Wanajamii,
Kila ukanda una nchi ambayo inachuliwa kama super power. Mfano S.Africa ni top kwa ukanda wa southern, Egypt north, nigeria West Africa na Angola Central Africa.
Sasa ndani ya jumuiya ya Africa Mashariki nani zaid? Wanansema Kenya je ni kweli? na tutumie vigezo gani ku-grade nchi.
hivi Angola iko Central Africa? hii ni mpya kwangu, au ni kwa vile nilisoma Janja janja Primary School na hatukuwa na mwalimu wa Jogi???
by the way...swali lako ni subjective na linaweza kuwa na jibu zaidi ya moja kutegemea na vigezo unavyotaka kutumia:
1. Kiuchumi na Maendeleo ya kijamii ya vitu na watu....hakuna ubishi Kenya wako mbali sana
2.Kisiasa....again Kenya wametuzidi, wakati sisi tunapiga porojo za katiba mpya, kenya walishaipata hiyo kitu ingawa ni kwa mbinde sana, jambo baya lakini uzuri wake ni kuwa mchakato wake una political legitimacy ya wananchi wakati sisi kila mtu,
"tunamshukuru Mh...kwa kutuletea katiba mpya....." maana si haki yetu bali favour fulani. Pamoja na ufisadi uliotamalaki Kenya lakini huwezi kumsikia rais wao akijitapa, mafisadi nawajua na dawa yao iko jikoni...kiama chao ni Oct 31(kumbuka kauli ya mkulu pale mjengoni back in 2009 nadhani).
3. Kijeshi...hili ni gumu kusema maana hyo mambo ni siri sana, lkn pengine sisi tukawa zaidi maana kwa asili nchi za kijamaa zimewekeza sana kwenye majeshi hasa kwa kuwa na jeshi lenye askari wengi na ukizingatia kuwa sisi tu wegi zaidi kwa idadi ya watu.
kwa kifupi nadhani Kenya wametuzidi na pengine ni kwa kukubali hilo ndiyo sababu sisi tumekuwa wazito na kwa kweli tuawaogopa sana wakenya katika kuelekea kwenye shirikisho la Afrika Mashariki.
Mwisho...siku hizi hilo neno Superpower halitumiki sana....nchi hazilinganishwi kwa u-superpower bali kwa economies zao na ndiyo maana utasikia the largest economy in the world ni USA, ikifuatiwa na China, Japan, Germany......etc.
biashara ya u-superpower ilikwisha na Cold War, kuanguka kwa USSR, Yogoslavia, CheckSlovakia, Berlin Wall na kuungana kwa Ujerumani mbili.