GAME THEIRY,
Unapomsema Salim kutazama ndugu yake mkuu ebu kwanza rudi nyuma uzitazame mila za Mdanganyika.....
Tupo kibao ambao tuna ndugu zetu, wazazi wetu wanapuyanga mitaani utafikiria hawa jamaa hawana ndugu wanaojiweza.
Kumbuka tena kuwa viongozi wetu ni binadamu kama sisi wenye kufikiria kama wadanganyika wengine hivyo hawapo mbali na ukweli wa FMES kuwa wao ni reflection yetu sisi tofauti moja tu wameweza kushika madaraka na kuitwa waheshimiwa
Ni mila ya Mdanganyika kutojua kurithisha elimu wala mali zake, utasikia usia usiokwisha jinsi yeye alivyoweza kufanikiwa. Leo hii wapo wazee kibao wamefikia jua la magharibi kimaisha lakini bado wanaendesha biashara zao bila hata kuwahusisha ndugu wala watoto zao, kutokana na kikorosho cha maisha....Na ndio maana wazee wetu wakisha kufa huondoka na kila kheri kiasi kwamba majeshi huandaliwa siku msibani.. Mali itagawanywa, hata nyumba za marehemu zitauzwa kwa sababu sio mila yetu kurithiana elimu, mali, ujuzi ama biashara..sisi hugawana kilichopo na msiba ndio mwanzo wa hujuma za kuua undugu... Hua naelewa sana tunapolia sana kilioni sio kuondokea tu bali balaa linalofuata ni kubwa.. halibebeki.
Hata hivyo, ukitazama upande wa pili wa shilingi hii hii utawakuta ndugu wanaokaa wakitegemea uwashushie rehma. Hawapendi kujituma kikazi wala kutafuta maisha nje ya riziki za wazi kama vile ndugu aliyejaliwa..Kwa bahati mbaya hawa hawa ndugu hufuja mali na pengine hata kuharibu jina la mhusika wakitumia address yako... wao hutuita sisi kina CHUMA ULETE...
Kuna wakti hujiuliza ni mbinu gani haswa inayotakiwa kwetu sisi ku deal na ndugu, jamaa ama jamii hii ya wadanganyika.
Nitakupa mfano mdogo sana, rafiki yako akija na shida ya kukopa fedha basi ni afadhali umpe bure kwa sababu hawezi kuzirudisha atakutia ndani. Ukimwamini ndugu, rafiki na hata mzazi wako kwenye fedha atakuzika sii rahisi hata kidogo kumpata mwaminifu atakayekuwa na uchungu na mali yako ama wadhifa wako. Kwa hiyo yawezekana kutokana na kijimila kama hiki ndo tumepata utaratibu wa KILA MTU NA MZIGO WAKE.
Hivyo basi ni vizuri sana kama ukitafuta undani wa mtu huyo kwanza kabla hujamlalamikia Salim, yawezekana mazishi na mtu anayesubiri kuletewa..na sababu moja kubwa uloitaja wewe mwenyewe.
Kama yukokweli London (nchi yenye kila opportunity) na hana mahala pa kulala wakati sii mlemavu basi nadhni hiyo pekee imekueleza mengi kuhusu huyu jamaa.