WHO yarekodi maambukizi zaidi ya 250,000 ya COVID-19 ndani ya saa 24 zilizopita

WHO yarekodi maambukizi zaidi ya 250,000 ya COVID-19 ndani ya saa 24 zilizopita

Mkuu ugonjwa huu hauko Tanzania peke yake.

Ugonjwa huu hauna uhusiano wowote na Tanzania kama nchi au Magufuli kama rais wala mtu.

Kujaribu kuuhusisha ugonjwa huu na Tanzania kama nchi au Magufuli kama rais au kama mtu, kwa hakika ni kushindwa kujitendea haki wewe mwenyewe na hao wote unaowahusisha nao. Yaani watu na nchi.
Mara ngapi mnamtaja Magufuli katika hili suala la corona kwa kuona anawatoa sadaka watanzania kawaambia corona hakuna/imepungua na ndio mnasema sababu ya wananchi kuacha kuchukua tahadhari za kujikinga na corona.
 
Ajabu ni kuwa kuna mijamaa ikiona habari kama hizi inakasirika kweli kweli na inaweza hata kupigana ngumi.

Jambo la kushangaza, wengine wanaposikitika wengine wana kasirika?!

Ikumbukwe kuna tofauti za wazi baina ya kusikitika na kukasirika kama ilivyo kwa kusikitika na kufurahi.

Ama kweli stajaabu ya kustajaabu lakini ya Firauni ni baba lao!
Nani akasirike kuna magonjwa yanaua kuliko Corona,Malaria ndio inaongoza kuua Africa lkn bado maisha yanaendelea kama kawaida cha msingi kuchukua taadhari kama tunazo zichukua kwenye Malaria.
 
Ili wapate nini nyinyi au sisi tukihofu?

Marekani, China, Russia, UK nk wote wamehimiza raia wao kuondoka.

Si nchi jirani hakuna anaye tu envy. Hivi huyo anayetuvalia hasira kwenye yasiyokuwa enviable ni nani?

Angalau mifano tahadhari.
Waache waondoke,kuna wataliano kila siku wanaingia Zanzibar hapo ndio utajua kila serikali na mipango yake kwa raia wake.
 
Basi kwa sababu umesema mwenyewe kuwa hujui, nichukue fursa hii tena kukufananisha kuwa ipo tofauti ya wazi baina ya kusikitika na kukasirika. Vile vile kati ya kusikitika na kufurahi.

Fahamuni kuwa habari zozote mbaya kuhusiana na ugonjwa huu zinasikitisha mno na ndiyo maana tunaandika kila taarifa zenye mafunzo zinapopatikana.

Kukasirika huambatana na matusi na kejeli. Angalia mabandiko yenye matusi na kejeli kuwatambua nani wenye hasira na mabandiko na ugonjwa huu kujiuliza ni kwa maslahi yapi?
Habari zinazo sikitisha ni za Corona tu,ila za Malaria zinazoua watu wengi zinafurahisha ndio maana huandiki habari zake?
 
Ili wapate nini nyinyi au sisi tukihofu?

Marekani, China, Russia, UK nk wote wamehimiza raia wao kuondoka.

Si nchi jirani hakuna anaye tu envy. Hivi huyo anayetuvalia hasira kwenye yasiyokuwa enviable ni nani?

Angalau mifano tahadhari.
Acha kujiabisha, watu wanatoka na kuja huku, wewe unasema wameambiwa watoke. Nina mtoto mbichi hapa katika USA kuja kupata dushee baada ya mwezi anarudi, sasa ninacho kufanya ni kumpitisha kitaa ili ajionee kuwa korona hakuna huku.
 
Nyani kuona *undule ni shida. Acha kujiaibisha wewe.

Hadithi zako hizo na madushe jukwaa lenu umelisahau?

Matamko ya mabalozi walioondoa raia wao hukuwasikia ila tuamini hadithi zako za kitoto namna hii?

Hujihurumii wewe? Unadhani aliyekwambia mtanzania wa leo si wa jana hukuyaona ya mamboleo yaliyokuwa bora mno kuliko haya ya kwako.

Hata hivyo kama unaona una ushahidi mzuri zaidi wapelekee kina Kabudi, Ummy na wote wenye nia ya kuwa prove mabalozi hao wrong.
 
Mara ngapi mnamtaja Magufuli katika hili suala la corona kwa kuona anawatoa sadaka watanzania kawaambia corona hakuna/imepungua na ndio mnasema sababu ya wananchi kuacha kuchukua tahadhari za kujikinga na corona.

Wewe unasema kawaambia watu Corona imepungua?

Pia unasema kawaambia watu Corona imekwisha?

Bado hujui sababu ya watu kuacha kuchukua tahadhari?

Zikitajwa sababu za watu kutochukua tahadhari inakuwa issue?

Bado mnaona mko sawa?

Mtanzania wa leo mbona siyo yule wa jana?
 
Wewe unasema kawaambia watu Corona I?

Pia unasema kawaambia watu Corona imekwisha?

Bado hujui sababu ya watu walioacha kuchukua tahadhari?

Zikitajwa sababu za watu kutochukua tahadhari inakuwa issue?

Bado mnaona mko sawa?

Mtanzania wa leo mbona siyo yule wa jana?
Kwa ufupi mkuu huu ndio uhalisia wa corona kama unavyoona,watu hawachukui tahadhali na hali ndio hii wengine wanaita ni bahati.
Na tatizo sio Magufuli maana kiukweli toka mwanzo wenyewe wananchi hatukuwa tukichukua tahadhari ipasavyo tulikuwa na hofu tu kuliko hiyo hali ya corona yenyewe ilivyo alichofanya Magufuli ni kuondoa tu hofu.
 
"Tuko salama" by Magufuli

"Corona ilimalizwa. Iko mbali kule. Tuko salama. Kwani sisi hatuogopi kufa?" Jambo la kheri mno.

Bado humjui aliyesitisha harakati zozote za tahadhari.
 
"Corona ilimalizwa. Iko mbali kule. Tuko salama. Kwani sisi hatuogopi kufa?" Jambo la kheri mno.

Bado humjui aliyesitisha harakati zozote za tahadhari.
Ndio anakuuliza kwani wao hawaogopi kufa?
Kwa maana kama Magufuli angekuwa anasema hakuna corona halafu kumbe anajua ukweli ni kwamba ipo na inauwa basi angevaa barakoa pale ila anachokisema ndio anachoamini na ndio maana hata yeye na wale wengine wote pale hakuna aliyevaa barakoa.

Hali ya corona ingekuwa tete huyo Magufuli asingekuwa anasema hakuna corona au imepungua wakati uhalisia watu wanakufa na corona,tulikuwa tunaishi kwa hofu wakati kumbe huu ndio uhalisia wa corona.
 
Back
Top Bottom