Why is Safaricom and IEBC refusing to release this data?

Heshima sana Tiba Mimi naamini CORD wanazo copies za form 34,35 & 36 ambazo mawakala wao kwa vyovyote watakuwa wameshawapatia.Ninaamini pia wanataka copies za IEBC ambazo zitaonyesha utafauti na zile mawakala wa CORD hapo ndipo kesi itanoga.IEBC wanajua zipo tofauti ndiyo maana hawataki kuwapatia CORD hizo forms ambazo si classfied documents.

Mkuu ukwelikitugani endelea kutujuza kila kinachoendelea.Ningependa pia kupata maoni ya Ab-Titchaz katika hili sakata.



 
Last edited by a moderator:
Dr. Job yaani CORD wanatia aibu. Kama mwelekeo ndiyo huu wa kudai taarifa basi hawana lolote ila ubabaishaji mtupu na hiyo Kshs 5millions zimepotea bure.

jukumu la kuthibitisha madai ya ukiukwaji wa sheria ya uchaguzi ni ya mdai/mtuhumu...................na mpaka sasa mdai hana taarifa au ushahidi kuwa IEBC ilikiuka chochote na kwa hivyo kesi hii itatupwa tena kwa gharama zake.

Kinachonishangaza ni kwanini CORD hawajitokezi wenyewe moja kwa moja? Ni kwa sababu wanajua hawana ushahidi wowote ule na ndiyo maana wanajificha kwenye mgongo wa huyu mbabaishaji anayedai taarifa ambazo hastahili kupewa chini ya sheria ya uchaguzi wa Kenya.

kama kila mpiga kura atadai apewe hizo taarifa, huo mzigo wa gharama utabebwa na nani? Na ukizingatia hajui kama kuna ukiukwaji wa sheria ya uchaguzi kwa hiyo madai yake ni ya kuhisia tu.................mahakama ya kileleni kama zilivyo mahakama nyinginezo haina mamlaka ya kutoa maamuzi kwenye kesi za hisia kama hii. Lazima mdai atoe ushahidi siyo kudai ushahidi kutoka vyombo ambavyo haviwajibiki kwake kama mpigakura. Taarifa zote anaziomba za nakala za fomu za uchaguzi tajwa, CORD anazo sasa kwanini asiwasiliane nao kwenye hilo?

uhuru na Ruto wauchape usingizi hakuna kesi hapo. Kamwe, Uhuru na Ruto hawawezi kunyang'anywa haki ya ushindi bila ya kupewa nafasi ya kujitetea na kutohusishwa na hii kesi ni dhahiri kesi hii haina ubavu wa kuwavua uraisi na Umakamu haki ambazo ni za kikatiba...........

kesi zote za uchaguzi, AG ndiye mshitakiwa namba moja sasa kama ingelikuwa ni kesi ya kutengua matokeo ya uchaguzi alipaswa awe mshtakiwa namba moja, IEBC wa pili, Jubille wa tatu, Uhuru wa nne, Ruto watano na Safaricom wa sita..............................bila ya kuwashitaki wote hawa hakuna kutengua ushindi.........................na siku zinazidi kuyoyoma. Wamebakiza siku tatu kwani mahakama ziko wazi siku zote na hakuna cha wikiendi.
 
Mkuu Rutashubanyuma hivi hizo forms 34,35 & 36 ni classfied docs.

Ngongo siyo classified ila hakuna kwenye sheria ya uchaguzi ambako mpigakura anayo haki ya kuzidai. CORD ndiyo wanazo na vyama vinginevyo vilivyoshiriki pia wanazo.

Unapokwenda mahakamani siyop ktuafuta ushahidi ila ushahidi unapaswa uwe nao mwenyewe. Jukumu la kuthibitisha madai ya dhuluma ni ya yule anayelalamika. Hadi sasa mlalamikaji hajaanza hata kuonyesha ni kwa vipi anaona kadhulumiwa.......................mahakama itatupa haya madai. tena kwa gharama ya hiyo deposit ambayo ni karibu Tshs 100 millions.............
 
