wa kuishi Zanzibar wala kuendeleza siasa za Zainzibar akiwa nchi za nje.

Sema nachomkubali ni tabia yake akiwa kazini ya kutokubali upuuzi wa kujuana na ku favour mtu kwa sababu tu mnatoka nchi moja. Wapo Wadanganyika kibao wamefanya nae kazi na wamemshtumu sana na hata kumwita arrogant kwa sababu hakuwajali ama kuwapendelea wao kama Watanzania.

Hii ndio hulka ya Mdanganyika yaani akisha kuwa ndugu yako anataka anina fulani ya attention na p[engione kujikosha kuwa mnafahamiana.. Salim ni mtu asiyependa uvivu ktk kazi, mpango wa kusukana nywele kazini na hadithi za saloon ama migahawani.
Hizi zote ni sifa ambazo kwa sababu sio reflection yetu sisi basi bila shaka naweza kukubali kuwa hafai kuwa kiongozi na wala hastahili sifa za Ushujaa wa mdanganyika mvuvi wa kufikiri.

Kwani hata Kinjeketile anaweza kuitwa shujaa pamoja na kwamba matokeo ya mbinu zake zilitughalimu zaidi kimwili lakini pia zilitufumbua macho zaidi ya kuelewa kuwa wazungu walikuja kututawala na sio wapita njia ama wahamiaji (immigrant) ktk makazi yetu. Kifikra aliweza kutukomboa zaidi kama matunda ya vita ile ya Majimaji.

Usishoke mkuuu hii ni kutaka kumfahamu zaidi salim pengine zipo hoja ambazo hatujazisikia hapa na zitatusaidia sote.
 

Mkuu Mkandara,

Hapa nakupa 10/10

Natamani JF ifike hadi "remote areas" za Tanzania kwa njia ya internet au TV.

Kule ndio kuna wajinga ambao hata hawajui kwamba kuna ligi kuu ya soka ya Vodacom Tanzania achilia mbali mambo ya Andrew Chenge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…