Wife kanibadilikia, msaada pls

Mkuu mimi sisemi kitu,kwangu ndio usisema ila navumilia tu.mpaka sasa najiandaa kumuachia kila kitu nianze maisha upya.hatufunga ndoa,tuna watoto wawili.
 
Mkuu mimi sisemi kitu,kwangu ndio usisema ila navumilia tu.mpaka sasa najiandaa kumuachia kila kitu nianze maisha upya.hatufunga ndoa,tuna watoto wawili.
Ha! ha! ha! ha! ha! ha! ha! ha! ha! ha! ha! ha! ha! ha! ha! ha! ha! ha! ha! ha! ha! ha!
 

Umesema kweli (in red) hapo ndipo wanaume tunapokoseaga!
 
pole sn ndugu,naumia sana kuona watu wanachezea ndoa na wakati wengine tunalilia ndoa.Anyway maisha ya ndoa ni msalaba mzito sana hivyo busara ni ya muhimu,jaribu kuongea nae mayb atajirekebisha.
 
Nikwambie kitu?

Wewe ni mume dhaifu..........

Yaani mke anafanya kazi, bado unamwekea fedha ya mafuta na lunch juu? Wewe umekuwa mume wake au baba yake?

Inabidi saa nyingine uwe bandidu ili kuzuia hiyo hali.....(sikwambii usimhudumie mkeo, ila isipitilize)
mfano nikuulize kuna faida gani ya yeye kufanya kazi kama lunch tu anashindwz kujinunulia? Si aache hiyo kazi akae nyumbani ujue moja?

Kosa lako ni kumuoa?

Hebu simama kama mwanaume, si mnasema wanaume ni kichwa? Sasa hebu kuwa kichwa kwenye familia yako, sio kugeuzwa mkia......

Mwambie mkeo kama kashindwa kumanage gari mwambie unaliuza au fanya taxi......
Na mwambie kama ajira anayofanya anashindwa kujininulia chakula ana option 2, moja kuacha kazi, au ya pili abebe chakula toka nyumbani.....

Utakapojua nafasi yako kama mume utasimamia nyumba yako...la sivyo ipo siku utaambiwa lala sebleni kuna mume mwenzio kaja......

Ukishindwz mtagutie nyumba ndogo....(huwa sikubaliani na hili lakini inabidi) ila kwa unyonge wako nina mashaka hata nyumba ndogo itakupelekesha.....

 
Nakushauri kama ni mkristo fanya maombi wote na mshawishi hata mwende sehemu za ibada na maombezi wote. Mimi binafsi nilishikwa na tatizo la kumchukia na kumnunia kila wakati nimuonapo mme wangu. Nilimfanyia visa vya kwako ni vya kitoto...nakumbuka nilikuwa sipendi hiyo hali lakini nikawa siwezi kujizuia. Mwishowe nikaanza kusoma vitabu vya mungu na kwenda kwenye vipindi vya dini. Mpaka sasa tatizo langu limekwisha na bado kila siku najishangaa nilipatwa na nini. Mvumilie mkeo ukiendelea kutafuta ufumbuzi
 
Kama ulimuoa kutokana na mapenzi na sio circumstances itakuwia rahisi sana kumuweka kwenye mstari..
Tofauti na hapo utainvest a lot of energy na personalities with poor outcomes..!!
 

Achana na habari ya maombi bana....

Natamani ningempata mwanamke mwenye akili ndogo kama huyu.....ningekuwa jela tayari natumikia kifungo cha maisha....

Bahati nzuri mungu kanipa mwenye kusoma alama za nyakati,hanisumbui.....nafikiri keshajua humu kichwani mwangu sio kuzima,anaweza akazimwa muda wowote.........

nayafurahia maisha ya ndoa.....
The Magnificient...
 
Last edited by a moderator:
Si bora hela ya mafuta? Mwenzio anampa hadi hela ya lunch.....
In short jamaa ni dhaifu katika kusimamia nyumba yake, hawezi kutoa maamuzi.....

Laiti kama mie ningekuwa mume wa huyo dada... Mida hii gari ingekuwa taxi...na kama haifai kuwa taxi ningempokonya tu..... Apande dalaldala...wiki moja tu angejua kujaza maguta....

Na hela ya lunch angeisikia kwenye bomba, na kama hatuna mtoto ninhekuwa narudi home nimeshibaje sasa?

Na senti tano yangu asingeiona mpaka ajirekebishe....

Maana mwanamke wa namna hiyo kesho na keshokutwa atakusaidia kweli? Mmmmmmmh

Kwa nini unampa ela ya mafuta na yeye ana kazi yake? Usipompa hataenda kazini??? Au atakunyima??? Mnawaendekeza wenyewe...wakikomaa mnakuja kulalamika humu..
 

Ni kweli wengi tuna kero kibao za wake zetu. Wengine hadi kupata unyumba ni tatizo. Hawa wanawake ni noma! Hapo bado wanadai haki sawa kwa wote.
 
Ukishaona mwanamke hataki kuhudumia familia yake mwenyewe ujue anahudumia pengine.

Tena mwanae wa kumzaa ashindwe kumnunulia diapers na nguo ili mwanenu apendeze ni hatari! Mwanamke mwema hutumia fedha zake kwa ajili ya familia yake sawa na njiwa anavojitoa mhanga kuhudumia kinda lake.

Wewe ni baba kaa nae mpe ultimutum; ukiona habadiliki fanya uchunguzi wako taratibu lazima utagundua kitu anajenga somewherer huyo.

Nakushauri usimdekeze kumpa hela za mafuta ya gari wala lunch we hudumia nyumbani atajirudi huyo na wakati unamnyima wala usiongee mengi just do the action.

Unamwendekeza huyo na ameshakusoma madhaifu yako badilika sasa acha kumdekeza
 
Kukaa na mwanamke inabidi utumie akili na busara! '...wanaume kaeni na wake zenu kwa AKILI ...' (1Pt 3:7) 'Mpe heshima mke kama chombo kisicho na nguvu...' kwamba ni chombo weak, kisicho na nguvu, japo sometimes ujitutumua as if kina nguvu. Je ni akili ya namna ili uishi na mke? Za mbayuwayu changanya na za kwako!
 
Hadi hela ya birthday anataka refund, ulimtuma akanunue?
Huyo anaproject anaifanya kwao na kuna mtu kamshika masikio huyo.
 
Duuuhhhh,Na wewe mjukuu unashabikia mangumi? Hata siamini!!
 
Mwambie anataka umfanyie nini ili muishi kwa amani? Muulize kiburi cha nini? Muulize anakufananisha na nani? Kama anapata habari ya wewe kutoka nje ya ndoa akuambie ukweli
 
Hadi hela ya birthday anataka refund, ulimtuma akanunue?
Huyo anaproject anaifanya kwao na kuna mtu kamshika masikio huyo.

ama kweli,wengine tunalilia ndoa wengine wanachezeea ndoa!....bt somtym nguvu za giza zipo
 
Anyway maisha ya ndoa ni msalaba mzito sana

Chief,maisha ya ndoa si msalaba. Ukiyaona maisha ya ndoa kama msalaba,hakika hapo hakuna ndoa. Maana utayaona kama ni mzigo uliokuelemea,mzigo unaopaswa kuutua ili husiendelee kukuchosha.

Maisha ya ndoa ni upendo na kupendana. Huo ndiyo msingi wa mafanikio katika ndoa.
 
Kiswahili chote mfukoni. Hata sijui nichangie nini!

Ngoja kwanza...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…