Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,540
Watanzania tumekumbwa na bumbuwazi baada ya hotuba ya Rais Kikwete bungeni mwishoni mwa mwezi. Ukweli ni kuwa tusishangae tuliloliona au lililotokea, lilipangwa litokee hivyo baada ya sisi "wapiga kelele" kupimwa na kuonekana kuwa Mtanzania kamwe hatachukua hatua zaidi ya kulalamika.
Kosa kubwa tulilolifanya na tunaendela kulifanya ni kudhani kuwa tukiongelea ufisadi kwa nguvu zote, basi mafisadi wataogopa, Serikali itawajibika na CCM itatikisika. Hao tumecheza pata potea na ndio maana hata baada ya kufukua madhambi yote, hakuna hata mtu mmoja aliyefikishwa mahakamani na waliotuhumiwa wote sasa wanatudhihaki kiasi cha kusafishwa majina yao.
Pamoja na alichosema Kingunge majuzi kuwa Wabunge wa CCM wanapotoka kuongelea ufisadi ni kauli ya kijinga na kipumbavu, lakini hiyo ndiyo hali halisi kuwa CCM na Serikali yake, havitishiki wala kuogopa vilio vya wanaodhulumiwa wanaotaka ufisadi ukomeshwe.
Ni udhaifu huo huo kudhani kuwa kuongelea na kuukemea Ufisadi Tanzania tunakokufanya hapa JF na kumbi nyingine, ndiko kutaleta mabadiliko ya kungoa CCM, ndivyo vyama vya upinzani vilivyopotoka na kupoteza miaka 15 kujaribu kuing'oa CCM kwa kauli dhaifu za kulalama na si kuwa na sera za kimaendeleo kumkomboa Mtanzania kutoka kwenye unyonge na umasikini ambao umemfanya aitegemee CCM na kuitumikia huku akidhulumiwa na kudhihakiwa.
Ili kuleta mabadiliko ya kweli na kuing'oa CCM madarakani, inabidi tubadilishe mapigo na mbinu za medani.
Kwanza inabidi tuanze kujijenga kumkomboa Mtanzania awe huru, huru wa mawazo, mwenye kujitegemea na kujivunia mali na ujuzi alionao. Kuna mtu anayejiita WUN humu ndani ambaye amesifia safari hii ya August 2008 kuja Marekani na kusema ni muhimu kuja kutafuta MISAADA!
Tanzania ni nchi tajiri sana, kwa nini bado tunategemea Misaada? Ni lini tutaanza kujitegemea?
Wanasiasa wetu na hasa hawa wa Awamu ya Tatu na ya Nne, wametuingiza katika mfumo wa uchumi huria bila kujiandaa kwa kuwa na uwezo mzuri wa uzalishaji mali hivyo kujenga Taifa linalojitegemea.
Ni udhaifu wao wa Uongozi, Uvivu wa kufikiri na kubuni, Uvivu wa kuchapa kazi na kuwajibika na uzembe ulioandamana na ugoigoi ndio unaolea tabia ya kutegemea Misaada na wengine waje kutuokoa na kutuzalishia mali.
Mwalimu Kichuguu kazungumza vizuri ni jinsi gani Awamu ya Kwanza ilifanya juhudi kujenga Taifa linalojitegemea pamoja na umasikini wa hali na mali tuliokuwa nao na kuachana na bidhaa za kuagiza. Serikali zilizofuatia zimeuza kila kitu kwa jina la Ubepari Uchwara, huku tukiongeza nguvu na juhudi za kuwa ombaomba.
Ni kutokana na tabia ya kuwa tegemezi, ndivyo Mtanzania naye anaiga tembo kutoka Serikali na Wanasiasa wake na kuendekeza unyonge ambao unamfanya awe mjinga na masikini, asiye huru kufikiria na mwepesi kurubiniwa na msaada na takrima na hivyo kuendelea kukubali kuongozwa kwa kuchagua viongozi wabovu na kukitukuza chama kisichojali maslahi na maisha yake.
Hotuba ya Kikwete na kauli ya Kingunge ni vitu tosha kutufundisha kuwa Mafisadi, hawatatikisika mpaka pale ambapo Uhai wa CCM kuendela kuwa chama tawala utakapoingia matatani na mashakani.
Kwa kipindi cha mwaka mzima, hoja kuu hapa JF zimekuwa ni kupiga vita ufisadi. Anza Richmond, rudi IPTL, Rada, Ndege, Kiwira, TRC-TRL, Buzwagi, Karamagi na makontena, EPA, ATCL na mengine mengi ambayo hata ushahidi wa wazi upo, hakuna hata hatua moja imechukuliwa na Serikali na kiongozi mkuu amekaa kimwa huku akihuzunika kwa marafiki na wasaidizi wake wakituhumiwa na wananchi, lakini badala ya huzuni hiyo kuwa ni hasira ya kulaghaiwa na aliowaamini, ni huzuni kuwalinda!
Inabidi tukae chini tutumie akili zetu vizuri na tusikubali kuingizwa mjini tena. Changa la macho limetupwa kwetu mara nyingi na tumeingia kichwa kichwa.
Sina maana tukae kimya kuhusu ufisadi, bali natoa nasaha kuwa tusitegemee kuongelea ufisadi kuwa ndio njia pekee ya kupatikana mabadiliko Tanzania au kushinda uchaguzi.
Hili si kwa JF pekee, ni kwa wote ambao wanataka mabadiliko ya kweli kwa Tanzania!
Tujipange upya na kuanza kujiuliza, ni vipi kwanza tutaweza kumfanya Mtanzania awe huru na kujitegemea?
Siku Mtanzania ni huru, mwenye uwezo wa kufikiri bila kurubuniwa na ana kiburi cha kujitegemea, ndipo siku hiyo ukombozi utawasili na harakati za kuing'oa CCM na kufikisha Ufisadi kwenye sheria zitafanikiwa.
Kama tutashindwa kumpa Mtanzania huyu uhuru na kumjenga ajitegemee, basi ndoto za kuingoa CCM na kubweka kwetu kwa utaalamu kuhusu ufisadi ni kazi bure!
Bob Marley alisema "emancipate yourselves from mental slavery" nami nawaambia wenzangu, "lets emancipate ourselves from mental dependency"!