#COVID19 WHO yasema ukosefu wa chanjo Afrika unaweza kuirudisha nyuma dunia

#COVID19 WHO yasema ukosefu wa chanjo Afrika unaweza kuirudisha nyuma dunia

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema Afrika inakabiliwa na upungufu wa dozi milioni 470 za chanjo ya COVID-19 mwaka huu, baada ya mpango wa kimataifa wa COVAX kupunguza makisio ya shehena yake, na kuibua wasiwasi wa aina mpya na hatari za kirusi hicho.

Kitengo cha WHO barani humo kilisema katika mkutano wa kila wiki mjini Brazaville hapo jana, kwamba ni asilimia 17 tu ya wakaazi wa Bara hilo ndiyo watakuwa wamechanjwa kufikia mwishoni mwa mwaka huu, ikilinganishwa na shabaha ya asilimia 40 iliyowekwa na WHO.

Mkurugenzi wa WHO Afrika, Matshidiso Moeti, alisema ukosefu wa usawa na upatikanaji hafifu wa chanjo vinatishia kuyageuza maeneo Barani Afrika, kuwa maeneo ya kuzalisha virusi visivyosikia chanjo.

Kutokana na uhaba wa kimataifa, mpango wa COVAX utasafirisha karibu pungufu ya dozi milioni 150 kuliko ilivyopangwa.

Upunguzaji huu wa malengo ya chanjo unakuja wakati Afrika imevuka mambukizo milioni nane wiki hii, imesema WHO.
 
Watu bado wamegawanyika,walio chanja na waosiotaka chanjo,kaazi kweli kweli...
 
Tangu kuingia kwa huu ugonjwa hofu kubwa imekuwa ikielekezwa afrika.
 
Back
Top Bottom