Besta Mlagila
Senior Member
- May 29, 2018
- 101
- 191
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetabiri kuwa idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona barani Afrika haitakuwa kubwa kama ilivyokadiriwa na kilele chake pia kitachelewa kufika katika nchi nyingi za bara hilo kutokana na hatua madhubuti zilizochukuliwa kuzuia kuenea kwa virusi hivyo.
Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika Bibi Matshidiso Moeti amesema utabiri uliotolewa na WHO ulionesha kuwa idadi ya wagonjwa wa virusi vya Corona barani Afrika itafikia kilele chake wiki tano baada ya mgonjwa wa kwanza kugunduliwa katika nchi moja ya Afrika na kwa wastani, asilimia 26 wa watu wote wa Afrika wangeweza kuambukizwa virusi hivyo.
Ameongeza kuwa utabiri huo ulifanywa katika msingi wa maambukizi kati ya watu na watu haswa katika maeneo ya vijijini, lakini hatua zinazochukuliwa na serikali za nchi za Afrika kama vile zuio nusu, umbali wa kijamii na kunawa mikono zimepunguza maambukizi ya virusi.
Ameongeza kuwa WHO inashirikiana na Tanzania, ambayo haijatangaza takwimu ya idadi ya wagonjwa tangu Aprili 29, kufanya hivyo ili kuandaa mpango mwafaka wa kukabiliana na virusi vya Corona.