Why the WARIOBA COMMISSION has failed the nation in many ways!

Ibara 20.-(b) (iii) ninashauri iwekwe wazi na kuondoa utata uliojitokeza hapa kwa kuirekebisha kama ifuatayo:-
"Kutoshiriki kabisa katika shughuli za biashara kwa wakati wote ambao atakuwa mtumishi wa umma."

Ibara 21 (1) ninashauri isomeke kama ifuatavyo:-
"Mtumishi wa umma aliye katika ajira ya kudumu hataruhusiwa kuingia kwenye ajira nyingine ye yote ile yenye ujira wa aina yoyote ile siku za kazi ili kuboresha utendaji wake wa kazi aliyoajiriwa nayo na kutonyima wananchi wengine nafasi ya kuzifanya kazi hizo za muda au kudumu."
Ibara 21(4) ninashauri isomeke kama ifuatavyo:-
"Nafasi ya utumishi kwenye Bodi za wakurugenzi wa taasi wa umma hautazidi vipindi viwili au jumla ya miaka sita kwa kila atakayetunukiwa wadhifa tajwa."
Ninashauri kuongeza Ibara ndogo ya 21 (5) na isomeke kama ifuatavyo:-
"Utumishi wa umma kwenye ujumbe wa kamishina zilizoanishwa ndani ya katiba hii utakuwa wa kipindi kimoja kisichozidi miaka sita."
Ibara ya 24 (5) iongezwe maneno yafuatayo kati ya maneno yafuatayo:- "Mahala walipotokea" na " maoni yao ya kisiasa"
"maeneo wanayoishi"
Ibara Na. 24 (7) (g) ninashauri iongezwe kama ifuatavyo:-
" Ni marufuku kwa mtu kuadhibiwa mara mbili au zaidi kwa kosa lilelile."
Ibara Na. 38 (1) (e) ninashauri isomeke kama ifuatavyo:-
"Kupelekwa mahakamani ndani ya siku mbili za siku za kazi tangu siku aliyokamatwa."
Ibara ndogo ya 39 (3) ninashauri iongezewe maneno yafuatayo mwishoni mwa sentensi hiyo:-
"…….isipokuwa pale ambapo taifa hili kupitia maidhinisho ya bunge letu limeafikiana na mataifa mengineyo kubadilishana watuhumiwa wa makosa ya jinai tu."
Katika Ibara ndgo ya 42 (1) (d) ninashauri iondolewe koma na kuwekwa maneno yafuatyo kama mbadala wake:-
"……………..ikiwa ni pamoja na…….."
Ibara na. 57 irekebishwe kwa kuondoa maneo ya Tanzania bara na kuwekwa Tanganyika kwani hakuna Tanzania bara kama hakuna Tanzania visiwani. Kwa mtazamo mwingine mbadala ni kuwa serikali zilizoungana ni ya Tanganyika na ya Zanzibar sasa hii ya Tanzania bara uhalali wake unatoka wapi kisheria zaidi ya kuwa ni hekalu linaloelea hewani na halina msingi wa kisheria wa kusimamia.
Ibara ya 69 (1) (h) iilipe bunge mamlaka ya kuhakiki teuzi husika kama zimezingatia mahitaji ya husika.

Ibara 69 (1) (k) Kifutwe. Adhabu ya kifo iondolewe kwani inakiuka haki za msingi za kuishi kwa mwanadamu na tangia adhabu hii kutolewa haijaweza kuleta mabadiliko ya tabia za wahalifu wa aina hii.
Ibara 69 (2) Isomeke kwa kupata kibali cha Bunge kwenye utekelezaji wa madraka hayo.
Ninashauri iongezwe Ibara ndogo ya 69 (5) Bunge litakuwa na mamlaka ya kuhakiki na kuidhinisha maamuzi haya kabla ya utekelezaji wake.
Ibara Na. 75 (d) Isomeke ana umri wa miaka 18 badala ya 40 kwa sababu inakinzana na ibara zifuatazo 6 (a), 24 (3), 33 (1), 33 (2) na 34 (2).

Ibara 82 (1) (2) kifutwe hatuhitaji adhabu ya kifo.
Ibara 84 (12) igeuzwe na kuwa zaidi ya nusu ya wabunge wote kulingana na ujumla wao bila ya kuzingatia mahudhurio yao badala ya robo tatu kama ilivyopendekezwa. Inakuwaje kuwa Rais ni nusu ya kura lakini kumwondoa masharti yanakuwa makubwa zaidi?

