Why should I confess?

Why should I confess?

Ngoja niende, nika fanye order ya vidole vya Mrs Pablo 😂😃
ukiwa na B moja tuu navileta mwenyewe 😂😂, Kuna mtu nammanya yeye alikuwa akinunua ticket za ndege huko ticket ya dola 1000 ananunua kwa dola 100 kutwa kujipostisha anapanda ndege , Yani maisha ya watu sio ya kuiga au kutamani kabisa maana hujui behind amepitia nini mpaka kupost post anaishi maisha expensive 😂
 
ukiwa na B moja tuu navileta mwenyewe 😂😂, Kuna mtu nammanya yeye alikuwa akinunua ticket za ndege huko ticket ya dola 1000 ananunua kwa dola 100 kutwa kujipostisha anapanda ndege , Yani maisha ya watu sio ya kuiga au kutamani kabisa maana hujui behind amepitia nini mpaka kupost post anaishi maisha expensive 😂
yaani ana nunua used ticket ili awa rigishie au sija elewa???.

hivyo vidole usi vikate mwenyewe, vina takiwa kukatwa kwa meno ili iwe fair🤣😂
 
Tatizo mmeandika sana Looh,. Hata sijui nimjibu nani nimwache nani😂😂

PMs hazifunguki wakuu, sijui shida ni simu yangu au kwa wote... So siwezi kuwajibuni
 
Nilichojifunza kuhusu jf baada ya hii str watu wenye changamoto za kweli humu huwq hawapati msaada unaostahili maana kwa str hii ya huyu dada na str aliyoleta nafikir ni mwanzoni mwa january kuhusu utapeli unaweza ukajiuliza mara 2 hawa dada zake walikuwa wp mpka akakimbilia huku
Jigine jf id za kike zinawashughulisha sna watu na kimtindo nimemuona mmoja dizaini kama anajutia hv msaada aliotoa
Dah😓😓😓,.
Ila to be honest wakuu hili suala la kutapeliwa kwa jinsi mlivyolichukulia baadhi yenu linaniumiza sana japo mie ni mpuuziaji sana ila inafika kipindi linanikwaza inabidi tu nifunguke,.

Mbona ule uzi niliweka tu japo nipate faraja na wala siku intend mtu yeyote yule anisaidie( Nenda kapitie mwenyewe).. Ni members wenyewe ndio ambao waliniomba Account number hadharani na nikaiweka tena hadharani kabisa watu wakanifuta machozi na niliweka tena shukrani zangu hadharani na majina nikawataja wote Kwasabu sikuexpect kama ingekuwa vile ,. Kwasabu Mie ni mtu ambaye siwezi kukaa na kitu rohoni chochote ninachokipitia huwa naandika labda kama hunifuatiliii na nikwambie tu humu watu wengi sana wananifahamu nje na Jf na wananifahamu kuanzia nyumbani,. Nakofanyia kazi na hata baadhi ya ndugu zangu pia wanawafahamu,. Na sina chochote cha kuficha ndio maana kitu chochote kiwe cha kijinga au cha maana huwa naandika kwa hii hii I'd yangu..

Hizi roho zenu za kwanini na chuki, na wivu wenu ulioshindwa kujificha ndio ambazo zinasababisha hata walio na matatizo washindwe kusaidika🙏🙏.

But mnivumilie nikifika 24yrs naacha kuandika andika, I promise
 
Mm ushauri wangu Hauwezi kuwa Mbali na wengine kaa Mbali na hao marafiki ,sijui Msaada n.k hilo ni Pepo linakuvuta ukae mao karibu ,Mbona Watu wanahama vituko vya kazi wanapata mazingira mapya na wanakuwa vzr ....Wahenga walisema"Usipoziba ufa ,utajenga ukuta"...Hapo ulipofikia ni kama njia panda kuna nafsi inakusukuma utoke afu kuna nafsi yako inayolilia material things ambayo ni vitu vya kupitia...

