Wakati ndugu zetu wanauliwa na kemikali zitokanazo na ujasiriamali wao hatusikii kelele. Tunapoporwa hazina yetu kupitia makampuni hewa kama Meremeta sauti zao hazisikiki. Ndugu yao mmoja apatapo madhara kidogo kulinganisha na madhara wanayotusababishia, tunatishiwa kufutiwa misaada. Pengine kwa kuondoa misaada yao hiyo tutakachopungukiwa ni vumbi tunalotimuliwa na magari tusiyoyahitaji yanayonunuliwa kwa misaada yao hiyo. Na waende na misaada yao!