Why Magufuli administration misses the point on Government splurge

Why Magufuli administration misses the point on Government splurge

Status
Not open for further replies.
MACHO YA ROHONI 23

Katika katika makala ya niliwaletea mstari mmoja ulioonesha namna Musa alivyomtegemea Mungu hata katika mambo ya kawaida kabisa. Lakini ukitaka kuelewa vizuri huyu Musa alikuwa mtu wa aina gani, unahitaji kumsoma katika matukio mbali mbali! Utaelewa kwa nini alifikia hatua hiyo aliyoifikia!

Moja ya habari inayoonesha upekee wa Musa ipo katika Kitabu cha Hesabu 12. Habari hii imebeba mambo mengi. Lakini ili kuyaona tunahitaji macho yanayoona zaidi ya haya tuliyonayo. Naomba uisome sura hiyo.

Sura inaanza kwa kusema, Haruni na Miriamu walimsimanga Musa kwa habari ya mkewe. Hatujui chanzo chake kilikuwa ni nini, lakini kama unaunganisha na yaliyotokea sura ya 11 na yale ya Hesabu 16, unaweza kuona kwamba kuna watu ambao walikuwa wanamwonea Musa wivu kwamba ni yeye tu ambaye anafanya hiki au kile. Kwa sababu ya wivu huo, Haruni na Miriamu wanaonekana kumpandia Musa kichwani, kwa kutafuta udhaifu alionao.

Ikumbukwe kwamba, Miriamu na Haruni walikuwa ni ndugu wa Musa, tena kuzaliwa kabisa! Miriamu alikuwa ndio mkubwa, akafuata Haruni, na hatimaye Musa. Wawili hawa waliotarajiwa kumuunga mkono Musa na kumtia moyo kila ambapo alikutwa na jambo lolote gumu. Hatujui kama walikuwa wamechoka au kwa kuwa Musa alikuwa mdogo kwao, basi waliona huyu hawezi kutusumbua kwa hili wala lile.

Kwa hiyo wanaamua kumsimanga Musa. Maana ya kumsimanga ni kutafuta habari zinazoharibu sifa yake na kuzisema kwa watu wengine, tena wakati mhusika mwenyewe hayupo! Kwa lugha yetu ni tunasema ni umbea! Kama unataka kwa ile lugha ya kwetu tunasema ”vuhési.” Na hii inahusu pale tu watu wanaposema habari za udhaifu wa mtu. Wannapomsema kwa mazuri, hilo ni jambo zuri kabisa!

Miriamu na Haruni waliutazama udhaifu wa Musa na wakautumia huo kama nyundo! Matokeo yake wanaishia kuitangua huduma aliyopewa. Kwa kuwa wamemwona wa kawaida kuliko wao, wanaiona hata huduma yake ni kawaida kabisa. Na wanasema mbona hata sisi Mungu amesema nasi!

Baada ya kusikia hayo, Musa alifanyaje? Kumbuka, hata kama Musa ni mdogo kwao kiumri, bado ni kiongozi wao. Ni mtu mwenye mamlaka. Umri wao na nafasi zao hazikutakiwa kuwa kigezo cha kufanya hilo walilolifanya. Na hapa ndipo ambapo wengi wetu huwa tunakosea. Inaweza ikawa aliye kiongozi wetu ni mdogo kiumri, hana uzoefu katika majukumu, elimu yake ni ya chini ukilinganisha na ya kwetu, uchumi wake ni wa kipato cha chini ukilinganisha na wa kwetu, na bado akawa na mapungufu mengine mengo. Je, tunamchukuliaje? Bila kujali kama ni kiongozi wa taasisi ya kidini au nyinginezo, wajibu wetu ni kumsaidia atimize majukumu yake vizuri. Maana kila alifanyalo, ikiwa litafanyika vema, litasaidia ustawi wa jamii ambayo hata sisi tumo. Hata kama amekukosea wewe binafsi, kumbuka nafasi yake! Kuna mkono wa Mungu katika nafasi hiyo!

Tutakapoanza kumsema au kumteta, mbali na kuharibu nafsi yake, tutamvnja moyo, na tukumbuke kuwa yeye ni binadamu pia. Wakati mwingine kile tunachodhani ni udhaifu, kumbe tunaweza tusijue Mungu amekusudia nini katika hicho. Tutaangalia vizuri kwa habari za Musa juu ya kumwoa mke kutoka kabila la Kushi. Maana, kwa dhahiri kabisa kulikuwa na mpango wa Mungu katika kulifanya hilo. Kwa bahati mbaya Haruni na Miriamu hawakulijua. Wao walichokijua ni utaratibu tu na baada ya kupandwa na wivu, wakadhani kuwa hiyo ni nyundo watakayoitumia kummaliza Musa. Ukiendelea kuisoma sura hii, utaona kuwa Mungu aliingilia kati na kuwanyoosha. Yule yule waliyekuwa wanamsema, walimwendea na kumwomba radhi wakisema, ”tumefanya kwa upumbavu”. Ninawapogeza Miriamu na Haruni. Hawakuona aibu kukiri na kutubu uovu wao. Hawakujali tena kama huyu ni mdogo au ameoa mke mkushi. Waliinama na kuomba radhi.

Makosa hayafichwi wala kurahisishwa. Ukitaka kupatana na watu uliowakosea, dawa pekee siyo kutunga maelezo ili kosa lisionekana kuwa ni kosa. Dawa ni kuomba radhi. Katika ulimwengu wa roho, mtu anayeomba radhi anaonekana kuwa ni wa pekee na anapanda daraja haraka. Hiki ndicho kilichompandisha daraja Yuda. Hata kama alikuwa wa nne, katika kuzaliwa, na hata kama alikuwa kutoka kwa mke asiyetarajiwa, alikwaa enzi, na hadi leo hii tunazungumza habari za simba wa Yuda, fimbo ya enzi itatokea katika Yuda, n.k.

Hebu chekecha uhusiano wako na Mungu na uhusiano wako watu wanaokuzunguka ukoje. Unapoona mambo hayapo sawa, dawa pekee ni kuomba radhi. Hii inahusika kila mahali, tangu kwenye familia, ndoa, kazini, kwene ajira, na ushirika wa kila aina. MUNGU AKUBARIKI. [emoji2399] Gerson Mgaya.

Sent from my SM-A715F using JamiiForums mobile app
 
LOL! Mistresses part and parcel of our political spectrum
IMG-20201109-WA0008.jpg


Sent from my SM-A715F using JamiiForums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom