Katika kitabu chake(Mirza Qadian) shahadat Quran p27, 28 Roohani khazain volume 6 page 323, 324, Azala Auhaam p31)
Mirza ghulam Qadiani anaeleza hivi: "Mtume wetu ndo wa mwisho na haiwezekani nabbi mgine kujitokeza baada yake"
Mirza wrote this, I sincerely sought for a serious explanation:
"Our prophet is the seal of the prophets and there cannot come another prophet after him."
Kitabu kama hicho huwezi kukikuta kwenye website yao watakua wamesha ki edit au kukiondowa kwasabb Mirza alikata kwamba yeye sio Nabbi muhammad (saw ) ndo Mtume wa mwisho.....sasa maQadiani wanalazimisha kumita nabbi, ili waendelee kuchanganya uislamu na kumdhoifisha Mtume wetu (saw)
1---Wewe elimu yako ni ndogo sana katika dini ya Uisilamu na hiyo ni kasoro uliyonayo , kwanza jifunze dini ndipo uingie kilingeni kuhoji mambo mengine.
2----Roohan khazain ni nini??---- Roohan khazain (Hazina za Roho) ni majalada (volumes) yaliyokusanya vitabu 82 alivyotunga Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad (as). Vitabu vyake vingi vimeandikwa kwa lugha ya kiurdu, Kiajemi na baadhi katika kiarabu.
3-----umenukuu unayoiita tafsiri ya maneno ya Hadhrat Ahmad (as) kutoka katika au vitabu ulivyovitaja hapo juu, cha kushangaza hujaleta maneno halisi ya tafsiri hiyo katika lugha yake ya asili ili tuone kama unavyodai yamenyofolewa au laa au ni ujanja wenu wa KIJAHILI wa kuficha haki, kupotosha na kuwapakazia Waahmadiyya, juu ya yote tuchukue hiyo tafsiri yako (for the sake of discussion) ili tuijengee hoja; umeandika (BILA SHAKA KWA KUNUKUU WAPINZANI WA AHMADIYYA) kwamba Hadhrat Ahmad (as) ameandika:--
" I sincerely sought for serious explanation our prophet is the seak of the prophets and there cannot come another prophet"
Swali ni hili; kama Hadhrat Ahmad (as) yupo sahihi anaposema; " ----there cannot come another prophet after him" (yaani hawezi kuja mtume mwingine baada yake mtume Muhammad saw), je huyo nabii Isa (as) kwa imani yenu akishuka duniani kutoka mbinguni atashuka kama nani ??.
4---Ili kuyaelewa Maneno ya wachamungu mtu anahitaji unyenyekevu mbele ya Allah na sio kiburi na majivuno, marakadhaa Hadhrat Ahmad (as) anaposema haji nabii mwingine maana yake ni kwamba haji nabii mwingine mwenye Sheria mpya minghairi ya Qur'an tukufu kwani Allah mwenyewe anasema ndani ya Qur'an tukufu kwamba watakuja MITUME kusoma/kufundisha aya za Qur'an, sasa wewe huoni kwamba tukichukua hiyo maana yako potofu ya "cannot come another prophet after him" Hadhrat Ahmad (as) atakuwa kaikengeuka Qur'an ??--- kitu ambacho hakiwezekani aslan.
Angalia aya hizi mbili japo zipo nyingi zinazoonyesha Utume unaendelea katika umma wa kiisilamu;
يابنى ادم اما ياتينكم رسل منكم يكصون عليكم ايتي فمن ا تقى و اصلح فلا خوف عليهم و لا هم يحزنون
Yaani; Enyi Wanadamu bila shaka watawafikieni mitume kutoka miongoni mwenu watawaelezeni aya zangu. Basi atakayeogopa na kufanya wema haitakuwa hofu juu yao, wala hawatahuzunika. (7:35)
و من يطغ الله و الرسول فاولءك مع الذين انعم الله عليهم من النبين و الصديقين و السهدء و الصلهين و حسن اولءك رفيقا ذلك الفضل من الله و كفى با الله عليما
Yaani; Na mwenye kumtii Allah na MTUME , basi hao ni miongoni mwa wale aliowaneemesha Allah--- Manabii na masadiki na mashahidi na masalihi ba hao ni marafiki wema. Hivyo ni fadhili itokayo kwa Allah na Allah anatosha kuwa mjuzi. (4:69-70).
