Pole mwaya, achana nae, mi naona kakupunguzia mengi, hapo ulitoa mashuka masafi, ungeenda sokoni kumuandalia msosi wa nguvu gharama hizo zote zingekuwa juu yako kutokuja kwake siamekuepushia msongamano
Mungi taratibu
anakutana na wakurugenzi wenzie kwa vikao vya jioni
Kinachomcost David Mataka mpaka leo ni kwenda kwa ndege ya kukodi Musoma wakati wa msiba wa Baba wa Taifa JK Nyerere, halafu yeye na rafiki zake walikuwa hawalali Butiama bali walikuwa wanalala Hotelini Musoma Mjini.Yaani ndugu yangu alifika kabisa hata kwenye gari hakushuka aliishia kunitupia bia za kopo chini.
Kwa mtindo huu hata akirudi kijijini kwa wazazi wake atakataa kulala nyumba ya mama yake ya nyasi kisa yeye ni mkurugenzi? Mambo mengine tuwe tunaangalia na utu kesho na kesho kutwa akistaafishwa ukurugenzi nani watakuwa ndugu zake si ni sisi wenyewe?
Mtu yupo ndani ya gari bia zipo kwenye ctn alikuwa anatoa moja moja na kurusha chini kama angekuwa mstaarabu si angenipa ctn yote kuliko kutoa kopo moja na kutupa mchangani eti mtakunywa hizo mi nimetosheka
Jamani mwenzenu na wifi yangu mke wa kaka angu baada ya kuukwaa Ukurugenzi huko Dodoma ameanza nyodo zilizo pitiliza wakati nilimpokea mwenyewe mjini kaja kujiendeleza kimasomo Chuo kikuu na tulikuwa tunakula dagaa leo hii amepata ukurugenzi anasema hawezi kabisa kufika kwangu anataka alale guest nilipoiy muuliza mbona pakulala nimekuandalia akasema hadhi yake hawezi kabisa kulala kwangu mitaani pale guest bei gani chumba nikamwambia zipo za Tsh.10000-30000/= akasema hakuna guest yenye hadhi ya kulala yeye akaniambia anaenda Sinza kulala kwenye guest za hadhi yake kwakweli ubinadamu kazi jamani.
Achana nae bwana angalia maisha yako siku zote kumbuka ile methari isemayo tenda wema nenda zako,
mbona mwanzo hakuwa akijishebedua kama hivo? !
hawa ndio ukisikia wachawi wanaoroga wenzao. Sasa unakasirika nini? bia kwani hukuzinywa?
Yeye kakerwa na "attitude" nzima, sio kukataa tu, ni namna ya kukataa, na dharu ilio fata. vile alimpa bia bila kushuka kwenye gari etc.Take it easy,it is just a matter of time.Inawezekana na wewe ulimnyanyasa,Hata kama hukumnyanyasa kwani anakupunguzia nini?
Jamani mwenzenu na wifi yangu mke wa kaka angu baada ya kuukwaa Ukurugenzi huko Dodoma ameanza nyodo zilizo pitiliza wakati nilimpokea mwenyewe mjini kaja kujiendeleza kimasomo Chuo kikuu na tulikuwa tunakula dagaa leo hii amepata ukurugenzi anasema hawezi kabisa kufika kwangu anataka alale guest nilipo muuliza mbona pakulala nimekuandalia akasema hadhi yake hawezi kabisa kulala kwangu mitaani pale guest bei gani chumba nikamwambia zipo za Tsh.10000-30000/= akasema hakuna guest yenye hadhi ya kulala yeye akaniambia anaenda Sinza kulala kwenye guest za hadhi yake kwakweli ubinadamu kazi jamani.
Huo uroho wa bia ndio unakuponza. Ushazinywa ndio ukaamua kuja kumkandia hapa? na zile Mpesa na vocha anazokutumia mbona huzisemi?
undugu kazi sana...........mimi binafsi nilisadia ndugu wengi sana na leo wana nafasi zao....sasa hivi waikija dar wanafikia hotelini kwangu hawafiki utasikia tu fulani alikuja dar, hakufika kwako?....mimi huwa sijali na nilipokuwa nawasaidia sikutegemea malio yoyote......mke wangu alikuwa na moyo kama wa huyu mleta mada hapa alikuwa anaumia kweli kuona jamaa hawafiki nyumbani...nikamwambia waache tu maana geti liko wazi wanakaribishwa ila kwa kweli inaudhi kiasi flani......
huyu wifi yako katika maisha yake hakutegema kupata kazi kama hiyo...kwa kifupi hana tabia nzuri hasa hiyo ya kukutupia bia moja moja.....we endelea na kazi zako dada yangu achana nae......