Ndugu zangu kuna corona vidudu aina 3au 4 sasa hivi. Ile aina ya kwanza ilikuwa Na dalili za muda mrefu. Pale ulikuwa ukijisikia homa, kichwa kuuma, mafua chafya, kukosa kusikia harufu , kifua Na koromeo unakimbia mara moja Na kuanza kujifukiza na dawa zingine nk. Hivyo vilikuwa vidudu vya mwanzo tokea China.
Sasa hivi vimezuka vingine kutoka Uingereza, Africa ya kusini ni vibaya zaidi. Havina hizo dalili za muda mrefu. Ukiambukizwa tuu utasikia kifua kinauma kidogo baadae unashindwa kupumua mara unakufa kwa haraka kabisa. Ukiwahiwa hospitali ndio utaambiwa umepata nimonia. Taadhari hapa epukeni misongamano maana hujui aliyeambukizwa.
Mimi binafsi Nina ndugu wamekufa wiki jana Na wiki hii hapo Dar . Na wengine wamenusurika hapo hospitali wameruhusiwa. Ila gonjwa ni kifua Na kushindwa kupumua. Ndugu zangu chukuweni taadhari za kujikinga pamoja Na maombi. Kumbukeni kwamba Mungu anafanya kazi Na wanaadamu. Mungu anafanya sehemu yake Na mwanaadam anafanya sehemu yake. Kwa kushirikiana hivi ndio matokeo yanakuwa chanya. Usilete ubishi Na kukaa tuu unangojea mtu akuambie funga mlango. Wewe funga mlango wako ili Uwe salama. Nawaombea Mungu wote mlioko Tanzania pia najiombea mimi Na wote tulioko USA pia nawaombea watu wote nchi zote ulimwenguni ili Mungu atuondolee hili gonjwa
C&P