WHO wanaposisitiza nchi zitoe takwimu badala ya dawa ya Corona nayo ni Siasa ya Dunia

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2011
Posts
1,684
Reaction score
2,156
Kwa level ambayo dunia imefikia kwa sasa sio rahisi kuamini kwamba hadi sasa dunia imeshindwa kupata dawa au njia sahihi ya kuthibiti kirusi cha Corona. Ikumbukwe kuwa jamii ya kirusi hiki kipo tangu siku nyingi kitu kinacholeta ukweli kwamba tayari wanasayansi walikwishafanyia utafiti siku nyingi jamii ya kirusi kinachofanana na kirusi hiki.

Sasa haiingii akilini kila siku WHO na mashirka ya kimataifa yanasisitiza zaidi nchi kutoa takwimu za walioathirika, kupoteza maisha na wanaopona na wanafikia hatua ya kutilia mashaka idadi za vifo kwa baadhi ya nchi badala ya kusisitiza uharakishwaji wa kutafuta dawa kuokoa maisha ya watu. Hapa ndipo siasa ilipo.

WHO imekuwa kama agent au middlemen wa mataifa makubwa kuwatengenezea soko kwa kulazimisha nchi zihesabu idadi ya wateja waliokwishaingia sokoni wakati wababe wa dunia wakiendelea kugombana nani dawa yake iingie sokoni. Na kwa vyovyote vile Marekani anahofu china asijekuteka soko la corona kwa kuuza mashine na dawa maana atakuja kupindua meza ya kuwa kiongozi wa dunia

Dunia inaelekea kurudi kwenye utaratibu wa kawaida kwa kuondoa masharti yaliyowekwa awali lakini siku hadi siku takwimu zinazidi kuongezeka duniani kote, sababu zinazofanya hizo nchi kulegeza masharti sio kwamba kirusi kimeondoka la hasha ila wanaanza taratibu kuja na siasa nyingine kwamba hiki kirusi kuna uwezekano tukaishi nacho

wakati huo huo China na Marekani kila siku wanapigana vijembe. Wametoka kushutumiana kwamba china imeleta corona na marekani walileta UKIMWI sasa hivi wanashutumiana kudukuliana formula za kutengeneza chanjo. Hii ni rahisi kuamini hata hizi takwimu wanazitaka ili wajue ni wateja wangapi wameshaingia sokoni kwa chochote watakacholeta kitumike kama dawa ndiomaana hawataki mitishamba yetu ya kiafrika isijekupunguza soko walilo target.
 
Mkuu mashirika hayo wao ndio wanaoyafadhiri mapesa kibao unataka yamtii nani?

Si nasikia sisi ni donor country tunaweza kujitoa umoja wa mataifa tujitegemee kama north korea ili kuepukana na hayo unayoita manyanyaso
 
Hili suala linanipa ukakasi kwa nini takwimu na kwanini malumbano ya mataifa mawili tu China na Marekani?

Nafikiri kuna jambo linaendelea nyuma ya pazia inahitaji akiri kubwa sana kung'amua.
 
Hivi hujui hata umuhimu wa takwimu sahihi?
 
Hili suala linanipa ukakasi kwa nini takwimu na kwanini malumbano ya mataifa mawili tu China na Marekani?

Nafikiri kuna jambo linaendelea nyuma ya pazia inahitaji akiri kubwa sana kung'amua.
Mbaya zaidi siku hizi wako bize kutoa utabiri wa ongezeko la maambukizi badala ya kutoa utabiri wa dawa ya Korona.

