Rugemeleza:
Kufikia mwishoni mwa 60 na mwanzoni mwa 70 wakati vita vya Biafra, tayari uzalishaji wa mafuta ulikuwa ni zaidi ya mapipa milioni 2 kwa siku. Na bei ya pipa moja ilikuwa kati ya dola 2.5 na 3.0 kwa wakati huo. Hivyo kwa kipindi cha miaka hiyo, sekta hii pekee yake iliweza kuleta Gross ya zaidi $2Bilion kwa mwaka. Hicho ni zaidi ya mapato ya dhahabu yanayopatikana Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Niliuliza swali hilo makusudi. Huko sahihi kabisa kuhusu bei ya mafuta ya wakati huo kitu ambacho kinaonyesha wazi kabisa kuwa bei ilikuwa ni ya chini sana na kwa wakati ule kampuni zifuatazo ndizo zilikuwa zinatawala uchimbaji wa mafuta huko Nigeria Shell-BP, IVIobil, Tenneco, Texaco, Gulf (sasa Chevron), Safrap (sasa Elf), Agip, Philip na Esso. Nyingine ni Japan Petroleum, Occidental, Deminex, Union Oil, Niger Petroleum and Niger Oil Resources. Kwa Mujibu wa N.K.Obasi katika makala yake "Foreign Participation In The Nigerian Oil and Gas Industry"
Nigeria: Foreign Participation In The Nigerian Oil and Gas Industry - OnlineNigeria.com.
Kuhusu suala la kiwango cha mafuta takwimu unazosema si sahihi uzalishaji wa mafuta nchini Nigeria ulikuwa hivi mapipa 5,000 kwa siku mwaka 1958, 17,000 mwaka 1960 na mapipa 45,000 mwaka 1966. Nigeria ilifikia kiwango cha mapipa 1,000,000 mwaka 1970. Hii ni baada ya vita ya Biafra kwisha. Ukisoma makala ya Obasi utapata maelezo ya kutosha. Ikumbukwe kuwa Nigeria haikupata fedha nyingi kutoka kwenye mafuta kwani kampuni zilikuwa zimepewa vivutio na misamaha mingi. Ilianza kupata fedha nyingi baada ya kujiunga na OPEC mwaka 1971 na kwa kweli mara baada ya Mgogoro wa Mafuta wa mwaka 1973-4 ambapo OPEC ilipitisha azimio kuwa nchi zote wanachama lazima ndizo zinatunga bei ya mafuta na serikali zao lazima zifaidi. Kwa hiyo chanzo cha mgogoro wa Biafra hakikuwa suala la mafuta bali madhira mengi ambayo watu wa huko waliona wanapata katika nchi yao na sana sana baada ya mapinduzi ya mwaka 1966 ambayo yalilepelekea Waibo wengi (30,000) kuuawa katika sehemu za kati na kaskazini ya nchi. Vilevile zaidi ya Waibo 1.8 walikimbia maeneo hayo kwenda kwao. Vita ya Biafra ilianza Julai 1967 na kumalizika Januari 1970. Ni rai yangu iliyotulia kuwa Mwalimu hakukubali kufumbia macho mauaji hayo na hakuliona tatizo lile kama la vita vya Wakristu na Waislamu. Ikumbukwe kuwa Yakubu Gowon ambaye ndiye alikuwa Raisi wa Nigeria, wa wakati huo, alikuwa Mkristu na alikuwa anatoka Kaskazini.
Na hata mwaka 1994 mauaji ya Rwanda yalipotokea Mwalimu alimuomba Mwinyi apeleke Majeshi lakini Mwinyi akakataa kwa sababu ya kuwa Tanzania ilikuwa ndio mpatanishi. Kutokana na hilo Mwalimu alimwomba Mwinyi ruhusa ya kuzungumza na Waandishi wa Habari na kueleza msimamo wake. Mtu asiyeelewa anaweza kumtuhumu Mwinyi kuwa hakujali kwa sababu waliokuwa wanachinjana hawakuwa Waislamu. Lakini kwangu mimi nitamtetea Mwinyi kwani hoja yake ya kuwa Mpatanishi hawezi kuingia vitani dhidi ya wale anaowapatanisha ni ya msingi kabisa. Tunaweza tukasema angepeleka majeshi kwa ajili ya kuwalinda Wakimbizi lakini hiyo ni kutokana na mtu kunufaika na mapito ya historia (hindsight) au (20/20).