Hayo ni madaraja ya kiroho ambayo waisilamu wanaweza kuyapata hapa duniani kwa kumtii Allah na Mtume wake (saw) madaraja hayo ni 1--Unabii, 2--- Usidiq, 3--- Ushahid, 4--- Uswalih. Unabii likiwa daraja #1.
Sasa tuangalie katika kitabu cha Hadhrat Ahmad (as) mwenyewe kilichotafsiriwa katika kiswahili anasemaje, yeye ni nabii au si nabii/mtume??--- hicho kitabu alikiandika mwaka 1905 katika lugha ya kiurdu Title page yake transliteration yake ya kiswahili ni hii; Aiik Ghalati ka Izalah yaani kuondoa kosa moja kipo katika Roohan khazain ya volume 18., kosa lenyewe ni jinsi watu walivyokuwa hawauelewi unabii/utume wake, naye anasema;
"----Naapa kwa yule Mungu aliyenituma, ambaye kumtungia uongo ni kazi ya waliolaaniwa, kwamba Yeye amenituma akinifanya niwe masihi aliyeahidiwa; nami kama ninavyoziamini aya za Qur'an tukufu ndivyo hivyo niuaminivyo bila tofauti hata chembe Wahyi waziwazi wa Mungu ulioniteremkia ambao ukweli wake umeshanidhihirikia kwa bishara zake mfululizo . Nami naweza kuapa kwa kusimama katika kaaba ya kuwa Wahyi mtakatifu uniteremkiao ndio maneno ya Huyu Huyu Mungu aliyewashushia maneno yake Hadhrat Musa na Hadhrat Isa na Hadhrat Muhammad Mteule (saw). Ardhi ikashuhudia kwa ajili yangu na mbingu pia ; kwa ajili hii mbingu ikazungumza kwa ajili yangu na pia ardhi ya kwamba.mimi ni khalifa wa Mwenyezi mungu. Lakini ilikuwa imelazimu kuwa ningekataliwa kwa mujibu wa bishara. Hivyo basi wenye pazia juu ya nyoyo zao hawanikubali, Nami najua kuwa Mwenyezi mungu lazima atanisaidia kama vile alivyoendekea kuwanusuru mitume wake siku zote. Wala hakuna yeyote awezaye kunishinda mimi, kwakuwa hao hawana msaada wa mwenyezi mungu pamoja nao.
Nami popote nilipokana unabii wangu au utume wangu, ni katika maana hiyo tu ya kwamba mimi sikuleta sheria yoyote mpya wala mimi siye nabii wa kujitegemea.
Lakini kwa njia hii ya kuwa nimepata habari za ghaibu kutoka kwa Mwenyezi mungu nikijipatia fadhili za kiroho kutoka kwa mtume wangu nimfuataye --- Muhammad (saw) --- na kwa kupata jina lake na kwasababu ya Wasila wake, mimi ni MTUME na NABII, lakini bila sheria yoyote mpya, Nami sitakana kamwe kuitwa Nabii wa namna hii bali katika maana hiyohiyo Mungu ameniita Nabii na Mtume; wala sikatai hata sasa kuwa kwangu Nabii na Mtume katika maana hii. Na usemi wangu huu:
من نيستم رسول و نياورده ام كتاب
Mimi siye mtume wala sikuleta kitabu, una maana hiyo tu kuwa mimi siye mwenye kuleta sheria mpya.------"
( kitabu "Kuondoa kosa moja" uk 14-15).
Hayo ni sehemu ya tafsiri ya maneno ya Hadhrat Ahmad (as) mwenyewe juu ya unabii na utume wake.
Kitabu hicho kimetafsiriwa katika lugha mbalimbali kuu za dunia.