Unajua, wewe huwezi kuelewa kwa sababu hata hicho unachodhani unakielewa, pia hukielewi. Mimi kuhoji juu ya hayo yanayomhusu mungu wenu ni kwa sababu nahitaji ufafanuzi na si kingine, sasa mnapojawa na jazba badala ya kutoa hoja zenye ushahidi, ni jambo lisiloleta faida kwa mjadala huu.
Labda wewe unaeelewa, nitolee ufafanuzi wa hayo aliyoyazungumza ili niweze kuelewa kuwa mungu wenu yupo na hajafa, haumwi, hajasafiri au kuhama.
Uso wa nyoka
Sasa huyo mungu unaemwamini, anajipinga yeye mwenyewe? Au utofauti wa kimafundisho kati ya wale wanaomwamini kuwa ishara ya juhudi za kumtambua na kumfikia yeye, huoni kuwa ni uthibitisho tosha kuwa uwepo wake una walakini pia? Huoni kuwa hata hayo maandishi unayoyaamini yanaweza kuwa sehemu ya juhudi za kibinadamu katika kufikia malengo yao na si maandiko yaliyotoka kwa mungu kama unavyoamini?
Tukija katika swala la maadili, ningependa urudie posti yangu hapo juu unifafanulie jinsi mungu alivyohusika katika kuandika miongozo na maadili katika taaluma.
Ni kanuni gani zinazoongoza katika kumtambua mungu wa kweli na asie wa kweli?
Cureone
Umewahi kusikia kitu kinaitwa Fallacy of definition ?
Tikikosa common ground ya kumdefine Mungu ndicho chanzo kikuu cha mjadala huh.
Uwepo wa Mungu hauna utata ila namna Mungu anabyotafsiriwa na watu mbalimbali kwa kupenda au kutokupenda ndio chanzo cha kukosa hekima na ujuzi.
Hata wewe unaugua ugonjwa huo huo, unameona Mungu katika human behavior na sio kwenye broad picture Kama universe na vijazavyo ndiyo sababu kuelewa kwako ni mbindee
Kwa mfano wa kidunia na tujadili habari za Mungu @ corporate level na sio kwenye petty business ambazo hatuwezi kukubaliana kutolana na am a matatizo ya kuelewa au kukosa Kabisa uwezo wa kutafakari