Tatizo jingine la kuweka masharti makubwa ya kumwonda Raisi madarakani ni kuwa hana uhalali na ndiyo maana anahitaji katiba kumlinda.

Ibara 85 (2) irekebishwe kuhusisha watumishi wite wa umma kunufaika na angalizo hili ili kuondoa aina zote za ubaguzi wa kinyadhifa.
 
I understand your frustrations with everything constitutional but because you have candidly admitted ignorance for the first time; I honestly feel you deserve, a little of free constitutional tutorials from me!
I will go as far as saying thanks for the trouble in presenting your facts (the gesture is based on the understanding that you do read), as for giving me a tutorial on the constitution matters i don't know about that even though i am not a dab-hand on the matters.

Reasonably Mr Mtikila had no case at all from the beginning, all he did was exercising his rights as a citizens in questioning his constitutional rights as a political candidate. To think the amount of time he had been given and the chances to challenge the constitution i don't think it will be fair to criticize the government for not being fair on this matter.

Based on the attachment you have included in post #1

Mtikila's built his case based on this constitutional element,

Kwa maana hiyo katiba hipo wazi and clear taratibu za sheria lazima zifuatwe hili zoezi lifanyike, hivyo Mtikila amekuwa akisumbua tu mahakama kwenye hili suala la mgombea binafsi kwa sababu sheria mama hipo very plain


Kwa hiyo from the beggining Mtikila hakuwa na kesi ya kusikilizwa yaani kikubwa hapo kwake ilikuwa kutumia uhuru wake kama raia ku-challenge lakini kesi hakuwa nayo maana hata mahakama inalijua hili ndio maana swala likaamia huku

Mr. Masaju submitted that since the dispute is on articles of the Constitution of the United Republic then the High Court of Tanzania had no jurisdiction to construe it. With all due respect to the learned Deputy
Hayo yote ni kwasababu sheria hipo wazi ni nani mwenye huwezo wa kubadilisha katiba pekee na majority hipi ya bungeni, namna inaweza isiwe sawa lakini ndio katiba inavyosema.


kwa hivyo from the outset it was lobbying matter to the parliamentarians rather than a court issue, as the outcome was clear by law as stated by the constitution.

Now you tell me do you still think we need my uncle who is tired of the current administration too, but has standard four qualification of their time to participate in the process of making the new constitution or should we focus on the right experts sitting in that panel to give us a constitution that makes sure the issue of rights and checks are properly done.

Kwakuwa tunajichanganya wahusika watachukua nafasi hii kuturudishia katiba ambayo itakuwa na pretty much same problems, leo Mkuu wa upelelezi anasema kesi tunazo na ushahidi tunao kisheria DPP ndio mwenye mamlaka kupeleka mahakamani sijui au ndio mwenye kutoa the go ahead. Meaning TAKUKURU is just toothless as they cant prosecute those who are responsible for messing up the economy nor deprive us of our social needs as human-beings of the 21 century, sasa sijui Mkandawire atachangia nini hapa kwenye technical issue hizi za checks kwenye katiba.

Ndio maana wengine tunaona hili suala mmelitoa kwenye vitu ambavyo ni kero kama kuhakikisha accountability na kuanza kutuamishia mpira kwenye masuala ya muungano na other unnecessary calls. Muungano huwepo usiwepo mafisadi watakuwepo tu kama njia zao azija zibwa.
 

Am glad that you have been doing some serious reading (most of our fellas don't as a matter of habit!)and you seem to have made some informative steps ahead! Bravo! Since Mtikila's case is not the main theme of this thread I will keep my opinions to myself. However, I would like you to comment on whether the House had powers to pass a constitutional amending act under the current constitution and based on the A.G v. Mtikila (supra) ruling by the Appeals Court.
 

Ibara ya 78 ( 1) inapingana na Ibara ya 6 ambayo imeweka hatma ya nchi hii mikononi mwa raia wakati Ibara ya 78 (1) inawanyang'anya raia haki ya kuhoji matokeo ya uraisi sasa watakuwaje walinzi wa demokrasia kama wananyanganywa haki hii ya msingi kabisa?

