Mkuu Mwanahabari,
Consultancy kila mtu alizifanya lakini ni wazi kuwa hizi sio ajira za kumpa mtu kipato cha kila mwezi, na ndio maana hufanyika nje ya muda wa kazi. Mwandosya ana mambo mengi ya kujibu, tokea 1985 alipoingia serikalini hadi alipokuwa PS wa wizara ya viwanda na biashara 1992-93 na baadaye uwaziri. Lakini tokea alipoupata u-PS & uwaziri , Mwandosya alibadilika na kuwa tajiri overnight, kama ilivyo kawaida kwa baadhi ya mawaziri wetu mafisadi na maPS wetu. Hapa ndio panapoleta maswali hasa ukitilia maanani kuwa ndio kipindi hiki pia alichoweza kupeleka watoto ughaibuni. Ukiongezea na ununuzi wa ndege mbovu ya raisi, Mwandosya anabaki kuwa wa maswali mengi hadi atakapoeleta majibu yake.
"What is the cost of the pride of the nation? The number does not mean anything as long as we buy the plane, maintain it and look after the welfare of our people". -Mwandosya on the purchase of the controversial Presidential Jet.
_______________________
napingana kabisa, consultants kama Mwandosya wanalipwa ajira kubwa tu, pamoja na kuandika (na kuuza vitabu kadhaa) muda wakati hakuwepo kabisa serikalini, na watoto wake wamekuwa nje wakati hayuko kabisa serikalini na akijiendeleza na private sector huku bado akishika nafasi nyingi tu kwenye makampuni tofauti ambayo yanalipa. Kupeleka watoto nje kwa mtu kama Mwandosya kipindi ambacho hakuwa kabisa serikalini siyo kitu cha kushangaza. pamoja na kuwa chairman wa SIemens Tanzania, TPDC, Director Standard CHartered.. na mengine mengi (wakati hakuwepo serikalini 1993-2000), inasikitisha sana kuona kwamba watanzania wenye kazi halali na uwezo wanahusishwa na ufisadi.
Watoto wote wamesoma nje wakati Hakuwepo kabisa serikalini, wote walienda nje after 2 years yeye kuondoka serikalini.
Nenda Amazon ukaone bei ya vitabu alivyoandika vinauzwa kwa bei gani, kwa hiyo tu mtu yoyote anaweza kupeleka watoto shule.
Kuhusu ndege ya serikali, kwanza G550 siyo mbovu (muulize John Mkony, ceo tgfa - Pilot wa Rais atakuambia), Jk haitumii kwa sababu anazozijua mwenyewe preferres to fly first class commercial including entourage yake kubwa tu, inatumika zaidi na Dr. Shein na wengine. Hata watu binafsi wanaweza kukodi ndege za serikali. Kama argument ni bei ya ndege, G550 ilinunuliwa kwa bei halali kuzingatia specific options serikali ilizochagua zikiwemo custom designs and performance specifications suited for operating in our conditions and usage specification(thats another argument though, maana tukinunua bei rahisi mnaona yanayotokea ---> richmond) hii hapa gulstream ikiwa Cologne this Feb
http://www.planepictures.net/netshow.php?id=718457
Labda kama kuna maswali ni vizuri kuuliza kuliko kuhukumu mtu amepataje utajiri au kama una data mpya tuko wengi hapa tunapenda kujua, na kusema alibadilika kuwa tajiri overnight kama kigezo ni kwamba alisomesha watoto wake nje ---> kazi lizokuwa anafanya nje ya kuwepo serikalini zinalipa vizuri tu na mtu yeyote mwenye kazi kama hizo anaweza kusomesha mtu.
Bali nakubaliana na wewe, kila mtu ana maswali ya kujibu na wengine kama Chenge, Lowassa Karamagi, Rostam wote tunaona paper trail na majina yao yanakjitokeza kila sehemu, kama kuna mtu ana data za Mwandosya kuhusika na mambo haya, wekeni humu watu wachambue.
Flashback from JF
Salma atesa na ndege ya Kikwete
Ni ile ambayo rais anaogopa kuitumia kikazi Ulaya
Aipanda kwenda na kurejea katika ziara binafsi
Aitumia kuendea sherehe za mila za Mswati III
na Mwandishi Wetu
BAADA ya Rais Jakaya Kikwete kuogopa kutumia ndege yake iliyonunuliwa kwa mabilioni ya shilingi bila idhini ya Watanzania, sasa ndege hiyo inatumiwa na mkewe, Salma katika ziara binafsi.
Mara ya mwisho, Salma alitumia ndege hiyo kwenda kwenye sherehe za kimila nchini Swaziland, kushuhudia Mfalme Mswati III akichagua mke wa 13.
Uchunguzi wa Tanzania Daima umethibitisha kuwa Salma aliondoka Dar es Salaam Agosti 29, mwaka huu saa tisa jioni, akiwa amepanda ndege hiyo aina ya Gulfstreame Jet Engine kwenda Manzini, Swaziland.
Ndege hiyo ya rais namba 05H-ONE, iliondoka Dar es Salaam kuelekea Swaziland, alikokuwa anakwenda kuhudhuria sherehe za kimila, ambazo baadaye zimeshutumiwa na wanaharakati kwamba zinawadhalilisha wanawake.
Septemba 5, mwaka huu, ndege hiyo ilimfuata na kumrejesha Dar es Salaam.
Kwa hakika haya ni matumizi mabaya ya ndege ya rais, kwa kuwa mke wa rais, si rais, na hapaswi kuitumia kama anasafiri peke yake kwa safari binafsi.
Fursa pekee aliyonayo mke wa rais kutumia ndege hiyo, isiyoweza kunungunikiwa hata kidogo, ni pale anaposafiri na mumewe katika safari za kikazi.
Matumizi haya ni kashfa nzito kwa serikali ya awamu ya nne, inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete, aliyesema tangu awali kwamba urais wake usingekuwa wa ubia na mtu yeyote.
Miezi miwili iliyopita, gazeti hili liliandika habari kuwa Rais Kikwete anahofu kupanda ndege hiyo katika safari zake za kikazi Ulaya, kwa madai kuwa ni gharama kubwa mno kwa nchi maskini kama Tanzania.
Badala yake, ameazimia kuitumia katika safari za Afrika, hali inayotafsiriwa pia kuwa anaona aibu kupanda ndege ya kifahari kwenda Ulaya kuomba misaada kwa serikali zinazoongozwa na viongozi wanaotumia ndege za kawaida katika safari zao za kikazi.