Gwajima yaelekea neno la Mungu halijui:-
1) Nabii ni kinywa cha Mungu haongei atakalo kwa hiyo maswali yote ya Gwajima ni kupoteza muda kwani chungu kamwe hakiwezi kujitia kinaujuaji zaidi ya Mfinyanzi. Kama Mungu kaamua kumtumia kuutabiria mfupa mkavu wa Tanzania hivi Gwajima ni nani akhoji kwa nini Nabii Bushiri asitabirie mataifa mengine bali Tanzania? Huko ni kukhoji busara ya Mwenyezi Mungu!
2) Inatosha kusema Gwajima ni mwongo anapodai Lowassa hatakufa. Ukweli ni kuwa sote tutakufa kwa muda ambao Mfinyanzi alitupangia.
3) Gwajima anadai Nabii Bushiri kwanini anatutabiria mambo mabaya tu? Sasa kama mabaya yanakuja kwetu je Gwajima anataka Nabii Bushiri atabiri uongo?
4) Biblia hususan vitabu vya Deuteronomy, Jeremiah na Ezekiel vimeonya manabii wanaotabiri mema huku Mfinyanzi hajawatuma. Gwajima ni taswira ya Nabii wa uongo Hananiah na adhabu yake ya kupingana na Nabii Jeremiah ilikuwa ni mauti. Soma Jeremiah 5:31, 14:14, 23:25 & 28:15-17.