 
Ibara ya 78 (1) pia inagongana na Ibara ya 52 kama inavyojionyesha hapa:-



Haki ya kuhoji mahakamani matokeo ya Uraisi haiwezi kuachiwa wagombea pekaa na kuacha kuheshimu haki ya mpigakura tukiruhusu hivyo basi uwajibikaji kwenye chaguzi zetu utaporomoka sana maana wagombea wanaweza kukubaliana kubeza haki ya wapigakura kwa manufaa yao na wapigakura wakaachwa solemba. Sijaona sababu ya Ibara 78 (1) kuwekwa jinsi ilivyowekwa zaidi ya kulinda ufisadi na tume yenyewe imefurika mafisadi kawahiyo hakuna la kushangaza hapo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 

haki zote zilizotolewa na Ibara hii ya 33 zinaporwa na Ibara 78 (1)!!!!!!!!!!!
 

Inapokuja kumwadibisha mbunge tume haina noma kwa wapigakura kufanya hivyo kama Ibara hii ya 124 inavyoelekeza sasa inakuwaje iwe noma kwa mpigakura kuhoji na kumwaibisha Raisi ambaye ameingia mdarakani kinyume na matakwa ya katiba hii?
 

Inapokuja kumwadibisha mbunge tume haina noma kwa wapigakura kufanya hivyo kama Ibara hii ya 124 inavyoelekeza sasa inakuwaje iwe noma kwa mpigakura kuhoji na kumwadibisha Raisi ambaye ameingia mdarakani kinyume na matakwa ya katiba hii?
 

Ibara 128 (3) na 128 (4) zina migongano mikubwa mbali ya mwingiliano wa mihimili miwili ya serikali. Raisi anatoka wapi na mali za Spika kama vile Spika anatoka wapi na mali za Raisi kama lengo siyo kudhalilishana?

Pili Raisi anatoka wapi kuingilia shughuli za Tume huru ya maadili ya viongozi?

Ushauri: Ibara ya 128 (4) ni yakufuta ili kuondoa migongano tajwa.
 

Ibara 128 (3) na 128 (4) zina migongano mikubwa mbali ya mwingiliano wa mihimili miwili ya serikali. Raisi anatoka wapi na mali za Spika kama vile Spika anatoka wapi na mali za Raisi kama lengo siyo kudhalilishana?

Pili Raisi anatoka wapi kuingilia shughuli za Tume huru ya maadili ya viongozi?

Ushauri: Ibara ya 128 (4) ni yakufuta ili kuondoa migongano tajwa.
 


Ibara ya 125 (2) (c) ni y kuiondoa kwa sababu inakinzana au kuingiliana na ile ya Ibara 125 (1) (c).

Kubwa zaidi ni kuwa Bunge siyo kazi yao kujitungia sheria wazitakazo bila kuwekewa maangalizo kwenye katiba juu ya viwango vya kufungua mashitaka viwe sawa na kesi za kawaida za madai badala ya kujirundikia Tshs 5.0 mill ili kuwazuia wapigakura kudai haki yao ya kimsingi.

Pia ni jukumu la katiba kuweka wazi kuwa wapigakura ndiyo wenye haki ya kimsingi ya kulinda uhalali wa matokeo ya chaguzi za maeneo ambayo wameshiriki sasa hii rasimu ilichofanya ni kuwaachia wabunge ambao wana masilahi mazito kwenda kujipimia sheria wazitakazo ili waweze kujenga mazingira magumu ya wapigakura kudaia haki yao ya kimsingi.

Tume haikufanya utafiti wa kujua kwanini kuna "voter apathy" inayozidi kukua hapa nchini ni kutokana na mfumo mzima wa kupigakura kugubikwa na vitendo vya wizi na rushwa na kuwafanya wapigakura kukata taama pale waonapo hawana hata haki ya kuhoji kwanini kura waliyoipiga hata haina maana kwani hawawezi kuhoji mahakamani kwa kuzuiwa aidha na katiba au sheria za uchaguzi.

USHAURI: Katiba iweke vigezo vya wapigakura kudai haki yao mahakamani kwenye chaguzi za aina zote, pili ianishe viwango vya kulipia wakati wa kufungua jarada la kesi viwe sawa na vya kesi za madai na tatu muda wa kufungua mashauri ya namna hii uwe wa mwezi mmoja baada ya matokeo kutangazwa na kesi kukamilika ndani ya miezi sita tangia zimefunguliwa.

