Pole mdogo wangu! Unajua mambo ya ndoa ni magumu wanayajua walioko kwenye ndoa. Wewe umeolewa? Msamehe bure wifi yako maana hapo alishasoma alama za nyakati? Labda nikuulize hao marafiki zako ni wanawake au wanaume? Ungeenda na marafiki wanaume nadhani haingekuwa shida! Kama ni wanawake lazima alishawasoma kwa kuangalia sura tu na kwa kumfahamu mume wake akaamua awakate maini kabisa, wajuute kumfahamu huyo mgonjwa! Alishaona body languages, usikimbilie kusema kuwa ana dharau. Siajabu mavazi yao, walivyojiremba, walikuwa wanajishaua kiaina, wewe unaweza usione lakini watu wazima tunafahamu. Msamehe buree na fikiria hata wewe ungeweza kufanya vituko hivyo maana sababu si juice kama walivyosema wengine ila kuna mengine. Siku nyingine kaka akiumwa usiende kumwona na kundi la warembo ukijua kabisa wanamzidi wifi kwa urembo na manjonjo, nenda peke yako au na ndugu wa karibu.
Hata mimi wifi wa kuniletea marafiki warembo, wenye vinguo vya siku hizi nido nje nje, skin tight za ajabu ajabu kutwa nyumbani kwangu simtaki. Sitaweza kumwambia live peke yake kwani ataona sijiamini, au simuamini mume wangu, wakati mwingine vitendo vinatumika. Akinielewa niko poa sina kinyongo na mtu.....