Tambua Mafanikio hayapimwi kwa vitu vikubwa hata vidogo vidogo mfano Watu wanaokuzunguka,mambo unayoyafanya ukute yanakupishanisha na Watu wazuri sahivi unaweza usione soo,ila baadae Sana utaona kuwa ulikuwa wafanya upuuzi
Thanks🤝
 
Tuendeleee

BAsi buana mdogo wenu nikaanza napendwa pekeyangu,. Mie ni mtu ambaye sio mtokaji kabisa yaani sijawahi kuhudhuria hata mtu wangu wa karibu awe anafanya birthday Party sijui nini mie sijawahi kuhudhuria huwa naagizaga tu zawadi,. Au labda niwe naenda na mama labda kuwe na harudi kitchen party na shughuli kama hizo mama akiniomba nimpeleke ndio huwa tunaenda wote,.
Lakini hawa wadada walinifanya nianze kwenda kwenye party za watu usiku, Yaani utakuta nimekaa tu sina hili wala lile napigiwa simu "Lee kuna namba nimekutumia hapo ya fundi uende akupime gauni Utalivaa Jumamosi kuna party mie nitakuletea kadi na viatu".. Kwa Approach kama hiyo jamani ningeweza kuchomoa kweli? Baasi nikawa naenda na nikifika kule kila mtu atatamani akae na mimi yaani nakeiwa kwelikweli hadi chooni nikitaka kwenda napelekwa😄😄,.


Hawakuishia hapo,. Kuna siku alinipigia simu mmoja akasema nimepita ofisini kwenu nimeambiwa haupo uko wapi nikamwambia sijafika leo niko kwenye graduation ya mdogo wangu,. Akaniuliza tu wa kike au wa kiume nikamwambia wakike akasema nimwelekeze aje na zawadi basi akaja yeye na wenzie tunasherekea pale mda wa kutoka mie nikaondoka na kina mama na wao wakaondoka zao,.

Kuna siku nlikuwaga niko na stress zangu tu wateja walinivuruga sijui akili yangu iliwaza nini nikasema nimpigie huyu mdada tumwite "Tina " nikawa nimeongea nae tu akanotice kama siko sawa akaniambia nakuja kukuchukua,. Hii ndio siku ambayo nilikunywa pombe mwenzenu na nilikuja kustuka asubuhi,. Mama yangu alipiga simu missed calls sijui zaidi ya ngapi hata sikumbuki, dada na baba ndio kabisa maneno ambayo sikuwahi waza kama nitaambiwa na baba yangu basi siku hiyo niliambiwa kwenye meseji... Lakini cha ajabu huyu Tina wala hata hakustuka aliniambia tu Jiandae twende peramiho Hospitali,. Nikafika kule nikakata kadi nikapimwa malaria, na vihoma vingine vingine nikapewa na dawa halafu ndio akaniambia niwapigie simu nyumbani waje Hospitali halafu sisi tuanze kutoka tukutane njiani, Kwa jinsi nlivyokua nimechoka na ile midawa nliyokuwa nayo moto wote ulizimika waliamini tu labda nilizidiwa njiani nikasaidiwa😥😓😂

Story zisiwe nyingi jamani maana scenarios ni zilezile .......
Ila tu Kiukweli ni watu ambao wamekuwa wamenizoea sana naweza kusema wamenizoea kupitiliza na ndio cycle yangu ya sasa,. Na ninaweza kusema wameniharibu mnoo yaani mimi najiona kabisa sio yule Lee ambaye kila mtu anamjua japo najitahidi sana kuficha nyumbani wasigundue chochote,.

Nashindwa namna ya kuwaepuka jamani maana saizi ndio kabisa wananichukulia kama mwenzao tu,. Yaani wananiona mdogo wao kwenye kazi zao Japo sijawahi kufanya nao chochote kibaya zaidi ya Pombe.. Vishawishi vyao vyote niliweza, nimeweza na ninaweza kuvipangua ( Japo hii huwa naamini ni nguvu ya maombi ya mama yangu) .. Maana mda mwingine mmmh


Kwa namna ambavyo naishi nao saizi ni ngumu sana gafla kusema nipotezane nao,. Nimejaribu mbinu zote hadi kubadili namba za simu lakini ilisaidia nini unadhani?,. Watu wanakujua nyumbani hadi nakofanyia kazi zangu.. Natamani kuwatema moja kwa moja lakini kwa upande mwingine jinsi walivyo Supportive naona kama nitapoteza watu wazuri,. Lakini hapohapo nawaza isije wakaniingiza kwenye matatizo ukizingatia ni watu ambao najioneaga aibu hata kusimama nao njiani isije watu wanaoniheshimu wakaniona nao wakanidharau,.
Sijui nifanye nini kwakweli ila ndio hivyo buana

Mwishooo,.
Embu tuone picha zao dada lee....
 
Back
Top Bottom