WHO imegeuka nabii wa kutabiri ongezeko la Corona
 
Ahhh tangu huu ugonjwa ulipoanza kutangazwa .... Baadhi tulishajua tu kuwa hii ni issue ya vita ya kiuchumi hakuna lolote hapo yanayo endelea mengine yote ni janja janja tu na kuwa brainwashed watu

You know what ? mahala ambapo dunia imefikia sasa nchi nyingi zinamiliki silaha za kinyuklia so nivigum kushuhudia baina ya nchi ambazo ni super power zikipigana vita wanaogopa kuwa vita ya nuclear boom Haito muacha mtu yeyeto salama ....so kama patakuwa hakuna mtu atakae baki so it means vita hiyo haitokuwa na maana ..... So vita ambayo inategemewa kwa kiasi kikubwa kwa sasa baina ya mataifa yenye nguvu ni hizi biological weapons
 
Mbaya zaidi siku hizi wako bize kutoa utabiri wa ongezeko la maambukizi badala ya kutoa utabiri wa dawa ya Korona.

WHO imegeuka nabii wa kutabiri ongezeko la Corona
Wananikera sana ...hiyo taasisi ilipaswa kufutwa..kama watu bado wanaendelea kufa duniani na mpaka sasa wameshidwa kuja na solution umuhimu wa taasisi yao kuendelea kuwepo ni upi sasa !!!!?.... WHO ni puppets
 
Kila mwaka wa uchaguzi kuna viwavi jeshi vinaajiriwa kwa ajili ya propaganda za mitandaoni kutetea vyama vyao, aisee.
Kwa hiyo wewe unaridhika na namna WHO wanavyoshughulika na hili janga la Corona kwa kuhimiza utoaji wa takwimu badala ya tiba?

Jana kwenye dira ya dunia BBC Swahili Salim Kikeke alimuuliza swali zuri sana mtu wa WHO ambaye ameshiriki kufanya tafiti ya namna Afrika maambukizi yatakavyoongezeka kwa mwaka huu wa kwanza

Japo utafiti wao unaonesha Afrika haitaathirika sana, ila alishindwa kujibu "kwanini mara zote tafiti zinazofanywa kuhusu ongezeko la maambukizi linailenga Afrika tu?

Baada ya kutoka nje ya swali ikabidi Kikeke amrudishe tena kwa kumuuliza kwamba haoni kama tafiti zao WHO zinaionea zaidi Afrika?

Kwa kujing'ata ng'ata aliishia kusema wanataka Afrika ijiandae.

Badala ya kukesha na tafiti za tiba wao wako bize na tafiti za kuongezeka kwa Ugonjwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
WHO wapo kwenye pay roll ya Bill Gates foundation, jamaa huyu na mkewe wamekwisha teka nyara WHO lengo lao ni kutaka kulazumisha chanjo yao ipewe kipa umbele na kuhakikisha makampuni mengine yana hujumiwa na WHO wanapo gunduwa dawa ya kuponya au chanjo mfano:Madascar (dawa) na Italy (Chanjo) hivyo hawa visemi wako busy kuzungunzia nafawa na chanjo kutoka makampuni ya madawa ya huko America pamoja na chanjo za Bill Gates, basi.

WHO inasahau kwamba ujasiri na umakini wa wanasayansi wa Kitaliano ndio waliweza kwa mara ya kwanza kusema kwa usahihi kabisa jinsi Corona inavyo wamaliza watu baada ya kuzifanyia postmortem zaidi ya maiti hamsini wakagunduwa kwamba kinacho uwa watu ni damu kuganda kwenye mishipa - hii inamaanisha mwanzo wana sayansi walikuwa wana misdiognise tatizo, bahati nzuri Italy imekwisha gunduwa chanjo ilifanya juhudi kubwa kutoka na wananchi wao kufa kwa wingi kutokana na ugonjwa wa Corona - cha ajabu WHO haizungumzii sana chanjo ya kutoka Italy - ingekuwa ni USA au UK ingepewa publicity kwenye home page ya WHO.
 
