Tanzania sio nchi yakujifunzia u ceo kwa raia wakigeni basi kama ni hivyo wange promote intetnally.
Ninakuelewa sana
eddy. Ninadhani hoja isingekuwa kwa "Sylvia". Hoja iwe kwamba, nafasi zozote zinapotoka kwa Tanzania, kipaumbele wapewe Watanzania. Maana ayngu kwenye usaili, ashindanishwe na Watanzania hata kama wote kwa maana ya huyo Sylvia na Watanzania hawana uzoefu wala Masters. Ikibainika yeye anasifa kuliko wenzake, apewe hiyo kazi lakini kuwa Mtanzania iwe added advantage.
Lakini pia, ninatamani sana mjadala huu urudi nyuma kwenye viwango vyetu vya elimu. Elimu ya Tz iko chini sana. Vyo vinatoa wahitimu wasiokuwa na uwezo hata wa kuandika barua ya kuomba kazi. Leo hii sasa usijekushangaa huyu mtu unayesema hana hata Master's degree, ukimweka kwenye mzani mmoja na PHD zetu, akawatoa knock out.
Ninashukuru sana kwamba sasa tunaona mifano halisi ya madhara ya kughushi elimu. Ku pika marks za ufaulu kwa misingi ya siasa, kuwaita wakosoaji adui, na kulazimisha watu waseme elimu inapanda wakati iko ICU, kunakuja kututokea puani katika hali halisi ya maisha. Hakuna mtu anayetaka kufanya kazi yake impe maslahi na alipe kodi, atakayekubali kuajiri majuha (ceremonial graduates), wakati kuna watu wanaweza kufanya kazi bila longolongo.
Nainaomba Watz, tukubali kubalidilisha mifumo yetu ya ufanyaji kazi. Uvivu, ujinga na viburi vya kuridhika. Vinatunyima nafasi nyingi za kimataifa. Uwezo mdogo wa matumizi ya ludha za kimataifa ni tatizo kubwa sana kwa graduates wa TZ. Acheni propaganda za kusema eti hakuna sababu ya kujifunza lugha za kimatifa tuenzi kiswahili chetu. Kiswahili ni lugha ya kisiasa na kijamii lakini kamwe haina uwezo wa kumpaisha mtu kisayansi na kitaaluma.
Kwa ufupi tu, mwananchi akitaka kufanay kazi kimataifa, anapashw akuachana kabisa na viwango vya kazi vya maoifisi ya serikali kwa sababu ni bench mark ya failures. Jifunze kazi kwenye private sectors, jifunze utaalam, ubunifu na uadilifu.
Tunahitaji kujiongezea viwango vya ufahamu, uwezo na namna ya kufanya kazi, ili tuweze kushindana wakati serikali itakapoamua kuwapa vipaumbele wananch iwenye uwezo.
CV yake tayari imeshapwaya huwezi linganisha na akina Dr.Kimei.
Kina kimei wako Wangapi Tanzania? Kimei alisoma Mzumbe?
"Dr. Charles S. Kimei is a Managing Director at CRDB Bank Plc and Chairman at Tanzania Bankers Association. Dr. Kimei was previously employed as Director-Economic Research & Policy by Bank of Tanzania.
He received his undergraduate degree from Moscow State University Lomonosov, a graduate degree from Stockholm School of Economics and a doctorate degree from the University of Uppsala."
Wamekutana kweney forum gani na Kimei tukapima na kuona kwamba Sylvia kwenye fani yake amepwaya?
Kimei alianzia wapi?
Nguvu gani aliyotumia Kimei kumpandisha ngazi?
Tunapashwa kufanya nini ili kutengeneza kina Kimei kwa mamilioni?
Kuongeza viwango vya marks kwa watoto waliofeli? Kudumaza private schools? Kulazimisha watu wa praise performances na standards za elimu nchini na kwamba wakikosoa ni adui? Ku politicize elimu bila utashi wa kukubali misingi inayofanya failures, vyo vya juu kutokuwa na uhusiano na soko la ajira duniani? Kulazimisha watu waliochini ya viwango kupewa nafasi ndiyo kutatufanya kutengeneza kina Kimei?
Huko alikosoma kimei, nako wanaongezaga marks ili kudanganya watu ufaulu umepanda?