Mi naweza kusema wanaume wote ni sawa kwa staili hii hapa!!
Jinsi wanavyochukulia swala la mahusiano/mapenzi sio kama wanawake. Na ndio maana haoni shida kukuacha, kukuzalisha na kukuacha tu na maumivu yako. Yani akimua ameamua kwa gharama yoyote ile.
Na hata kama yeye ndo ameachwa na mwanamke haumii kwa muda mrefu kama mwanamke, ni rahisi kusahau mapema na kuendelea na maisha. Tofauti na mwanamke.
Wote hawaoni shida kuwa na wanawake zaidi ya mmoja, labda kama ameshikwa tu na Neema ya mungu na anayo hofu ya Mungu kweli kweli.
Wote ni wajanja na wana mbinu za kuuteka ufahamu wa mwanamke hata kwa ulaghai.
Wote hawapendi kuwa chini ya mwanamke, hata akijitaidi kuna siku atachoka. Wote wanatamani kwa macho yao, na akipata nafasi na akiamua anatimiza tamaa ya macho yake.
Kwa maana hiyo basi hata baba zetu babu zetu, mtoto wa kike lazima ukae naye kwa akili, kwa sababu baba haoni shida kutembea na mwanae kutimiza tamaa ya macho na moyo wake kwa mwanae, achilia mbali housegirl.
Hivyo ndo ninavyofikiria mimi. Kama mwanaume ana upendo atakupenda, kama hana atakuchakachua na kukutupa kule. Wote!!!