Unachokisema kingekua na maana kubwa kwa nchi zilizoendelea lakini sio maskini kama Tanzania, nyie hamjafikia hadhi ya nchi yoyote kupoteza muda wake kuiwaza hadi kuwatuma wadukuzi kuja kudukua mawasialiano yenu. Nilishangaa hadi hata radar zetu ndio mnatumia, jameni ina maana tukiingia vitani nanyi, mtategemea radar zetu kuona ndege zetu za kivita.
Kwa sasa bado mpo sana, mruhusu watu waje kufanya kazi bila ubaguzi wenu huo, kampuni za Kitanzania zinaingia gharama sana kuwafuata wageni kuja kufanya kazi kwenu, mnachofaa kufanya ni kuboresha mifumo ya elimu yenu, kujiamini na kujituma, bila ya yote hayo mengine ni makelele tu.