eliakeem
JF-Expert Member
- May 29, 2009
- 17,214
- 15,853
Hasira za nini anko? Sio mimi nilikuhadaa kwamba sijui Putin amewajibu Wakenya. 😄 Waliotengeneza hiyo 'meme', walikuwa wananuia kuwaingiza box vinyangarika kama wewe. Ambao hawajui kufanya vitu viwili vitatu simpo sana. Vya kuwasaida kudhibitisha kama habari ambazo wameziona mitandaoni ni za kweli au ni FAKE NEWS.
Jombaa, hadi nakuonea wivu. Kama huwa unamiini kila jambo, ambalo unaliona mitandaoni virahisi hivyo. Mawazo ndani ya kichwa chako yatakuwa ni kama filamu moja kali sana. Ambayo ina action, drama, sci-fi, kila kitu hadi na horror, tena zote kwa mpigo. 😆
Umeongea kwa hisia kali sana, lkn bado hujathibitisha kwamba ile ni Fake News.