Haya ni masuala nyeti siyo ya kuwaachia wabunge waende kuyafunika watakavyo.
 

Hii Ibara ya 114 ina misingi mizuri ya uwajibikaji wa Raisi kwa theluthi mbili ya wabunge lakini meno ya wabunge hao theluthi mbili yameng'olewa na Ibara ya 84 (12) kwa kuhitajika robo tatu kumn'goa Raisi madarakani! Khofu ya tume inaelekea ni kwa kufahamau Raisi hana uhalali na ndiyo maana wanamtafutia uhalali kupitia katiba. Khali ya namna hii inatisha wakati uhalali hautokani na wapigakura bali kwa nguvu ya sheria!!!!!!!!!!!!!!!!!!


1) Ibara 84 (12) inakinzana na Ibara 114. Ibara 114 (12) inalipa Bunge kumshinikiza Raisi kupitisha sheria walizozitunga kwa kutumia theluthi mbili ya idadi yao huku Ibara 84 (6) na 84 (12) inawataka wabunge kumwondoa Raisi madarakani lazima wawe na kura za robo tatu yao!!!!!!!!!!!!!!!!!

Inavyoelekea tume inaona uhalali wa Raisi una utata mkubwa ndiyo maana wameonelea wamlinde kwa kutumia katibaa zaidi ya asilimia hamsini ya kura zilizopigwa uhalali wa kulindwa na kura ya kumwondoa iwe robo tatu inatoka wapi kama siyo kufifilisha uwajibikaji eneo la kazi? Ikumbukwe karibu ya zaidi ya asilimi themanini ya ufisadi mkubwa husukwa kutoka Ikulu sasa Raisi akilndwa kulikoni hata anavylindwa na katiba iliyopo tujue vita dhidi ya ufisadi vimeota mbawa.

2) Ibara ya 108 inalizuia Bunge kuingilia kazi za watendaji serikalini lakini Ibara 84 (7) imewapa mamlaka mahakama kuingilia shughuli za bunge kupitia Jaji Mkuu na majaji wengineo! Tatizo ni kuwa uhalali wa uongozi wa Uraisi upo mikononi mwa wabunge na wala siyo mahakama!

USHAURI:-

1) Tume ya uchunguzi iwe inatokana na kamati ya bunge inayohusika na masuala ya katiba na waheshimiwa wa mahakamani wakae mbali siyo kazi yao.

2) LAZIMA MASUALA YA NAMNA HII YA KUHOJI UTENDAJI WA RAISI YAANZIE KWENYE MABUNGE YA ZANZIBAR AU Bunge la Tanganyika kwa zaidi ya nusu ya kura za wabunge wote. Endapo Bunge moajawapo kati ya hayo likapitisha muswada wa kumshitaki Raisi basi hoja hiyo imepita na itasikilizwa na kuamuliwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano chini ya uenyekiti wa Spika wa bunge hilo kwa zaidi ya nusu ya kura za wabunge wote kwa sababu Raisi kaingia madarakani kwa uhali huohuo na aweze kuondolewa kwa uhalali uleule.


 

Hii Ibara ya 114 ina misingi mizuri ya uwajibikaji wa Raisi kwa theluthi mbili ya wabunge lakini meno ya wabunge hao theluthi mbili yameng'olewa na Ibara ya 84 (12) kwa kuhitajika robo tatu kumn'goa Raisi madarakani! Khofu ya tume inaelekea ni kwa kufahamau Raisi hana uhalali na ndiyo maana wanamtafutia uhalali kupitia katiba. Khali ya namna hii inatisha wakati uhalali hautokani na wapigakura bali kwa nguvu ya sheria!!!!!!!!!!!!!!!!!!


1) Ibara 84 (12) inakinzana na Ibara 114. Ibara 114 (12) inalipa Bunge kumshinikiza Raisi kupitisha sheria walizozitunga kwa kutumia theluthi mbili ya idadi yao huku Ibara 84 (6) na 84 (12) inawataka wabunge kumwondoa Raisi madarakani lazima wawe na kura za robo tatu yao!!!!!!!!!!!!!!!!!

