Marcossy A.M
Member
- Aug 21, 2008
- 61
- 24
Tanzania: kama familia ya mama Pekupeku
Nani aje kuisimamisha nchi yetu katika mzunguuko huu wa matukio na umasikini? Kwa maana bila yavyo, hatutoki ng'oo!
Kwamba ukiitafakari nchi hii, na yale YANAYOTOKEA siku hata siku, utabaini kuwa tuko kwenye mzunguuko wa matukio na matumizi. Ndio, tuko kwenye mzunguuko. Ndio, tuko kwenye matumizi mabaya ya rasilimali.
Kwa mfuatiliaji yeyote makini atabaini kuwa kila uchao watanzania tunalia kilio cha maisha magumu, umasikini, maradhi, ujinga, tiba na kinga mbovu ya afya, ajali za hovyo, kuibiwa na kutapeliwa na mengineyo, yote ikiwa ni mfululizo wa matukio mabovu yanayoonesha kutosonga kwetu kwenye maendeleo. Ni kweli, Tanzania imeendelea kuwa masikini sana. Ni moja kati ya nchi masikini sana duniani. Tena umasikini wetu hauendani na kiasi cha rasilimali tulonazo. Tunazo rasilimali nyingi za kutosha kutuondolea umasikini, lakini bado ni masikini sana wa kutupwa.
Hapo, ndipo swali linakuja: inawezekanaje tuendelee kuwa masikini katikati ya utajiri huu wa rasilimali? Ajabu.
Ukifuatilia kwa makini, matukio, mipango, bajeti na utekelezaji shughuli za maendeleo na huduma za jamii nchini, utabaini kuwa nchi hii inaendeshwa zaidi na matukio, visa, mikasa, vijambo na siasa uchwara. Kila kukicha kunazuka jambo angalau la kuwaweka watu vibarazaji wajadili hilo. Sitaki kuyataja hayo, mnayajua. Walioko mamlakani ndio watuhumiwa wakuu wa kuzua vijimambo hivi......na hata nia zao kufanya hivyo zinaonesha kutia shaka. Mungu anawaona.
Matendo kama hayo yanafanana sana na ile familia ya Mama Pekupeku......ambaye kila uchao hutumia fedha za familia kununua hiki na kile, kwa visingizio na sababu tofauti.
Rwanda wanaringa, Uganda wako njiani, Kenya hao......a Chili a mbali Zambia na Msumbiji. Watoto wa mama Pekupeku wameanza kufunzwa kwa majirani, wanakodowea chakula asubuhi mpaka jioni. Mama Pekupeku analalamika.
Tanzania, visa vitaisha lini, matumizi ya hovyo yataisha lini, lini utasimamia rasilimali zetu tukatekeleza vipaumbele vyetu?
Soma Why is Tanzania poor? By Dr. Albanie Marcossy, PhD
Available at amazon.com
Au Agiza kitabu chako kwa 0712417307 uletewe hapo ulipo kwa Tsh 50,000 tu.