Why should Magufuli reject Sylvia Mulinge as Vodacom CEO


Pitia sababu za kwa NINI mKenya tu ndiyo anapigiwa kelele NDIYO uje kwenye mjadala.
Hayo maelezo YAKO unaonekana hujapitia huu uzi. Umerudia MAWAZO yoliyokwisha kujibiwa tayari.
 

Mlichofaa kufanya ni kuwanyanyua TTCL na kuwapa nguvu badala ya kuingilia makampuni ya watu. Japo Magufuli naona ameanza kuwanyanyua hao TTCL, juzi kuna mradi nimeomba kwenu huko, ambapo tulikua kwenye ushindani na makampuni mengine na pia TTCL waliomba, ni mradi wa serikali, yaani TTCL waliachiwa washinde moja kwa moja na wakachukua mradi.
Sasa kama wana akili waamke, wasiishie kulialia kama mnavyofanya, maana wanapewa miradi yote ya serikali inayohusiana na teknolojia za malipo. Kuanzia kwa LUKU hadi mifumo ya malipo kwenye hospitali.

Angalia hata wamepewa kandarasi ya DART, sasa wabebwe hivi lakini bado wanashindwa kwa kauli zenu za eti lazima CEO sijui awe mzawa sijui mara hiki mara kile....

Fuata hii habari TTCL kukata tiketi za Udart
 
Huyu mama hajawahi kuwa CEO popote. Hana uzoefu wakuendesha kampuni kubwa kama hiyo na wapo watanzania wenye sifa na ujuzi wa kuendesha hili shirika.

Vodacom iliuza hisa kwa watanzania tunayo haki ya kulinda maslahi ya watanzania. Tukumbuke CEO wa precision air alichotufanya tusijerudia makosa yaleyale.

Pia tuweke kigezo cha mtu kuwa CEO Tanzania lazima awe PHD holder hata kama ni mzungu.

Soma: MD mpya wa Vodacom Tanzania hana Masters degree na aliyetoka hana pia

Soma: Why should Magufuli reject Sylvia Mulinge as Vodacom CEO
 
unaona sasa yaleyale kila siku tunayoyapigia kelele ndio mnaanza kusema,kama unamaliza chuo ukafanya field mbalimbali pindi uendapo kuomba kazi lazima wakwambie lazima uwe na uzoefu kazini sasa unapataje uzoefu wakati ulikuwa unasoma, mkuu mimi huyo mama na mpongeza kuwa ceo hata hivo wa chini yake ndoo anawasimamia uzoefu atapata kazini
 
Hata hao ma ceo hawakuwa na uzoefu wa kuwa ma ceo kabla.
Akili zako za usiku hizi
 
wewevkia
 
Angekuwa mtanzania sawa ila kwa raia wakigeni kujifunzia tanzania hapana. Tusifanye nchi yetu sehemu yakujifunzia. Tumahitaji kulinda maslahi yawatanzania tumenunua hisa tumewekeza fedha zetu. Huyu mama hata hisa moja vodacom hana
 
Tanzania sio nchi yakujifunzia u ceo kwa raia wakigeni basi kama ni hivyo wange promote intetnally.
Wawapromote internally hata kama hamna uwezo! Ongeza juhudi na maarifa!
 

Hajawahi kuwa CEO popote, si ndiyo anakuwa sasa?

Ninatamani ungesema katika nafasi unazofahamu alikuwa nazo, alionyesha failures wapi. Hii bila shaka ingetupa mwanga wa kuchambua uwezo wake na kuona kama anazo sifa za kupanda ngazi ama hana.
 
Hajawahi kuwa CEO popote, si ndiyo anakuwa sasa?

Ninatamani ungesema katika nafasi unazofahamu alikuwa nazo, alionyesha failures wapi. Hii bila shaka ingetupa mwanga wa kuchambua uwezo wake na kuona kama anazo sifa za kupanda ngazi ama hana.
CV yake tayari imeshapwaya huwezi linganisha na akina Dr.Kimei.
 
kazi tunayoweza kuifanya kiufasaha ni ngono,majungu, chuki, ufitini na wivu
 
Tanzania sio nchi yakujifunzia u ceo kwa raia wakigeni basi kama ni hivyo wange promote intetnally.