Inavyoelekea tume inaona uhalali wa Raisi una utata mkubwa ndiyo maana wameonelea wamlinde kwa kutumia katibaa zaidi ya asilimia hamsini ya kura zilizopigwa uhalali wa kulindwa na kura ya kumwondoa iwe robo tatu inatoka wapi kama siyo kufifilisha uwajibikaji eneo la kazi? Ikumbukwe karibu ya zaidi ya asilimi themanini ya ufisadi mkubwa husukwa kutoka Ikulu sasa Raisi akilndwa kulikoni hata anavylindwa na katiba iliyopo tujue vita dhidi ya ufisadi vimeota mbawa.

2) Ibara ya 108 inalizuia Bunge kuingilia kazi za watendaji serikalini lakini Ibara 84 (7) imewapa mamlaka mahakama kuingilia shughuli za bunge kupitia Jaji Mkuu na majaji wengineo! Tatizo ni kuwa uhalali wa uongozi wa Uraisi upo mikononi mwa wabunge na wala siyo mahakama!

USHAURI:-

1) Tume ya uchunguzi iwe inatokana na kamati ya bunge inayohusika na masuala ya katiba na waheshimiwa wa mahakamani wakae mbali siyo kazi yao.

2) LAZIMA MASUALA YA NAMNA HII YA KUHOJI UTENDAJI WA RAISI YAANZIE KWENYE MABUNGE YA ZANZIBAR AU Bunge la Tanganyika kwa zaidi ya nusu ya kura za wabunge wote. Endapo Bunge moajawapo kati ya hayo likapitisha muswada wa kumshitaki Raisi basi hoja hiyo imepita na itasikilizwa na kuamuliwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano chini ya uenyekiti wa Spika wa bunge hilo kwa zaidi ya nusu ya kura za wabunge wote kwa sababu Raisi kaingia madarakani kwa uhali huohuo na aweze kuondolewa kwa uhalali uleule.


 

Muundo ulioanishwa hapa ni ubabaishaji mkubwa na nafikiriumechangiwa kwa kiasi kikubwa kwa Mwenyekiti wa Tume na Naibu wake kuwa majaji kwahiyo mwamba ngoma huvutia kwake.

Rushwa iliyokithiri kwenye mahakama zetu inahitaji muundo ambao unawahusisha walaji watumiaji wa huduma za mahakama zetu.

USHAURI:-

1) Nafasi za uwakilishi zilizotajwa kwenye Ibara ndgo za c. d. e. na f ziwe mbili badala ya moja na kila nafasi hizo ziwepo uwakilishi wa jinsia zote mbili. Tusipofanya hivyo inawezekana kabisa asiwepo mwanamke kwenye tume hii.

2) Nafasi za uwakilishi kwenye Ibara ndogo ya (g) asipewe Jaji Mkuu kuteua na wasomi wa vyuo vikuu wasiwemo kwani hakuna tija katika kupambana na ufisadi kwa kufanya hivyo. Ninaamini kuwemo kwa Prof. Kabudi kumechangia upotoshaji huu akifikiria yeye na prof. yule wa cdm wamejiwekea ulaji humo!!!!!!!! Nafasi hizo wapewe mashirika yasiyo ya kiserikali na kama ilivyo kwenye pendekezo langu la (1) hapo juu jinsia zote mbili ziwakilishwe. Uwakilishi huu lengo lake ni kuwawakilisha watumiaji wa huduma za mahakama ambao vilio vyao dhuluma huwa vinapuuzwa na majaji ndani ya mahakama.

3) Nafasi zote za uwakilishi tajwa uteuzi wake uzingatie matakwa ya kidemokrasia kwa wale wote wahusika katika ulengwa tajwa wapige kura za wazi ili kuchagua uwakilishi halali na kukwepa uwakilishi haramu.
 


Haya mapendekezo ni "business as usual". Yaani hakuna mabadiliko kwa sababu majaji waliomo ndani ya tume ni nyani wasioona kundule. Wanasema kazi yao ni kupendekeza majina ya majaji wanayatoa wapi? Wanasema kuteua watendaji wengine wa mahakama wanawatoa wapi?

USHAURI:

1) iT IS TIME TO GET SERIOUS WITH NATIONAL BUILDING.............