Tiba,

hio ni mali ya uma na IEBC hawawezi kukataa kuitoa...hata kama ni private citizen anaulizia copy.
Nguvu ya katiba Mpya ya Kenya.

Pili, wanataka hizo copy za form kutoka IEBC ndo waeze kuonyesha tofauti iliopo kati ya hizo na za
kwao.

Its that simple but hawa IEBC wanamambo yakizamani kana kwamba bado ni serikali ya Moi.
 
Last edited by a moderator:

Sina la ziada maana umesema yote.

Inapaswa kukumbukwa kwamba Uhuru alipita ile mark ya 50%+1 kwa kura 4,000 pekee na kwa usawa huo ni
rahisi kupata idadi hio ya kura zilizochakachuliwa and force a run-off. This thing is on a very slippery slope.

Ninachoomba ni hao majaji wasikubali kulipwa hela ya hongo maana mtoto wa Kenyatta ana-fweza ya kutisha!
 

Dr. Job Yaani raila kweli ni bomu kabisa...................kila chama cha siasa kilichoshiriki uchaguzi kilizijaza na kuzisaini hizo fomu....labda kwa kuanzia watueleze zile zao wamezitupa wapi?

Pili kesi ya kutengua uchaguzi lazima iwashirikishe A.G, Jubilee, Uhuru, Ruto na kwa kutokufanya hivyo hii siyo kesi ya kutengua uchaguzi wa uraisi kama masharti yake yalivyobainishwa na sheria ya uchaguzi wa kenya.

haki walizopewa Uhru na Rutto ni za kikatiba huwezi kuwanyang'anya bila ya kuwashitaki nao..............huu ndiyo ubabaishaji wa raila..................
 

sheria ipi inakuongoza kusema haya? Hakuna kifunbgu chochote kwenye sheria ambacho chama cha siasa au mtu binafsi anayohaki ya kudai fomu tajwa kutoka IEBC ila anaweza kuruhusiwa kwenda kuzikagua tu jambo ambalo CORD walifanya na kuishia
 

Uhuru alipata 50.07% ile 0,07% ni karibu kura zipatazo 24, 000 na wala siyo 4, 000 kama ulivyodai. Mengineyo ni hisia tu ambazo hazina mashiko..............
 
Leo umepepesa kweli rafiki Rutashubanyuma.
Hadi sasa petition ya kutengua matokeo ya uchaguzi haijawekwa wazi. Unachoongelea ni ile ilowasilishwa leo mbele ya Mahakama kuu ya kutaka Court order ya kuwaamuru IEBC na Safaricom kuachia uzandiki wao wa kuzuia access ya nyaraka hizo.
Pia CORD ina wanasheria smart kuliko upeo wako unavyodhani. Mutula Kilonzo ni moto wa kuotea mbali, James Orengo, Former AG Amos Wako, Ababu Namwamba, Oraro,..wote hao ni senior and most respected Learned Counsels in Kenya legal firms,
Subiria moto wake pale Supreme court..
 
Last edited by a moderator:
My two cents is that cord wants to try this in the court of public opinion, what they are asking for is what they should be furnished with when the case is ongoing not to help them build a case from scratch, they say they have tons of evidence why dont they start their submissions with that?
 