Ninakuelewa sana eddy. Ninadhani hoja isingekuwa kwa "Sylvia". Hoja iwe kwamba, nafasi zozote zinapotoka kwa Tanzania, kipaumbele wapewe Watanzania. Maana ayngu kwenye usaili, ashindanishwe na Watanzania hata kama wote kwa maana ya huyo Sylvia na Watanzania hawana uzoefu wala Masters. Ikibainika yeye anasifa kuliko wenzake, apewe hiyo kazi lakini kuwa Mtanzania iwe added advantage.

Lakini pia, ninatamani sana mjadala huu urudi nyuma kwenye viwango vyetu vya elimu. Elimu ya Tz iko chini sana. Vyo vinatoa wahitimu wasiokuwa na uwezo hata wa kuandika barua ya kuomba kazi. Leo hii sasa usijekushangaa huyu mtu unayesema hana hata Master's degree, ukimweka kwenye mzani mmoja na PHD zetu, akawatoa knock out.

Ninashukuru sana kwamba sasa tunaona mifano halisi ya madhara ya kughushi elimu. Ku pika marks za ufaulu kwa misingi ya siasa, kuwaita wakosoaji adui, na kulazimisha watu waseme elimu inapanda wakati iko ICU, kunakuja kututokea puani katika hali halisi ya maisha. Hakuna mtu anayetaka kufanya kazi yake impe maslahi na alipe kodi, atakayekubali kuajiri majuha (ceremonial graduates), wakati kuna watu wanaweza kufanya kazi bila longolongo.

Nainaomba Watz, tukubali kubalidilisha mifumo yetu ya ufanyaji kazi. Uvivu, ujinga na viburi vya kuridhika. Vinatunyima nafasi nyingi za kimataifa. Uwezo mdogo wa matumizi ya ludha za kimataifa ni tatizo kubwa sana kwa graduates wa TZ. Acheni propaganda za kusema eti hakuna sababu ya kujifunza lugha za kimatifa tuenzi kiswahili chetu. Kiswahili ni lugha ya kisiasa na kijamii lakini kamwe haina uwezo wa kumpaisha mtu kisayansi na kitaaluma.

Kwa ufupi tu, mwananchi akitaka kufanay kazi kimataifa, anapashw akuachana kabisa na viwango vya kazi vya maoifisi ya serikali kwa sababu ni bench mark ya failures. Jifunze kazi kwenye private sectors, jifunze utaalam, ubunifu na uadilifu.

Tunahitaji kujiongezea viwango vya ufahamu, uwezo na namna ya kufanya kazi, ili tuweze kushindana wakati serikali itakapoamua kuwapa vipaumbele wananch iwenye uwezo.

CV yake tayari imeshapwaya huwezi linganisha na akina Dr.Kimei.


Kina kimei wako Wangapi Tanzania? Kimei alisoma Mzumbe?

"Dr. Charles S. Kimei is a Managing Director at CRDB Bank Plc and Chairman at Tanzania Bankers Association. Dr. Kimei was previously employed as Director-Economic Research & Policy by Bank of Tanzania.

He received his undergraduate degree from Moscow State University Lomonosov, a graduate degree from Stockholm School of Economics and a doctorate degree from the University of Uppsala."

Wamekutana kweney forum gani na Kimei tukapima na kuona kwamba Sylvia kwenye fani yake amepwaya?

Kimei alianzia wapi?

Nguvu gani aliyotumia Kimei kumpandisha ngazi?

Tunapashwa kufanya nini ili kutengeneza kina Kimei kwa mamilioni?

Kuongeza viwango vya marks kwa watoto waliofeli? Kudumaza private schools? Kulazimisha watu wa praise performances na standards za elimu nchini na kwamba wakikosoa ni adui? Ku politicize elimu bila utashi wa kukubali misingi inayofanya failures, vyo vya juu kutokuwa na uhusiano na soko la ajira duniani? Kulazimisha watu waliochini ya viwango kupewa nafasi ndiyo kutatufanya kutengeneza kina Kimei?

Huko alikosoma kimei, nako wanaongezaga marks ili kudanganya watu ufaulu umepanda?
 
Kivipi serikali iingilie masuala ya Uongozi ya sekta binafsi? Au Magufuli naye ni shareholder wa Vodacom Mwenye controlling interest?

Milambo Holdings na Vodacom S.A wametulia, Magufuli anaingiaje hapa?
Iko listed DSE tunahaki ya kuhoji
 
Ufanyike usaili wa wazi kupitia utumishi kama ni competence basi amaweza toka ethiopia brazil au mtanzania. Tusi generalize kuwa watanzania hawawezi. Kwanini asiwe Kadogosa ceo TRL
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…