Wifi yangu amezidi

Wifi yangu amezidi

Hongera inaonekana una upendo sana,Mungu akuzidishie zaidi
 
Pole mwaya, achana nae, mi naona kakupunguzia mengi, hapo ulitoa mashuka masafi, ungeenda sokoni kumuandalia msosi wa nguvu gharama hizo zote zingekuwa juu yako kutokuja kwake siamekuepushia msongamano
 
Take it easy,it is just a matter of time.Inawezekana na wewe ulimnyanyasa,Hata kama hukumnyanyasa kwani anakupunguzia nini?
 
Achana nae bwana angalia maisha yako siku zote kumbuka ile methari isemayo tenda wema nenda zako,
mbona mwanzo hakuwa akijishebedua kama hivo? !
 
Pole mwaya, achana nae, mi naona kakupunguzia mengi, hapo ulitoa mashuka masafi, ungeenda sokoni kumuandalia msosi wa nguvu gharama hizo zote zingekuwa juu yako kutokuja kwake siamekuepushia msongamano

Yaani ndugu yangu alifika kabisa hata kwenye gari hakushuka aliishia kunitupia bia za kopo chini.
Kwa mtindo huu hata akirudi kijijini kwa wazazi wake atakataa kulala nyumba ya mama yake ya nyasi kisa yeye ni mkurugenzi? Mambo mengine tuwe tunaangalia na utu kesho na kesho kutwa akistaafishwa ukurugenzi nani watakuwa ndugu zake si ni sisi wenyewe?
 
Mungi taratibu
anakutana na wakurugenzi wenzie kwa vikao vya jioni

Mwenyewe katamka kuwa hadhi yake imepanda. anaishi kulingana na mazingira na nafasi, hata mume atamtafuta anayeendana na hadhi na nafasi yake!
 
Yaani ndugu yangu alifika kabisa hata kwenye gari hakushuka aliishia kunitupia bia za kopo chini.
Kwa mtindo huu hata akirudi kijijini kwa wazazi wake atakataa kulala nyumba ya mama yake ya nyasi kisa yeye ni mkurugenzi? Mambo mengine tuwe tunaangalia na utu kesho na kesho kutwa akistaafishwa ukurugenzi nani watakuwa ndugu zake si ni sisi wenyewe?
Kinachomcost David Mataka mpaka leo ni kwenda kwa ndege ya kukodi Musoma wakati wa msiba wa Baba wa Taifa JK Nyerere, halafu yeye na rafiki zake walikuwa hawalali Butiama bali walikuwa wanalala Hotelini Musoma Mjini.
Watanzania tatizo letu kubwa ni moja, ni ulimbukeni ndio tatizo, kumbe inatakiwa kupanga muda wako wa kuwa na family members na professionals members.
 
Mtu yupo ndani ya gari bia zipo kwenye ctn alikuwa anatoa moja moja na kurusha chini kama angekuwa mstaarabu si angenipa ctn yote kuliko kutoa kopo moja na kutupa mchangani eti mtakunywa hizo mi nimetosheka

Huo uroho wa bia ndio unakuponza. Ushazinywa ndio ukaamua kuja kumkandia hapa? na zile Mpesa na vocha anazokutumia mbona huzisemi?
 
Jamani mwenzenu na wifi yangu mke wa kaka angu baada ya kuukwaa Ukurugenzi huko Dodoma ameanza nyodo zilizo pitiliza wakati nilimpokea mwenyewe mjini kaja kujiendeleza kimasomo Chuo kikuu na tulikuwa tunakula dagaa leo hii amepata ukurugenzi anasema hawezi kabisa kufika kwangu anataka alale guest nilipoiy muuliza mbona pakulala nimekuandalia akasema hadhi yake hawezi kabisa kulala kwangu mitaani pale guest bei gani chumba nikamwambia zipo za Tsh.10000-30000/= akasema hakuna guest yenye hadhi ya kulala yeye akaniambia anaenda Sinza kulala kwenye guest za hadhi yake kwakweli ubinadamu kazi jamani.


Hii kali wanawake mna roho mbaya akiukwaa uwaziri si atakuwa anavaa glove wkt wa kusalimiana.
 
hawa ndio ukisikia wachawi wanaoroga wenzao. Sasa unakasirika nini? bia kwani hukuzinywa?
 
Achana nae bwana angalia maisha yako siku zote kumbuka ile methari isemayo tenda wema nenda zako,
mbona mwanzo hakuwa akijishebedua kama hivo? !

Sipati picha huyo mmewe kama kazidiwa kipato na huyu mama.
 
