Uwoga huwa unachangiwa sana na suala la kutojiamini. Hivyo jitahidi kutokuogopa na jione kuwa wewe ni mwanaume na ni wajibu wako ku-express hisia zako kwa yule unayempenda. Usiogope kupigwa kibuti/kukataliwa, hilo ni jambo la kawaida kabisa. Wadada wengine wana tabia ya kukataa mara ya kwanza wanapotongozwa hivyo kibuti cha kwanza huwa ni cha kawaida. Usije ukakataliwa kwa mara ya kwanza ukafikiri huna bahati, unatakiwa kujaribu tena na tena mpaka upate ukweli wa unayempenda kama naye anakupenda au laa. Lakini pia ni kawaida kujikuta hisia zako zinaangukia kwa yule asiyekupenda. Usilazimishe, asiyekupenda achana naye.
Wengine hutuma meseji, lakini sidhani kama njia hii ni muafaka maana inaonyesha wazi hali yako ya kutojiamini ambayo nafikiri wadada wengi hawaifurahii.
Jitose kwa kuongea nao live, utashinda.