#COVID19 WHO yaonya kuhodhiwa kwa chanjo kutoka na aina mpya ya kirusi cha Omicron

#COVID19 WHO yaonya kuhodhiwa kwa chanjo kutoka na aina mpya ya kirusi cha Omicron

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Shirika la afya duniani WHO, leo limeelezea wasiwasi kwamba mataifa tajiri yanayotishiwa na kuzuka kwa aina mpya ya kirusi cha Omicron huenda yakahodhi chanjo za ugonjwa wa COVID-19 na kutatiza usambazaji wa chanjo hizo kote duniani hali itakayotatiza juhudi za kukabiliana na janga hilo.

Mkuu wa idara ya chanjo na biolojia wa shirika hilo la WHO Daktari Kate O'Brien, amesema namna ya pekee ya kukabiliana na ugonjwa huo ni kwa kila mtu hasa katika maeneo yanayokabiliwa na hatari zaidi za maambukizo kuchomwa chanjo.

O'Brien ameongeza kuwa inaonekana kuwa lengo hilo limepuuzwa. Baada ya mkutano na wataalamu wake, shirika hilo lilisisitiza ushauri wake kwa mataifa dhidi ya matumizi makubwa ya chanjo za nyongeza kwa raia wake ili mataifa yenye chanjo zaidi badala yake yaweze kupeleka chanjo hizo kwa mataifa maskini ambayo yana nakisi kubwa ya chanjo hizo.

DW
 
Hayo mataifa si wanasema wamesha chanja zaidi ya 78%? Sasa wanahodhi ili iweje...
 
Sisi tunapiga nyungu, hata michanjo yao wanadungwa wazembe wachache. Wahodhi tuu sisi hatuyahitaji
 
Back
Top Bottom