Take it easy,it is just a matter of time.Inawezekana na wewe ulimnyanyasa,Hata kama hukumnyanyasa kwani anakupunguzia nini?
Yeye kakerwa na "attitude" nzima, sio kukataa tu, ni namna ya kukataa, na dharu ilio fata. vile alimpa bia bila kushuka kwenye gari etc.
But as you say vitu vingine tuwe tunavichukulia kwa urahisi fulani.
Juliet MS: Sio mume wako, sio mtot wako. Kwanza hata sio kaka yako mwenyewe, ni wifi tu.
Mezea, siku mkipata wakati wa kuonana mwambie hukufurahia alivo fanya na yeye akupe sababu za kufanya hivo alafu mrudishe uwifi wenu unapo takiwa kua.
 
lakini usilalamike sana kwa vile mwenzako kawa hivyo hebu jiulize ulazima wa yeye kuja kukunyenyekea uko wapi??/ wakati ule alikuwa anatafuta maisha amepata basi wewe ni daraja la mafanikio yake sasa unataka nae akuvushe??? endelea na maisha yako si lazima afanye utakavyo wewe ... na huna haja ya kulalamika kupewa vitu kama fidia
 
Jamani mwenzenu na wifi yangu mke wa kaka angu baada ya kuukwaa Ukurugenzi huko Dodoma ameanza nyodo zilizo pitiliza wakati nilimpokea mwenyewe mjini kaja kujiendeleza kimasomo Chuo kikuu na tulikuwa tunakula dagaa leo hii amepata ukurugenzi anasema hawezi kabisa kufika kwangu anataka alale guest nilipo muuliza mbona pakulala nimekuandalia akasema hadhi yake hawezi kabisa kulala kwangu mitaani pale guest bei gani chumba nikamwambia zipo za Tsh.10000-30000/= akasema hakuna guest yenye hadhi ya kulala yeye akaniambia anaenda Sinza kulala kwenye guest za hadhi yake kwakweli ubinadamu kazi jamani.

kuwa mpole Dada, asikuumize kichwa anakula pesa yake. kama anakuja kukusalimia inatosha. hilo la kulala lisikuumize. anatumia pesa za mwajili wake, na kama si za mwajili ni zake, hata kama mlikula wote dagaa. kuwa na furaha,ukiona mtu umemsaidia na anaweza kusimama mwenyewe. ila kusema kwako hakuna hadhi nadhani amekurupuka, angeweza kutoa sababu nyingine yoyote.

binafsi nikiwa kikazi silali kwa ndugu, na ninawaambia kuwa nimelipiwa, haina tatizo, ila nakwenda kuwatembelea kuwasalimu. nikiwa na safari ya kuwatembelea wao tu na si kazi, hapo ninalala kwao kwasabau nimekwenda kwao
 
ndo matatizo ya kufuatana mpaka uvunguni hayo. Akila nyama utamwambia mbona tulikula dagaa leo wala nyama. Nyie watu wazima kuepusha vijineno kila mtu akae kwake. Mtakua mnatembeleana tu
 
undugu kazi sana...........mimi binafsi nilisadia ndugu wengi sana na leo wana nafasi zao....sasa hivi wakija dar wanafikia hotelini kwangu hawafiki utasikia tu fulani alikuja dar, hakufika kwako?....mimi huwa sijali na nilipokuwa nawasaidia sikutegemea malio yoyote......mke wangu alikuwa na moyo kama wa huyu mleta mada hapa alikuwa anaumia kweli kuona jamaa hawafiki nyumbani...nikamwambia waache tu maana geti liko wazi wanakaribishwa ila kwa kweli inaudhi kiasi flani......

huyu wifi yako katika maisha yake hakutegema kupata kazi kama hiyo...kwa kifupi hana tabia nzuri hasa hiyo ya kukutupia bia moja moja.....we endelea na kazi zako dada yangu achana nae......
 
Sasa tabu ipo wapi hapo akija kwenye kumi nane zako na wewe mlipue, mimi nilijua kaka yako ndio anakunyanyasa kumbe huyo hamchangii hata damu.
 
undugu kazi sana...........mimi binafsi nilisadia ndugu wengi sana na leo wana nafasi zao....sasa hivi waikija dar wanafikia hotelini kwangu hawafiki utasikia tu fulani alikuja dar, hakufika kwako?....mimi huwa sijali na nilipokuwa nawasaidia sikutegemea malio yoyote......mke wangu alikuwa na moyo kama wa huyu mleta mada hapa alikuwa anaumia kweli kuona jamaa hawafiki nyumbani...nikamwambia waache tu maana geti liko wazi wanakaribishwa ila kwa kweli inaudhi kiasi flani......

huyu wifi yako katika maisha yake hakutegema kupata kazi kama hiyo...kwa kifupi hana tabia nzuri hasa hiyo ya kukutupia bia moja moja.....we endelea na kazi zako dada yangu achana nae......

Si wabongo tukishapata basi hatukumbuki wapi tumetoka tunaangalia mbele tu siku wakikabwa au kuchoka ndo wanakumbuka ndugu wkt ss wanafikia new africa.
 
Back
Top Bottom