M-bongotz
JF-Expert Member
- Jan 7, 2010
- 1,736
- 408
Kwa kweli yamenikuta na sasa naelekea kujuta kumuoa mke huyu.
Ni mke wangu wa ndoa ambaye tunakaribia kutimiza mwaka mmoja wa ndoa japo tuliishi pamoja kwa kipindi cha miaka takribani minne kabla ya ndoa, katika kipindi chote hicho alikuwa ni mwanamke msikivu na mwenye heshima zote kiasi kwamba nikaona nimepata wife material.
Siku zote tulishirikiana kwa kila jambo kuanzia masuala ya kawaida tu hadi yale ya kiuchumi na daima kila tulichonunua tulijua kuwa ni "chetu" bila kujalisha kina jina la nani na hivyo ndivyo ilivyokuwa. Tuliaminiana sana kiasi kwamba mwisho wa mwezi kila mtu alikuwa anaweka mshahara wake mezani na kutafakari ni nini cha kufanyia. Tulifanya kila kitu pamoja na hata wazazi wetu walikuwa wakifarijika sana kuona angalau vijana wao wana mawazo ya kimaendeleo, na si haba kwa kweli tulipiga hatua kubwa sana....hayo yote yalikuwa kabla ya ndoa.
Uhusiano wetu ulijaaliwa kutuletea mtoto, tukaona si vyema kuendelea kuishi kama mahawara tukaamua kuhalalisha mahusiano kwa ndoa takatifu. Siku za mwanzo (japokuwa si nyingi) mambo yalikuwa safi, tuliendeleza maisha yaleyale na zaidi kidogo. Baada ya muda kidogo mwenzangu akaanza kubadilika kidogo kidogo, najua ni jukumu la baba kuhudumia familia yake (traditionally), lakini katika zama hizi nadhani maisha ni kusaidiana hususani kama wote mna kipato, basi tofauti na zamani, sasa hivi si kwamba tu ule mshahara wake unafanywa siri kubwa bali hataki kununua si kitunguu wala diapers za mtoto, worse ni kwamba niliona nimuepushe na adha ya usafiri nikamnunulia ka-gari tena very fuel efficient lakini licha ya kwamba ana mshahara na posho kibao lakini lazima hela ya fuel nitoe mimi, tena kabla sijasahau..,juzi juzi alinijia na mpya tena kwa macho makavu kabisa akitaka eti kila tunachonunua tuandike majina yetu wote wawili.,nikamwambia sema tu hata kama unataka nikuandikie urithi kabisa ( I think she is greedy and miser) kibaya zaidi ni kuwa anapenda mashindano na mimi, anapenda ku-argue kwa kitu ambacho kama angesema "samahani" maisha yangeendelea tu, kifupi ni kwamba amesahau nafasi yake ndani ya nyumba na anajaribu kujifanya yeye ndio baba na kutaka kunigeuza kuwa mtoto.
Ndugu zangu hebu nisaidieni,nyie wengine mliooa wake zenu pia wapo hivyo?.,kina dada ni kwanini baadhi yenu wanakuwa kama vinyonga, wakati wa uchumba wanakuwa wema kweli lakini wakiigia kwenye ndoa they reveal their true colors?i
UPDATES
Jana asubuhi aliniomba pesa ya fuel na lunch wakati anakwenda job,kwa kuwa sikuwa na hela ya kutosha na mimi gari yangu inataka fuel nikataka nimpe ATM card yangu akachukue hela (ATM ipo jirani tu na nyumbani) akakataa na ikawa ugomvi nikaona isiwe tabu nikampa 10,000 aweke hata lita 5 then mchana akatoe hela kwenye account yake.
Hilo lilikuwa kosa kubwa,toka jana jioni aliporudi home amenuna na usiku akaamua kulala chumba kingine leo asubuhi amekuja chumbani kunidai pesa aliyonunulia keki ya birthday ya baba yangu na hela aliyomtumia bibi yangu juzi hapa kwenye sikukuu ya Idd.