Huku nyuma nimezungumza na Mkulo anasema kweli wanazo taarifa za kufutwa kwa msaada kutoka Dutch. Kisa chenywe ni mfanya viashara mmoja wa Kidachi aliyekuwa anataka upendeleo kwenye biashara ya magogo akawekewa ngumu. alifika mpaka kwa Pinda akamrudisha kwa Mwangunga ambaye alisisitiza kuwa ni lazima afuate taratibu na ndio akaamua kuwasiliana na ubalozi wao
Kweli mkuu, tuanze kufikiri kufanya mambo yetu bila misaada ya hawa wajomba. Wanaweza kututia mfukoni hii tabia ya kuzunguka nje kila kukicha kuombaombaTumechoka sana na hawa mabwana na hivyo ni bora kubaki tukiwa na akili zetu lakini wewe habari hizi umezitoa wapi??
Kweli mkuu, tuanze kufikiri kufanya mambo yetu bila misaada ya hawa wajomba. Wanaweza kututia mfukoni hii tabia ya kuzunguka nje kila kukicha kuombaomba
Tumechoka sana na hawa mabwana na hivyo ni bora kubaki tukiwa na akili zetu lakini wewe habari hizi umezitoa wapi??
Mkuu hamna msaada usio na conditions. Mtu yoyote anayetoa pesa anataka kuona pesa zinatumika kama ilivyo kusudiwa na si kunufaisha wengine. Misaada doesn't mean unatumia pesa utakavyo. Ni kama scholarship. Ni msaada lakini kuna vigezo unabidi umaintain ili kuendelea kupokea msaada huo.I always ask myself... hivi misaada haitakiwi kuwa bila conditions? Nini maana ya msaada? kutoa back favour?
Netherlands ni wakoloni kabisa kwa fikra. Ikiwa hawawezi kuchuma kiujanjaujanja watakubatiza kwamba 'you are an unreliable'. Mimi natamani kujua details za hiyo kampuni lakini kwa ninavyowajua inawezekana kabisa Tanzania imeshtukia deal lao feki. Rwanda hivi karibuni imeanza kuachana na hiyo misaada taratibu. Kusema ukweli bora tutafutane waafrica tujadiliane jinsi ya kuleta maendeleo, hayawezi kuletwa na waholanzi. Wanaowaita wawekezaji ni makampuni yao yanayosaidiwa na serikali zao, kuja kufanya ukoloni si wa nchi nzima bali wa visehemu sehemu.
Mkuu ukiwa na sentensi general kama za Mugabe utakuwa unakosea. Sasa hivi Tanzania haiwezi kuwa koloni na sina hakika kama Uholanzi ina ambitions za Ukoloni. Tunachotakiwa kufanya ni kutumia akili na busara zetu, na si kuwaita wawekezaji hata wakiwa ni wawekezaji uchwara, wakoloni. Tuangalie ni namna gani tunanufaika, ni namna gani tunavuna kutokana na ushirikiano wetu. Westerners huwa wanasema THERE IS NO FREE LUNCH, sasa usitegemee kuwa m-dutch atatoa pesa zake halafu yeye asinufaike.
Inawezekana kuna mtu aliomba mlungula akanyimwa, inawezekana jamaa alitaka kurahisisha mambo halafu akagonga mwamba. Yote yanawezekana. Lakini sidhani kama ni sahihi kuwa na Mugabe mentality, kuwa wawekezaji ni wakaloni. Kama ndio hivyo tufukuze wote tubaki wenyewe.
Mkuu I think he is talking about neo-colonialism na siyo classic colonialism.
Mkuu mbona huu upo tayari. Sasa hivi hatuwezi kusema kuwa hatupo under neo colonialism. Si waholanzi tu, nadhani Kenya ndio ina practice vizuri sana neo colonialism hapa Tanzania kuliko hata Uholanzi, lakini hailalamikiwi unaweza kuona element fulani ya ubaguzi.
Hiyo misaada yenyewe haiwafikii walengwa inaishia kwenye matumbo ya wachache na kuishia kufanyia mambo ambayo hayamsaidii raia wa chini.
Labda wakitunyima tutajifunza kutumia rasilimali zetu kugenerate mapato.
Kama Kenya iliweza kudunda bila misaada kwa muda mrefu sioni kwa nini sisi tushindwe.