Ukweli ni kwamba, jinsi knowledge inavozidi kuongezeka watu wanazidi kwenda mbali na Mungu, hii hata kwenye bible imeandikwa though... Mtu anayesoma science kwa undani zaidi, any field of science, ukianza kuingia deep utaanza kuona kama sisi binadamu tunaweza fanya chochote kile...
Nimesoma na watu wa aina mbalimbali wengine walioshika dini kupindukia, siku zilivozidi kwenda tukachukua wote courses chuo physics, psychology, biology, computer science, kadri mambo yanavozidi kueleweka ndo imani ikaanza kuyumba, hadi jamaa aliyekua kashika sana dini alikuja akanambia ameanza ku-question uwepo wa Mungu, yote ni kutokana na ile elimu anayoipata kuhusu dunia na ulimwengu kwa ujumla darasani, unconsciously inaingia akilini inakubadilisha... Honestly hata mimi mwenyewe imani yangu imeyumba mara nyingi kwa ku-question uwepo wa Mungu kutumia science knowledge..
Na muda mwingine mtu unaanza ku-question, kwamba mimi ni Mkristo je ni kwa sababu nimependa mwenyewe au sababu nilizaliwa familia ya wakristo nikakua nikayashika mambo yakaniingia hivohivo?? sababu in reality mtoto mdogo anashika mambo na kuyapokea akilini na yakadumu milele, je ungezaliwa muislamu si leo hii ungetetea uislamu, je ungezaliwa Buddhist si ungeendelea na imani yako maana unconsciously iliingia akilini ulivokua unakua ikakaa... Je ungebadili dini ufate ukristo? ufate uislamu? Sasa je yupi anaamini cha ukweli yupi cha uongo?? pande zote mbili zina mafundisho yao na wana proof zao... Haya maswali yanachanganya at the end of the day mtu mwenye knowledge nyingi kama Mark, watu kama Bill Nye, wanaamua kua atheists tu kwa kuona dini haina logic....