Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
- #21
Ibara 20.-(b) (iii) ninashauri iwekwe wazi na kuondoa utata uliojitokeza hapa kwa kuirekebisha kama ifuatayo:-
"Kutoshiriki kabisa katika shughuli za biashara kwa wakati wote ambao atakuwa mtumishi wa umma."
Ibara 21 (1) ninashauri isomeke kama ifuatavyo:-
"Mtumishi wa umma aliye katika ajira ya kudumu hataruhusiwa kuingia kwenye ajira nyingine ye yote ile yenye ujira wa aina yoyote ile siku za kazi ili kuboresha utendaji wake wa kazi aliyoajiriwa nayo na kutonyima wananchi wengine nafasi ya kuzifanya kazi hizo za muda au kudumu."
Ibara 21(4) ninashauri isomeke kama ifuatavyo:-
"Nafasi ya utumishi kwenye Bodi za wakurugenzi wa taasi wa umma hautazidi vipindi viwili au jumla ya miaka sita kwa kila atakayetunukiwa wadhifa tajwa."
Ninashauri kuongeza Ibara ndogo ya 21 (5) na isomeke kama ifuatavyo:-
"Utumishi wa umma kwenye ujumbe wa kamishina zilizoanishwa ndani ya katiba hii utakuwa wa kipindi kimoja kisichozidi miaka sita."
Ibara ya 24 (5) iongezwe maneno yafuatayo kati ya maneno yafuatayo:- "Mahala walipotokea" na " maoni yao ya kisiasa"
"maeneo wanayoishi"
Ibara Na. 24 (7) (g) ninashauri iongezwe kama ifuatavyo:-
" Ni marufuku kwa mtu kuadhibiwa mara mbili au zaidi kwa kosa lilelile."
Ibara Na. 38 (1) (e) ninashauri isomeke kama ifuatavyo:-
"Kupelekwa mahakamani ndani ya siku mbili za siku za kazi tangu siku aliyokamatwa."
Ibara ndogo ya 39 (3) ninashauri iongezewe maneno yafuatayo mwishoni mwa sentensi hiyo:-
"…….isipokuwa pale ambapo taifa hili kupitia maidhinisho ya bunge letu limeafikiana na mataifa mengineyo kubadilishana watuhumiwa wa makosa ya jinai tu."
Katika Ibara ndgo ya 42 (1) (d) ninashauri iondolewe koma na kuwekwa maneno yafuatyo kama mbadala wake:-
"……………..ikiwa ni pamoja na…….."
Ibara na. 57 irekebishwe kwa kuondoa maneo ya Tanzania bara na kuwekwa Tanganyika kwani hakuna Tanzania bara kama hakuna Tanzania visiwani. Kwa mtazamo mwingine mbadala ni kuwa serikali zilizoungana ni ya Tanganyika na ya Zanzibar sasa hii ya Tanzania bara uhalali wake unatoka wapi kisheria zaidi ya kuwa ni hekalu linaloelea hewani na halina msingi wa kisheria wa kusimamia.
Ibara ya 69 (1) (h) iilipe bunge mamlaka ya kuhakiki teuzi husika kama zimezingatia mahitaji ya husika.
Ibara 69 (1) (k) Kifutwe. Adhabu ya kifo iondolewe kwani inakiuka haki za msingi za kuishi kwa mwanadamu na tangia adhabu hii kutolewa haijaweza kuleta mabadiliko ya tabia za wahalifu wa aina hii.
Ibara 69 (2) Isomeke kwa kupata kibali cha Bunge kwenye utekelezaji wa madraka hayo.
Ninashauri iongezwe Ibara ndogo ya 69 (5) Bunge litakuwa na mamlaka ya kuhakiki na kuidhinisha maamuzi haya kabla ya utekelezaji wake.
Ibara Na. 75 (d) Isomeke ana umri wa miaka 18 badala ya 40 kwa sababu inakinzana na ibara zifuatazo 6 (a), 24 (3), 33 (1), 33 (2) na 34 (2).
Ibara 82 (1) (2) kifutwe hatuhitaji adhabu ya kifo.
Ibara 84 (12) igeuzwe na kuwa zaidi ya nusu ya wabunge wote kulingana na ujumla wao bila ya kuzingatia mahudhurio yao badala ya robo tatu kama ilivyopendekezwa. Inakuwaje kuwa Rais ni nusu ya kura lakini kumwondoa masharti yanakuwa makubwa zaidi?
Tatizo jingine la kuweka masharti makubwa ya kumwonda Raisi madarakani ni kuwa hana uhalali na ndiyo maana anahitaji katiba kumlinda.
Ibara 85 (2) irekebishwe kuhusisha watumishi wite wa umma kunufaika na angalizo hili ili kuondoa aina zote za ubaguzi wa kinyadhifa.