Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
- #26,161
SERIKALI YA CHADEMA KURUHUSU SOKO HURIA KWA WAKULIMA KUUZA MAZAO YAO POPOTE KWA MASLAHI WANAYOYATAKA.
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kitafungua soko huria litakalotoa fursa kwa wakulima kuuza mazao yao popote wanapotaka hata nje ya nchi kwa bei wanayoitaka wenyewe.
Akizungumza na wakazi wa jimbo la Igunga mkoani Tabora leo Ijumaa, Septemba 18, 2020, Mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais, Mheshimiwa Salum Mwalim amewahakikishia wakulima wa Pamba na Choroko wa jimbo hilo kuwa watakuwa huru kuuza mazao yao popote wanapotaka kwa bei yoyote wanayoona inafaa ili wanufaike na kilimo chao.
Mheshimiwa Mwalim amesema kuna ukandamizaji mkubwa unafanywa kwa wakulima kuwapangia mazao yao wakayauze wapi na kwa bei gani bila kuangalia ni kwa namna gani walipata tabu kupata mbegu, pembejeo na kutunza mazao shambani mpaka walipoyavuna.
“Serikali ya Chama Cha Mapinduzi haitaki kuhangaika na wakulima wala kuwawezesha wakati wa kilimo. Wanaibuka wakati wa mavuno na kuwapangia wakulima wapi wakauze mazao yao na kwa bei gani.
“Nendeni mikoa ya kusini kule Lindi na Mtwara muone wakulima wa Korosho walivyopata tabu. Wamevuna Korosho zao lakini wakaanza kupangiwa bei na wapi wakauze. Mwisho serikali ikawaambia kuwa itazinunua Korosho hizo lakini mpaka leo watu hawajalipwa pesa zao,” amesema Mheshimiwa Mwalim.
Mheshimiwa Mwalim amesema Ilani ya Uchaguzi ya Chadema ya mwaka 2020 kipengele cha 8(i) kimeweka wazi kuwa Serikali ya Chadema imedhamiria kuunda vyama vya Ushirika ambavyo vitasimamiwa na kuendeshwa kwa ridhaa ya Wanaushirika wenyewe ili kuwezesha shughuli za kilimo, ufugaji na uvuvi wenye tija kwa wakulima na wafugaji wenyewe.
Mheshimiwa Mgombea nafasi ya Makamu wa Rais leo ameingia mkoa wa Tabora na kufanya mikutano kwenye majimbo ya Igunga, Manonga na Nzega Mjini. Kesho ataendelea na ziara kwenye mkoa huo kwa kufanya mikutano kwenye majimbo ya Sikonge, Uyui na Tabora mjini.
Imetolewa leo Ijumaa, Septemba 18, 2020 na;
Gerva Lyenda,
Katibu wa mgombea Makamu wa Rais,
Uchaguzi Mkuu 2020.
Nzega Mjini, Tabora – Kanda ya Magharibi
Sent from my SM-A715F using JamiiForums mobile app