WHO: Marekani kusitisha kugawa ARVs bure, itasababisha vifo vya watu Milioni 3

WHO: Marekani kusitisha kugawa ARVs bure, itasababisha vifo vya watu Milioni 3

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya maambukizi mapya ya HIV zaidi ya milioni 10 na vifo vya Watu milioni 3 vinavyohusiana na UKIMWI vinaweza kushuhudiwa kufuatia kusitishwa kwa msaada wa kigeni wa Marekani unaosaidia upatikanaji wa dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI, ARVs.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus WHO amesema hatua ya Marekani kujiondoa kusaidia mapambano ya HIV imeathiri usambazaji wa dawa katika nchi saba za Afrika, zikiwemo Kenya, Lesotho, Sudan Kusini, Burkina Faso, Mali, Nigeria, na Haiti, ambazo zinaweza kuishiwa dawa ndani ya miezi michache ijayo.

Dr. Tedros amesema kusitishwa kwa msaada huo wa Marekani kunaweza kufuta mafanikio ya miaka 20 katika kupambana na HIV huku pia akionya kuwa juhudi za kudhibiti magonjwa mengine kama polio, malaria, na kifua kikuu zimeathirika vibaya na ameiomba Marekani kuhakikisha kuwa inatoa muda wa mpito kwa nchi zilizoathirika ili ziweze kupata vyanzo mbadala vya fedha badala ya kusitisha msaada kwa ghafla

Itakumbukwa Rais wa Marekani, Donald Trump alitangaza mwezi huu kusitisha kutoa fedha za misaada kupitia miradi iliyokuwa chini ya Shirika lake la misaada la USAID, hali iliyoibua taharuki hasa kwa nchi nyingi za Afrika zinazotegemea fedha za ufadhili kushughulika na magonjwa kama Ukimwi.

who.png


===============================================================


The World Health Organization's chief says deaths from HIV, malaria and other diseases will surge if the US drastically cuts foreign aid.

WHO Director-General Tedros Adhanom Ghebreyesus told reporters in Switzerland on Monday that his organization is already seeing the impact of reductions in such assistance by the Trump administration.

The US president has moved to slash health spending, including suspending foreign aid provided through the United States Agency for International Development. It will also terminate about 80 percent of USAID projects.

Tedros said disruptions to the supply of medicines is severe and will hit especially hard as Africa struggles with a high number of HIV cases. He said such cuts could lead to 3 million HIV-related deaths, more than triple the number last year.

Source: NHK World Japan
 
Si mliletea vigisu kwenye Corona na mkaikumbatia china aliyesababisha,
Mwambien china asaidie kama mchina ana hayo Mambo ya haki ya mtu kuishi, tutakimbiana tu muda si mrefu!
 
Tatizo ukimwi unaitesa sana Afrika, na Afrika imeshindwa kujikomboa.
ingekuwa Ukimwi unasumbua sana Ulaya au mataifa ya wenzetu' suluhisho lingeshapatikana.
 
dozi ya chini kabisa ya ARVs inauzwa elf 80 kwa mtu amabye yuko tayari kwenye matumizi na vidudu vimefubazwa yaan viral load iko vinzuri amabayo inadumu kwa muda wa miezi miwili ambapo kwa kadirio la juu ni tshs 1500 kwa kidonge kila siku
ukiangalia kwa jicho la kizarendo na kwa mujibu wa takwimu za ukimwi serikali ya tanzania ikiamua kuweka ruzuku na kununua hizo dawa bila dalali yaan kizarendo upo uwezekano wa mgonjwa kuweza kuchangia tshs 500 mpkal 300per kidonge na kama selikari ikaamua kwa dhati

yaan goli moja la mama kwa simba na yanga linaokoa maisha zaidi ya watu 100

katika watu milioni 60 tanzania kuna watu milioni 1.5 wanaoishi na virusi vya ukimwi
good news ni kuw maambukizi mapya yamepungua kwa kiasi kikubwa ina maana ndani ya miaka kadhaa mbele ukimwi utakuwa umepungua kwa kiasi kikubwa tanzania kutokana na dawa za kufubaza
kama serikali haijachukua hatua stahiki mapema ni kweli juhudi zote zitakuwa bure
 
Tatizo ukimwi unaitesa sana Afrika, na Afrika imeshindwa kujikomboa.
ingekuwa Ukimwi unasumbua sana Ulaya au mataifa ya wenzetu' suluhisho lingeshapatikana.
Suluhisho lipo isipokuwa ni biashara
JFK alipotaka kusitisha vita VIETNAM walimshoot 7bu alitaka kuharibu biashara

gari ya kwanza ya umeme ilikuwa mtaani tangu miaka 1800 mwishoni

Elon musk alisema miezi 6 kabla kuwa COVID itakwisha hivi karibuni wakati huo bado mapambano yanaendelea ya COVID sheria kali na blah blah za nafasi mita 1
na ikawa hvyo watu wakawa busy na vita vya ukraine na urusi COVID ikasahaulika ikapotea
 
Suluhisho lipo isipokuwa ni biashara
JFK alipotaka kusitisha vita VIETNAM walimshoot 7bu alitaka kuharibu biashara

gari ya kwanza ya umeme ilikuwa mtaani tangu miaka 1800 mwishoni

Elon musk alisema miezi 6 kabla kuwa COVID itakwisha na ikawa hvyo watu wakawa busy na vita vya ukraine na urusi COVID ikasahaulika ikapotea
Suluhisho wanalo mataifa ya wenzetu!
Afrika tunasubiria muujiza
 
Back
Top Bottom