Wananikera sana ...hiyo taasisi ilipaswa kufutwa..kama watu bado wanaendelea kufa duniani na mpaka sasa wameshidwa kuja na solution umuhimu wa taasisi yao kuendelea kuwepo ni upi sasa !!!!?.... WHO ni puppets
Aiseee kama umeandikiwa hii comment ni sawa ila kama umeandika wewe nenda kwenye kioo kajitazame halafu ujitathimini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
WHO wapo kwenye pay roll ya Bill Gates foundation, jamaa huyu na mkewe wamekwisha teka nyara WHO lengo lao ni kutaka kulazumisha chanjo yao ipewe kipa umbele na kuhakikisha makampuni mengine yana hujumiwa na WHO wanapo gunduwa dawa ya kuponya au chanjo mfano:Madascar (dawa) na Italy (Chanjo) hivyo hawa visemi wako busy kuzungunzia nafawa na chanjo kutoka makampuni ya madawa ya huko America pamoja na chanjo za Bill Gates, basi.

WHO inasahau kwamba ujasiri na umakini wa wanasayansi wa Kitaliano ndio waliweza kwa mara ya kwanza kusema kwa usahihi kabisa jinsi Corona inavyo wamaliza watu baada ya kuzifanyia postmortem zaidi ya maiti hamsini wakagunduwa kwamba kinacho uwa watu ni damu kuganda kwenye mishipa - hii inamaanisha mwanzo wana sayansi walikuwa wana misdiognise tatizo, bahati nzuri Italy imekwisha gunduwa chanjo ilifanya juhudi kubwa kutoka na wananchi wao kufa kwa wingi kutokana na ugonjwa wa Corona - cha ajabu WHO haizungumzii sana chanjo ya kutoka Italy - ingekuwa ni USA au UK ingepewa publicity kwenye home page ya WHO.
Huu ndo upuuzi wa haya mashirika ya kimataifa. Na siku hizi Italy haisikiki kabisa hata kwenye media zao wakati kipindi kile watu wanakufa headlines zote zilianza kwa kutaja jina la Italy, lakini leo habari inaanza na kuisha husikii neno Italy

Kiuhalisia kama Italy siku hizi hakuna vifo ilibidi iendelee kubaki kwenye headlines kuelezea ni namna gani imeweza kuepukana na vifo
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili suala linanipa ukakasi kwa nini takwimu na kwanini malumbano ya mataifa mawili tu China na Marekani?

Nafikiri kuna jambo linaendelea nyuma ya pazia inahitaji akiri kubwa sana kung'amua.
Hii kitu ina siasa nyingi kuliko uhalisia. Njia zote zinazopendekezwa na WHO kujikinga na corona ni za kihuni na zimekusudia kupunguza kinga ya mwili ili tufe wengi, aayeelewa na aelewe, tusiamini kila jambo ni muhimu kujisomea ili kujua ukweli.
 
Kwa hiyo wewe unaridhika na namna WHO wanavyoshughulika na hili janga la Corona kwa kuhimiza utoaji wa takwimu badala ya tiba?

Jana kwenye dira ya dunia BBC Swahili Salim Kikeke alimuuliza swali zuri sana mtu wa WHO ambaye ameshiriki kufanya tafiti ya namna Afrika maambukizi yatakavyoongezeka kwa mwaka huu wa kwanza

Japo utafiti wao unaonesha Afrika haitaathirika sana, ila alishindwa kujibu "kwanini mara zote tafiti zinazofanywa kuhusu ongezeko la maambukizi linailenga Afrika tu?

Baada ya kutoka nje ya swali ikabidi Kikeke amrudishe tena kwa kumuuliza kwamba haoni kama tafiti zao WHO zinaionea zaidi Afrika?

Kwa kujing'ata ng'ata aliishia kusema wanataka Afrika ijiandae.

Badala ya kukesha na tafiti za tiba wao wako bize na tafiti za kuongezeka kwa Ugonjwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu usiende mbali, sisi wenyewe tumegundua nyungu na kuondoa hofu kuwa ni dawa ya corona. Mbona hawatuulizi tumefanikiwaje kuiteka corona? Wamekalia vitisho... Sasa hatutishiki hapa kazi tuu..
 
Back
Top Bottom