Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,540
Kishoka acha longolongo, hivi unajua maana ya 'progressive' wewe maana naona unaendeleza 'reactionary' politics na hiyo PPP yako!
Companero,
Kwani kuwa na reactionary politics ni makosa? Je kinachosababisa Upinzani au guerilla movement ni nini?
Sasa kwa kuwa hukupenda kwenda kusoma kuhusu PPPT, nitakurahisishia uone premise ya PPPT ambayo inazungumzia kuwepo kwa mfumo sahihi wa haki na utu katika kufuata kanuni, sheria na Katiba.
Rev. Kishoka
![]()
Rev. Kishoka has no status. Edit
JF Premium Member
Join Date: Mon Mar 2006![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
Location: USA
Posts: 3,323
Thanks: 621
Thanked 426 Times in 171 Posts
Rep Power: 131![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
Re: Progressive People's Party of Tanzania![]()
Katika mfumo bora wa kiutawala, Sheria lazima zifuatwe na Wananchi na wanaotunga Sheria na dhamana ya kutunga Sheria ni lazima wafanye kazi kwa kutimiza wajibu na majukumu yao.
Quote:
Chama hiki kipya kitafanya nini kushughulikia tatizo la ufisadi:
a. Benki Kuu
b. Serikalini (wizarani)
c. Wahusika wa ufisadi
Kilichotokea Tanzania ni kuvunjwa kwa Sheria na Wananchi wake na kukosekana kwa kuwajibika kwa waliopewa dhamana ya kulinda na kuhakikisha kuwa Sheria na Kanuni zinafuatwa.
PPPT katika safari yake ya kujenga Taifa, itahakikisha kuwa Sheria, Kanuni na Katiba ndio dira za nchi na si utashi wa mtu mmoja mmoja au vikundi maalum.
Hivyo, kabla ya kuanza kushughulikia ipaswavyo yaliyopita ya kuhujumu nchi, kazi ya kwanza itakuwa ni kuhakikisha kuwa Sheria, Kanuni na Katiba zinafanya kazi kwa haki na zinavyopaswa, bila kuteterekea kutokana na msukumo wa kisiasa, hujuma au namna yoyote ile ambayo lengo ni kutafuta mianya ya kukiuka Sheria, Kanuni na Katiba.
Kisha kwa ridhaa na dhamana ambayo PPPT imepewa, PPPT itafuatilia kwa kutumia kitana kila kitu kinachogusa uchumi wa Tanzania kuwa kuangalia mapengo na matatizo yaliyotokea na kuhakikisha hatua madhubuti zinachukuliwa kuziba mianya ya kuhujumu nchi na hatua kali za kisheria na kikatiba zitachukuliwa dhidi ya yeyote yule ambaye amevunja sheria, kanuni na kukiuka Katiba.
Hivyo kwa mifano hiyo mitatu, naamini kuwepo kwa mfumo bora na uongozi imara, PPPT itaweza kutatua matatizo ya kale na yajayo kwa kuyafanyia kazi na kutoa maamuzi ya haki kwa kutumia Sheria, kanuni na muongozo wa Kikatiba.