Mkuu Ruta:
Hivi AG,Uhuru na Ruto wao wanahusika vipi,CORD wanaituhumu IEBC kwa kutokusimamia haki ikizingatiwa kuwa IEBC ni legal entity hebu tujuze.
 

ukwelikitugani take it from me. Tarehe 26 Machi Uhuru Kenyatta atasimikwa raisi na jaji Mkuu kuwa raisi wa nne wa kenya hadi sasa hakuna kesi ya kupinga matokeo ya uraisi ila kudai nyaraka ambazo CORD walizisaini kwenye vituo na wanazo nakala halisi sasa sijui wanashindwaje kuthibitisha madai yao. La pili kama Mutula Kilonzo angelikuwa mwanasheria mzuri kwanini asijiuzulu uwaziri ambao umebakia wiki mbili tu na aende akasimame kizimbani badala ya kujificha nyuma ya kivuli cha mtu mwingine.................

tatu kama wa ushahidi kwa nini wanadai ushaidi mwmingine? Ni kuwa kama ile kesi ya ICC hawana ushahidi walalamikaji na mwishowe ni kutupwa tu........................na muda umebakia siku tatuz na ahata kesi ya msingi bado hawajaifungua kwa sababu hawana hela. Kila mshitakmiwa andai TShs 100m ziwe deposited na Supreme Court na washitakiwa wako sita.......................hivyo kitita cha tshs 600 miilioni kinahitajika.

Nani wakuzitoa na ndiyo maana wanadai kumbukumbu badala ya kufungua shauri rasmi,

nne, khoja zao kuhusiana na matumizi ya provisional results yananithibitishia hawajui hata sheria ya uchaguzi wa Kenya inasema nini..............technology imetajwa kuwa ni kitu ambacho ni "aspirational" and not "binding" kama wao wanavyodai na hili dai litatupwa na kesi kutupwa.....................of interest why not sue A.G, Jubilee, uhuru and Ruto as the stringent requirements of election law demands?
 
Sidhani kama hii ni petition ya CORD. Hii ni moja ya court cases ambazo IEBC ijiandae kushughulika nazo. I do see anything relating to CORD here.
 

Dhuks Na hapo ndipo utapeli wa Raila unafikia ukomo..without creating disorder Raila is useless.........finito.. na siku zinazidi kuyoyoma...........anadai ana timu kubwa lakini kwenye petition hata anaona aibu kuliweka jina la CORD kwanini kwasababu khoja hizi zinapingana na sheria ya uchaguzi kabisa
 
12,330,028*(.07/100) = 8631.0196
12,330,028*(.03/100) = 3699.0084

Hapo kwenye red mkuu sijui 24,000 umepaje?

Namtih58 kinachohitajika ni kura moja tu au? na wewe hiyo 0.03% umeitoa wapi? Asilimia 50.07% ni ya kura alizozipata Uhuru siyo za waliopiga kura wote.....................haya mahesabu mwenzetu umeyafyatulia kutoka wapi?
 
Duuuh, Rutashubanyuma?
This is too low indeed from you Sir!
Mutula Kilonzo uwezo wake na upambanaji wake Hauna mashaka. Amewahi kushinda kesi kubwa kadhaa, nitazining'iniza hapa. Pia Sheria ya kenya inazuia Waziri yeyote kutinga mahakamani,katika kofia yake. Pia CORD walieleza wazi kuwa the Three Ministers (Namwamba, Orengo,and Kilonzo)will be providing Technical support to Oraro, Amos Wako& co, Hivyo nilichokuwa napinga ni kule wewe kusema ati Raila si chochote si lolote...???
Pili, lazima utambue Hii ni do or die, hivyo wanapaswa kujiandaa ili wakishusha mawe pale Supreme Court basi kama noma na iwe noma. Hivyo huwezi kukurupuka na kusema walipaswa wawe wame-file kesi hadi sasa, why? wacha wajiandae vema, kwani Uhuru na wenzi wake mna mchecheto gani? Nyie kuleni bata tu, but behold i tell you, mtaingia kwenye Vitabu vya Historia kwa A two week presidency.. !!
Hiyo habari ya ati wamefulia hawana uwezo wa kutoa 100M Times 6, ni majungu tuu na uzandiki.
Btw, kwanini kuweka ngumu kuaccess info za IEBC hadi uchukuliwe kiboko (court order)??? lol!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…