2) Ajira zote za Idara ya mahakama kama zile za umma zifanyike kwa uwazi, ushindani na shirikishi na mahajiano yafanyike kwa uwazi ya zoezi lolote lile la kusaili majaji kwa kuwapa nafasi wananchi wenye malalamiko kupeleka hati zao kwenye Tume kuhoji sifa za baadhi ya waombaji kusailiwa. Tukifanya hivi asilimia kubwa ya ufisadi ndani ya mahakama zetu utapugnua lakini tukiwaachia wenyewe wajisimamie basi malalamiko yataendelea na uhalali wa dola nao uteaendela kuwa mashakani na itafikia kinga ya Raisi kuondolewa madarakani itabidi tuiongeze ifike 100%. Kwa sababu hataweza kutawala nchi iliyogubikwa na manung'uniko.
 
]

Ajira zote za serikalini zikiwemo za majaji zitangazwe, wenye sifa waombe, wafanyiwe zoezi la kuwasaili ambalo ni wazi na shirikishia kwa umma kwa kuwaruhusu wapeleke hati za viapo kwenye maeneo ambayo hawaridhiki na wasifu wa mwombaji yeyote yule.

Wakati wakupendekeza from nowhere kama ilivyo those days are over..........................na huu utaratibu wa kupeana ugali tena wakati mwingine kwa ngono ufikie kikomo.

Vigezo vya teuzi na mapendekezo haya lazima uwe wazi na sote katika jamii tushiriki maana "it is the wearer of the shoe who knows where it pinches."

Vinginevyo Rasimu hii ni kupoteza muda kama hakuna checks and balances kwenye ufisadi uliokithiri kwenye mahakama zetu...........................again, I say it is time to get serious!
 

huku kupendekezana kimyakimya si ndiko tunako? Lakini tuhuma za ufisadi kwenye mahakama zetu si zimekithir? Huu ubabaishaji ufikia mwisho sasa na uwepo ushindani, uwazi na ukweli na tuondoe usiri ambao ndiyo chanzo cha kulindana na kupeana ngono kama sehemu ya rushwa na majaji kukosa kujiamini kwa kuhofia kutopendekezwa kwa kuzingatia vigezo ambavyo hakuna anayevifahamu.
 

Kweli wazee majaji wastaafu waliomo ndani ya Tume wameamua kulindana! Yawaje wao wajipe upendeleo wa ajira za maisha wakati wengineo wanawawekea ukomo wa ajira kama Raisi, wabunge, CIG n.k?

Kuna uhaja wa kuweka masharti yanayofanana kila mahali maana hakuna ajira bora za utumishi wa umma zinazozidi nyingine.

USHAURI: Nafasi zote za ujaji ziwe za mikataba ya miaka mitano mitano na inapokwisha mhusika aombe na utumishi wake kwisha ufikapo miaka 60 kama watumishi wengineo wa umma. Majaji wasigeuze utumishi wao ni bora zaidi ya wengineo. Tukiruhusu hali hii basi ndiyo tunajenga umangimeza na hakuna uwajibikaji kwani mfumo mzima wa kuwawajibisha majaji unategemea ridhaa yao wenyewe na hawataki walaji wa huduma zao kuwa na hata na chembe ya sauti. Sasa kwa utani utani kama huu ufisadi utakwisha lini?
 


tatizo ya mapendekezo haya kuna usiri wa jinsi ya tume itakavyokuwa inapokea malalamiko ya utendaji wa jaji mtuhumiwa. Hili linachangia sana waathirika na maamuzi batili ya majaji kushindwa kutumia nafasi zilizopo katika kuwadibisha kimaadili na majaji kutumia huo mwanya kutenda maovu yao.

USHAURI:-

Iwepo Ibara ndogo ya kwanza ambayo itaweka bayana namna waathirika na utendaji wa majaji wanavyoweza kufikisha malalamiko yao kwenye tume na jinsi muda ambao tume itautumia katika kuyashughulikia na endapo hawaridhiki na utendaji wa Tume waruhusiwe kuyafikisha mahakamani kuchunguzwa zaidi.

Vita dhidi ya ufisadi wa mahakamani siyo lelemama ya kulinda uozo uliopo hivi sasa kama lengo ndilo hilo hii ni katiba mpya au changa la macho?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…