Kwa waswahili wenzangu
Sehemu ngumu zaidi katika kuachana kwetuni kukiachilia kipande cha mwisho cha moyo wangu. Sehemu ya kuhuzunisha zaidi si kuwa hatuongei na kupendana tena, ni kuwa hatuongei na kupendana kama zamani. Usiwe na huzuni kisa yamekwisha, kuwa na furaha kwa sababu yaliwahi kuwa yako na yenye kuvutia.
Tutazame sisi kama kioo kilichovunjika, kwa sisi kuachana ni bora kukiacha (kioo) kikiwa kimevunjika kuliko kujiumiza wenyewe kwa kujaribu kukirekebisha. Natamani ningeweza kuyakusanya machozi yote uliyonisababishia nikalia kwa miaka michache iliyopita tangu tumekuwa pamoja, ili niweze kuzama ndani yake. Moyo wangu unauma sana, lakini utapona, kovu ninalolihisi ndani ya moyo wangu daima litabaki kuwa kumbukumbu yetu.
Unasema hukuacha kunipenda, ila uliacha kuuonyesha (upendo). Ulibadilisha maisha yangu, Nilikupenda kuliko yeyote, na niliamini kwa kipindi kirefu kuwa nawe ulinipenda kuliko yeyote. Nataka usonge mbele. Na utakapokutana na yeyote yule, kumbuka hili mpenzi, majani si ya kijani katika upande mwingine kama utasahau kuyamwagilia majani hayo pia.
Nakupenda, huo ndiyo mwisho wa simulizi yetu, usifunge kitabu chako katika mapenzi, ni wakati wa kubadili ukurasa. Sijui kipi kinaumiza zaidi, kuendelea kujua kwamba bado nakupenda na nitaendelea kukupenda kuliko mwengine yeyote na kukukumbuka sana, au kujua kuwa hauwezi kunipenda kama zamani na utakutana na mwingine mpya. Nilifikiri sana jana usiku. Na nimekuja na hii, ni heri niingie kaburini nikiwa nakupenda, kuliko kuishi kila siku bila kulihisi penzi lako.
My take: Mapenzi yanaua sana.