beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Shirika la afya ulimwenguni WHO limepata kibali cha kusambaza vifaa vya matibabu katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia, ikiwa ni mara ya kwanza ndani ya miezi sita, lakini uhaba wa mafuta bado unakwamisha zoezi hilo.
Mkurugenzi wa shirika hilo, Tedros Adhanom Ghebreyesus ameeleza kwamba usambazaji wa misaada iliyoruhusiwa ni sehemu ndogo ya kile kinachohitajika. Usambazaji huo unajumuisha vifaa muhimu vya matibabu, ikiwemo vifaa vya kujikinga, dawa za malaria na kisukari, matibabu ya utapiamlo na madawa na vifaa kwa ajili ya afya ya uzazi.
Serikali ya Ethiopia ilizuia karibu usambazaji wote wa misaada ya kiutu na kimatibabu mjini Tigray mnamo mwezi Juni kufuatia miezi kadhaa ya mvutano wa kisiasa baina ya serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed na viongozi wa jimbo la Tigray
Source: DW Swahili